Naomba msaada kuhusu utaratibu wa kufanya maombi mapya ya chuo

Shimaje

Member
Apr 12, 2018
84
45
Habari wana JF,

Nina shida kidogo hapa naomba msaada.

Mimi ni muuguzi ngazi ya Diploma sasa mwaka jana nilijiunga na chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kuchukua Bachelor of science in Nursing nikajisajili nikaanza masomo lakini baada ya mwezi mmoja ikanibidi nihairishe mwaka wa masomo kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu.

Kwa sasa nataka nirudi tena masomoni lakini sitaki kurudi tena UDOM nataka niquit kabisa then nifanye application tena niende chuo kingine.

Je, hapa natakiwa kufata procedure gani kujitoa kwenye system za UDOM ili muda wa application ukifika niombe vyuo vingine.
 
Ingawa pia angalizo, kuna diploma holder kibao kitaa wameomba vyuo wamekosa zaid ya miaka 3.

So kama ulioata bahati ya kuchaguliwa mwaka jana baada ya application haina maana mwaka huu tena ikawa bahat yako ukapata nafasi! Fikiria na hilo pia!

Usije ukajutia mbeleni
 
Ingawa pia angalizo, kuna diploma holder kibao kitaa wameomba vyuo wamekosa zaid ya miaka 3...
Poa mkuu mazingira ya UDOM ndo yalinikatisha tamaa asee nadhan vile nili expect chuo kitakua na uhalisia nilivokuta ndo ikanifanya nishindwe kuendelea na masomo kabisa
 
Rudi chuo mkuu, Changamoto kama hizo zinavumilika.
 
Poa mkuu mazingira ya UDOM ndo yalinikatisha tamaa asee nadhan vile nili expect chuo kitakua na uhalisia nilivokuta ndo ikanifanya nishindwe kuendelea na masomo kabisa
Kuna watu wanaililia hiyo nafasi yako mwanzo mwisho, hawajaipata! Nothing comes easy! Piga kitabu mengine yatasomeka mbele ya safari!
#You will thank me later!
 
Mazingira ya UDOM mbona yako sawa tu mkuu, au ulipangwa COED, Kuvuka border Ikawa kipengele, Afy nursing nyie muda mchache mnakuwa UDOM muda mwingi mko Singida huko
 
Elimu ya chuo kikuu ni tofauti na Elimu ya secondary vyuo vyote ni sawa cha msingi ugraduate ukatafute mchongo ukienda Bugando nao watakwambia hapa ni pagumu ukienda St john universiry nako watakwambia pangumu ukija Muhas nako ni pagumu cha msingi tuliza akili baki Udom mwanzoni njia huwa ni ngumu huwa na mabonde na milima lakini ukituliza akili kila kitu kitakuwa sawa
 
Dah sure mzee nilipangwa COED Block B pale.
Singida & Morogoro mnaenda mkifika mwaka wa 3
 
Elimu ya chuo kikuu ni tofauti na Elimu ya secondary vyuo vyote ni sawa cha msingi ugraduate ukatafute mchongo ukienda Bugando nao watakwambia hapa ni pagumu ukienda St john universiry nako watakwambia pangumu ukija Muhas nako ni pagumu cha msingi tuliza akili baki Udom mwanzoni njia huwa ni ngumu huwa na mabonde na milima lakini ukituliza akili kila kitu kitakuwa sawa
Nimekuelewa mkuu ngoja nijipange nirudi tena mwaka huu
 
Kuna watu wanaililia hiyo nafasi yako mwanzo mwisho, hawajaipata! Nothing comes easy! Piga kitabu mengine yatasomeka mbele ya safari!
#You will thank me later!
Sure mkuu niliona kuna wenzangu kadhaa walikosa vyuo round zote.
 
Back
Top Bottom