Msaada wa vifaa vya tv cable station | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa vifaa vya tv cable station

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by KIBURUDISHO, Jul 29, 2011.

 1. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Wakuu hamjambo wote?,naombeni msaada wenu wa kimawazo na pia kiufundi nahitaji kuanzisha mradi wa kusambaza/kugawa chaneli mtaani ni nini ninachohitaji kuwa nacho ili niweze kuikamilisha master control room kwa kuanzia kwanza nahitaji kuwa na chaneli 15 za kuanzia na umbali ninaotarajia kusambaza ni kama kilometa tano. Naomba michango yenu kwa hali na mali ili niweze kulifanikisha zoezi hili.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Booster za ku boost video zako kila baada ya mita kadhaa ni muhimu ingawa mimi sio mtaalam sana wa kitu hii.
  Umejaribu ku google? site za wahindi zina resources hizi.
   
 3. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Kama zipi boss? Nisaidie
   
 4. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Mkuu mm wazo langu linafanana na lako lakni ni tofauti kdogo; nataka kurusha channel za tv kama wanavyofanya Ting, star times; Japo main concern yangu ni channel chache2 za sports burudani na news ambazo nitazitoa bure;
   
 5. Osaba

  Osaba JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 1,725
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sasa unataka kurusha kwa kutumia nini decoder au waya kama wanavyofanya wahindi,kama ni kwa kutumia satelite itakukost kidogo kuanzia kwenye vibali mpaka kwenye mitambo yenyewe ya kurushia
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Wajuzi mwageni maambo hapa watu tufanye maambo
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Binafsi sio mtaalma sana wa haya mambo lakini nimewaji kuyafuailia na kujifunza kwa karibu.

  kama uko serious Kabla hujaanza huu mradi pata muda japo wa kusoma free training . Unaweza kuziapta hata oonline . Kuna video moja niliwai i kuktana nayo sikumbuki link yake.

  training yenyewe inaweza kuwa
  • TELECOMMUNICATION
  • RADIO TELECOMMUNICATION
  • etc
  Mafunzo hayo kwa njia ya video yatakusaidia
  • Kujua Teknolojia mbali mbali na uzuri na na mpungufu yake eg digital Vs analog , spectrum , Transmission . Mfano ukisoma hapa HowStuffWorks "TV Broadcasts" kuna njia kama nne za mteja kupokea matangazo ya TV je wewe unataka wateja wako wapokee kwa njia gani ( FTA, Cable au Dish)
  • Vifaa tofauti na watengenezaji wa vifaa hivyo na ubora , uwezo na kikomo chake
  • Standard utazotakiwa kutumia na mamlaka zinazohusika na eg TCRA, Manispaa etc

  Otherwise kifupi soma maelezo haya

   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Mtazamaji hebu tumia mifano hai

  mfano tv kama clouds tv hivi

  teknolojia pale ni ipi?gharama za vifaa?
  Hapa bongo makampuni gani yanaweza kuwa na ujuzi na gharama nafuu?????
   
 9. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Sijui kama nimemsoma vizuri vizri huyu jamaa yeye anasema anataka kusambaza . So ina maana project yake ni complex kidogo kwa uelewa wangu. Ingekuwa antaka kurusha tu matangazo free to air ( FTA) kama TVT, ITV. ni rahisi kidogo. Akisema kusambza maana yake anataka kuwa na kama ka DSTV version kake.

  Kuhuusu gharama sijui na sina data wa kweli nimewahi kujifunza technical side ya television wakati nataka kujua uwezekano wa kuchakachua DSTV. Nilifanikiwa kwa siku chache lakini walivyobadilisha encryprion ndo basi.

  kwa uelewa wangu mdogo Nadhani kuwa na station iwe na radio au TV cha kwanza uchohitaji ni Transimitter. hii ni assumpation kuwa TCRA hatakupa vikwazo na masafa yatakuwepo. Sasa uwezo wa trasmiter inategemea pia aina ya kituo chako. Then kuna vitu kama amplifier. Vituo vingi karibu vyote vya radio na televion vina amplifier na retrasmiter station zao Kisarawe. Kama havina hata kusikika darzima ni kazi.

  Kwa huyu jamaa anayoonekana satelite is not an option kwake hata ingekuwa ni option nadhani gharaa yek ni kubwa sana.

  Kama akiamua yeye wateja wake watapata matangazo kwa cable requirement na vifaa atavyohitaji vinaweza kubadilika na may be gharama.

