Msaada wadau: Mchumba wangu ana maambukizi ya VVU

Kapepo

JF-Expert Member
Aug 14, 2015
1,066
1,194
Mimi ni kijana wa umri wa miaka 25 nimepata mpenzi kwakweli tunapendana sana na tumepanga mengi mno juu ya penzi letu, tatizo linakuja hiyu mwenzangu ni muathirika wa VVU sasa nashindwa kuamua nifanyeje hadi hivi sasa nikisema nimchane nitaonekana kumtenga nakumuonea, jamani ushauri wadau.
 
Mimi ni kjna wa umri wa miaka 25 nimepata mpenzi kwakweli tunapendana sana na tumepanga mengi mno juu ya penzi letu tatizo linakuja hiyu mwenzangu ni muathirika wa VVU sasa nashindwa kuamua nifanyeje hadi hivi sasa nikisema nimchane ntaonekana kumtenga nakumuonea jamani ushauri wadau
hapo kukushauri kuna mawili,
1.ukubali kuambukizwa ili muwze kuenjoy tendo vizuri na kupata watoto
2.kutuia condom maisha yenu yote na hamtokaa muzae.......CHAGUA MOJA
 
achana nae, tabia ya kujitoa sana sadaka na kuchukua matatizo ya watu kisa una upendo wa dhati, matokeo yake yanakuja kuwa majuto makubwa sana kwa kuwa watu wana usaliti na ubinafsi sana siku hizi
mpende mwenza wako ila jipende wewe mwenyewe kwanza, ukiona cost ya kuwa na huyo mwenza ni kubwa sana chukua tu uamuzi wa kuachana nae kwa amani
na hawezi kukulaumu kwa kua hayo maambukizi hujampa wewe, huja cheat ila unataka ujilinde
 
Acha vumbi fastaaaa,,,,,,au muonee huruma uje kula midonge kama korosho (ARV)
 
Kumbe wakat unaanza uhusiano nae ulijua ana maambukizi?sasa iweje saivi ubadili mawazo?
Wakati tunaanza nilihisi ananitania ila baada ya kuchunguza sana nimegundua ni kweli kwa kua anatumia dawa namuona
 
Hilo suala nalifahamu sikunyingi sana wala haina haja ya kuelezea sana nayeye anafaham kama nafahamu ana maambukizi hayo
Kwahivyo una asilimia 100% kuwa ana maambukizi basi,kama ni hivyo nenda nae AMREF mpate ushauri nasaha ya namna mtavyoishi..ili asikuambukize. Maana haina maana uanze kumnanga mtoto wa watu wakati umeingia kwenye mahusiano ukijua ana maambukizi..na umeshaiteka akili na moyo. Dhambi kwakweli.
 
Kumbe wakat unaanza uhusiano nae ulijua ana maambukizi?sasa iweje saivi ubadili mawazo?
Wakati tunaanza nilihisi ananitania ila baada ya kuchunguza sana nimegundua ni kweli kwa kua anatumia dawa namuona
Kwahivyo una asilimia 100% kuwa ana maambukizi basi,kama ni hivyo nenda nae AMREF mpate ushauri nasaha ya namna mtavyoishi..ili asikuambukize. Maana haina maana uanze kumnanga mtoto wa watu wakati umeingia kwenye mahusiano ukijua ana maambukizi..na umeshaiteka akili na moyo. Dhambi kwakweli.

Tatizo nalo jingine familia zetu hizi bado hawatambui hilo swala kwakweli sijui naanzia wapi kuweka wazi mambo
 
We endelea nae tu km unampenda kwa dhati, kwani makaburi yote unayoona inamaana ndo ukimwi iliwaua? Na je ukimwacha, huko wewe unakoenda hawaziki? Hakuna kifo? Je kifo kiko kwenye ukimwi tu?
 
Wakati tunaanza nilihisi ananitania ila baada ya kuchunguza sana nimegundua ni kweli kwa kua anatumia dawa namuona

Tatizo nalo jingine familia zetu hizi bado hawatambui hilo swala kwakweli sijui naanzia wapi kuweka wazi mambo
Kama unampenda kwa dhati,ifanye siri hali yake. Mstiri mwenzio for as long as you can. Kisha uende AMREF
 
Back
Top Bottom