Msaada wachawi wamekuja leo kuiba mahindi

Mchawi kaona chakufia nini? We teseka shamba uumwe mgongo afu yeye aje aibe na akukere usiku.
 
Piga moto wa maombi, kama mchawi atasogeza tena pua yake hapo kwenye mahindi...
 
Aisee huenda hawaibi, lakini huwa wanafanya alichoeleza jamaa.

Unasikia tu mahindi yanamiminwa kwenye lisinia krooooooooooo!!

Kama hawaibi basi wanafanya michezo ya mazingaombwe!

Sikuwahi kuelewa mpaka leo! Niliwashuhudia mwenyewe kwa macho yangu!
Hao sio wachawi ni wanga ndio wana michezo ya kitoto ya kulaza watu nje au kukupoteza njia ukalala unatembea mpaka asubuhi
 
Nipo mkoani kuanza maisha mapya takriban mwaka mmoja Sasa . Usiku wa kuamkia leo mida ya saa nane nilistuka usingizini nikasikia pale nilipohifadhi mahindi kwa ajili ya chakula mtu anayachota na kumimina kwenye sinia au ndoo ya chuma au sifuria, sikuamini ikabidi nijipe muda labda nisiwe nipo ndotoni. Ile Hali ikajirudia zaidi ya mara tano ikabidi nimwamshe wife kote huko kutafuta ushahidi kama niko sawa au naota

Naye kumbe alikuwa macho akaniambia anasikia ikabidi tuwashe tochi kufika pale tunapohifadhi mahindi hakuna mtu na mahindi yako kama tuluvoyaacha

Asubuhi ikabidi nimfuate mzee wa makamo nimuulizie kuhusu hili Jambo akaniambia mchawi alikuwa anachota mahindi Ila macho yetu hatuwezi ona kama yamepungua ila tunavyotumia yataisha mapema kuliko tunavotarajia.

Msaada jamani kwa anayefahamu jinsi ya kuzuia mchawi asichote chakula kwenye ghala langu.

Nakaribisha wote wachangie mawazo kwa aliye serious.
Hamisha Gunia weka uvunguni kwa kitanda...kachota kidogo huyo atarudi tuu....
 
Wachawi wameacha kula nyama za watu Sasa wamehamia kwenye mahindi ni jambo jema Sana Asante jpm Asante awamu ya 5
 
Nipo mkoani kuanza maisha mapya takriban mwaka mmoja Sasa . Usiku wa kuamkia leo mida ya saa nane nilistuka usingizini nikasikia pale nilipohifadhi mahindi kwa ajili ya chakula mtu anayachota na kumimina kwenye sinia au ndoo ya chuma au sifuria, sikuamini ikabidi nijipe muda labda nisiwe nipo ndotoni. Ile Hali ikajirudia zaidi ya mara tano ikabidi nimwamshe wife kote huko kutafuta ushahidi kama niko sawa au naota

Naye kumbe alikuwa macho akaniambia anasikia ikabidi tuwashe tochi kufika pale tunapohifadhi mahindi hakuna mtu na mahindi yako kama tuluvoyaacha

Asubuhi ikabidi nimfuate mzee wa makamo nimuulizie kuhusu hili Jambo akaniambia mchawi alikuwa anachota mahindi Ila macho yetu hatuwezi ona kama yamepungua ila tunavyotumia yataisha mapema kuliko tunavotarajia.

Msaada jamani kwa anayefahamu jinsi ya kuzuia mchawi asichote chakula kwenye ghala langu.

Nakaribisha wote wachangie mawazo kwa aliye serious.
We si ulikua kwa mganga Sasa mbona unahitaji msaada kwetu
 
Huku kwetu ukitaka kuanzsha familia hata kama utapanga chumba lazima utafute wataalamu wakufanyie mambo bila hvyo ndoo ya ujazo wa kg 18 za unga utaitumia kwa wiki moja au hata wiki haiishi mkiwa wawili,wewe na mkeo na Mtoto wenu mchanga
 
Benki hawawezi ndugu pesa za benki Zina mazindiko makubwa
Huu ni uongo . Kwanini watu huamini uchawi kiwango hichi
? Umewai kuona bank yoyote ikifanya ayo mazindiko .Barclays bank, BOT, ADB, WORLD BANK.CRDB , NMB ETC.
 
Aisee watu wanaweza kuchukulia hili swala kama la mzaha lakini lina ukweli kwa asilimia zote.

Nikiwa mdogo mdogo niliwahi kushuhudia wachawi wanaiba mahindi wanayamimina kwenye sinia la chuma.

Ni mida ya saa nane za usiku. Walikuwa wanakuja mara kwa mara unasikia tu wanachota mahindi wanayamimina kwenye lisinia fulani (kama ambavyo umeeleza exactly the same way)

Hii wala sio hadithi. Ni kitu nimeshuhudia kwa macho na masikio yangu.

Labda huenda ni mazingaombwe fulani ya nguvu za giza.
Umeshuudia kwa macho na maskio yako?!! Basi nawewe ni mchawi tu
 
samehe mkuu acha akale na watoto wake, njaa mbaya sana.

mi🖐 tena.
 
Aisee watu wanaweza kuchukulia hili swala kama la mzaha lakini lina ukweli kwa asilimia zote.

Nikiwa mdogo mdogo niliwahi kushuhudia wachawi wanaiba mahindi wanayamimina kwenye sinia la chuma.

Ni mida ya saa nane za usiku. Walikuwa wanakuja mara kwa mara unasikia tu wanachota mahindi wanayamimina kwenye lisinia fulani (kama ambavyo umeeleza exactly the same way)

Hii wala sio hadithi. Ni kitu nimeshuhudia kwa macho na masikio yangu.

Labda huenda ni mazingaombwe fulani ya nguvu za giza.
Wachawi wana ujanja wa kuchota mahindi bila kuonekana lakini hawana ujanja wa kuchota bila sauti kusikika?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom