Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 103
- 241
Kuna mabadiliko makubwa kwenye sera za Marekani kuhusu utoaji wa visa barani Afrika. Marekani imepunguza idadi ya balozi na ofisi za ubalozi zinazoshughulikia maombi ya visa kutoka 50 hadi 20 pekee. Hatua hii inatajwa kuathiri safari na mahusiano ya kidiplomasia kwa nchi nyingi.
Kwa mujibu wa taarifa, baadhi ya miji barani Afrika itaendelea kutoa huduma za visa.
Miji hiyo ni pamoja na;
Kwenye hili Tanzania imepona licha ya kuwa na mvutano wa Kidiplomasia ni mijadala inayolenga kuangalia upya mahusiano kati ya nchi hizo. Tanzania bado inapita kwenye misukosuko sana ya kimahusiano na uombaji wa Visa Tangu 2025
Kwa mujibu wa taarifa, baadhi ya miji barani Afrika itaendelea kutoa huduma za visa.
Miji hiyo ni pamoja na;
- Abidjan (Côte d’Ivoire),
- Accra (Ghana),
- Addis Ababa (Ethiopia),
- Johannesburg na Cape Town (Afrika Kusini),
- Dakar (Senegal),
- Dar es Salaam (Tanzania),
- Djibouti (Djibouti),
- Kampala (Uganda), Kigali (Rwanda),
- Kinshasa (DRC),
- Lagos (Nigeria),
- Lome (Togo),
- Luanda (Angola),
- Malabo (Equatorial Guinea)
- Monrovia (Liberia)
- Nairobi (Kenya)
- Port Louis (Mauritius)
- Praia (Cabo Verde), na
- Yaounde (Cameroon).
Kwenye hili Tanzania imepona licha ya kuwa na mvutano wa Kidiplomasia ni mijadala inayolenga kuangalia upya mahusiano kati ya nchi hizo. Tanzania bado inapita kwenye misukosuko sana ya kimahusiano na uombaji wa Visa Tangu 2025
- Oktoba 23, 2025, raia wa Tanzania wanaoomba visa ya B1/B2 wanatakiwa kulipa dhamana (bond) ya hadi milioni 39 baada ya tu kukubaliwa kwenye usaili.
- Januari 21, 2026, Marekani ilisitisha utoaji wa visa kwa raia wa nchi zenye idadi kubwa ya watu wanaoamia Marekani kwa kutegemea msaada wa Serikali ya Marekani, ikiwemo Tanzania. Hata hivyo, waombaji bado wanaweza kutuma maombi na kuhudhuria usaili (interviews) kama kawaida.