Msaada wa VISA ya Afrika Kusini

Vf-successfully

JF-Expert Member
Oct 25, 2017
253
166
Wana jamvi habari zenu.

Nipo South Africa nina uhitaji wa Visa ya Masomo au ya kazi. Kwa sasa nipo Capetown nina taarifa zisizo kamili kuwa, kuna uwezekano wa kupata Visa bila ya kurudi Bongo upo.

Kati ya taarifa hizo kuwa Oliver Tambo ninao uwezo wa kuipata.

Msaada kwa wenye uzoefu wa Africa Kusini. Asanteni.
 
Fika katika Ubalozi ata kama hawaihusiki utapewa mwongozo au tafuta mtu anafanya wizara ya mambo ya nje au watumie e-mail. WaTz huko South hatuhitaji Visa labda kama ni document nyingine itaje kwa jina lake halisi wadau wakusaidie..
 
Nadhani unaongelea residence permit itakayokuruhusu kuishi na kufanya kazi kwa muda wote.

Idara ya uhamiaji ya SA ndiyo wanatoa hiyo kitu ukiwa huko. Jaribu kutafuta tovuti rasmi yao utapata maelezo kamili.

Ikiwa unahitaji kukaa kwa muda usiozidi miezi mitatau yaani kutembea tu bila kufanya kazi mtanzania huhitaji visa.

Ikiwa ndiyo hivyo huhitaji kufanya kazi lakini unataka kukaa muda zaidi ya miezi mitatu basi siku mbili kabla miezi mitatu haijaisha vuka mpaka nchi jirani kisha rejea. Waweza fanya mara nyingi kila miezi mitatu inapokaribia kuisha.
 
Hii tovuti ya wizara ya mambo ya ndani itakusaidia.

Soma vizuri kwenye temporary na permanent residence permit.

Hii tovuti ya wizara ya mambo ya ndani itakusaidia.

Soma vizuri kwenye temporary na permanent residence permit.

Wakubwa nawaelewa lakini serikali ya Africa kusini siyo kama ya dhamani imebadilika sana hapa juzi kati ilibidi UNHCF waingilie kati kuhusu kuwapa vibali wakimbizi huku wageni hawatakiwi ndo maana juzi kati wakimbizi walikwenda kulala kwenye ofisi za UNHCF ili wasaidiwe. Naninavyo zungumza mpaka sasa bado baadhi yao hawaja pewa asylum seeker. Kwa hiyo hata upande wa Visa wamebana sana hayo yote nimekwisha fwatilia lakini hakuna msaada ndo maana nimekuja humu jamvini kuomba msaada.
 
Back
Top Bottom