komoakomesha
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 285
- 407
Nipo mkoani kuanza maisha mapya takriban mwaka mmoja Sasa . Usiku wa kuamkia leo mida ya saa nane nilistuka usingizini nikasikia pale nilipohifadhi mahindi kwa ajili ya chakula mtu anayachota na kumimina kwenye sinia au ndoo ya chuma au sifuria, sikuamini ikabidi nijipe muda labda nisiwe nipo ndotoni. Ile Hali ikajirudia zaidi ya mara tano ikabidi nimwamshe wife kote huko kutafuta ushahidi kama niko sawa au naota
Naye kumbe alikuwa macho akaniambia anasikia ikabidi tuwashe tochi kufika pale tunapohifadhi mahindi hakuna mtu na mahindi yako kama tuluvoyaacha
Asubuhi ikabidi nimfuate mzee wa makamo nimuulizie kuhusu hili Jambo akaniambia mchawi alikuwa anachota mahindi Ila macho yetu hatuwezi ona kama yamepungua ila tunavyotumia yataisha mapema kuliko tunavotarajia.
Msaada jamani kwa anayefahamu jinsi ya kuzuia mchawi asichote chakula kwenye ghala langu.
Nakaribisha wote wachangie mawazo kwa aliye serious.