  TV kama , TVT, startv ITV Clouds ni free to air channel . na hizi zote kuna sehemu kule kisarawe zina maeneo. Sababu wameamua kurusha matanagazo yao through air na wanahitaji yaende mbali zaidi inabidi pia wawe na vituo vya kuamplify.( Sina uhakika na clouds kama Nao wana kituo kisarawe)

  Anywa siku nyingi nimekula hii shule naweza kuwa nimekosea anyone might correct me.
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mkuu trannsmitter bai zake zikoje?
  hapa bongo zinauzwa?
  brand za transsimiteer ziko vipi?
  na amplifier brand zipo vipi?
  bei zake?
   
 11. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Nope, stak kutumia cable kama za wahindi, nataka wirelessly; is there a way of transmiting video without involving the satelite? Ni ndani ya kma 7km radius! msaada tafadhali.
   
 12. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Naomba nitoe ufafanuzi kiasi tena!
  Channels nazotaka kurusha ni kama 10 tu, na kati y hizo channel 7 zinawezakuwa selection ya channels za muhimu kwa locla news, international news, sports na entertainment; then zile 3 zinazobaki ni channels zangu maalum ambazo zitakua na contents ambazo upatkanaji wake ni sharti mtu alipie (you can watch the 7 channels for free, remember). Kwa mawazo yangu ya bei rahisi ni kuwa nakituo cha kurushia ambacho kitakuwa hookedup na hzo channels7, nachofanya ni ku-retransmit the selected channels+my3 channels, na kwa receiving end "anakuwa" na decorder ambayo inamruhusu kuona 7 channels free, lakn anapotaka kufungua the rest3 channels zinarequest code (leave alone the "coding"). Nilifikiria kuhusu suala la cable lakn nikaona kama kunakuwa na gharama kubwa za miundombinu; hata hivyo si mbaya kama wataalamu watasugest hii, na means ya kumrestrict viewer kkuaccess content pale tu anapokuwa na code!!!!! (kwa hili nawezapia kuongea na mtu aliyeko tayari established na cable network kwa maelewano yakukodisha hizo channel3 tu-japo mmbongo akiona unamake zaidi next year anakunyima kataba!!)
   
 13. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  amoeba labda wewe una vifaa gani tayari?
  au umepanga bajeti ya kiasi gani?
  na hizo trannsmitter umeshapata?
   
 15. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Mkuu,mm bado niko ha2a za mwanzo kabisa! anajaribu kufanya hesabu za mradi mzima na cost zake ili nione kama itanilipa; nataka nifanye kitu tofauti kidogo kaka! vp ww?
   
 16. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #16
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Boss wakati unabsuiri jibu la watalaama tembela hapa Digital Transmitter Price, Digital Translator Price. na wasome hawa pia http://www.thomson-broadcast.com/products/tv-transmission/elite-digital-tv-transmitter-family-0. Unaweza upata picha but hope wachina wanaweza kuwa wanatengeza trasmiter na vifaa vinge bora na nafuu. zaidi

  Nimesahau nanilikuwa mchovu wa mahesabu kidogo lakini nadhani kwa kujua ukubwa XXwatss unaweza kukadiria transmitter itarusha umbali gani. Watts ni kipimo cha power.

  Assuming kuwa hakuna vikwazo vya inteference na obstacle eg milima kati ya trasmiter na na maeneo yanayokusudiwa kupokea matangazo unaweza unaweza kujua ni tramsiter yenye nguvu gani utahitaji

  NB
  Mpaka hapo nikurusha matangazo ya bure tu kama ITV na TVT kama unataka wapokeaji walipe then cable ndio solution nafuu kuliko satelite.
   
 17. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #17
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Sijakusoma vzr hapo kwenye red mkuu, nafuuni ipi kama ninataka wapokeaji walipe?
  edit: nadhani ulimaanisha cable ni solution rahisi kuliko satellite! kama ndy hvyo, toa mawazo yako; kule kwa mpokeaji nitawezaje kumpa channel 7 bure na 3 kulipia?
   
 18. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #18
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nimechapia kimaandishi lakini nisharekebisha teh teh teh.
   
 19. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #19
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Jamani labda sikueleweka vizuri chaneli ninazohitaji kusambaza kwa njia ya cable ni za FTA kwa mfano chaneli zote unazopata kutoka kwenye ungo wako sasa uzisambaze mtaani kwa njia ya cable ili mteja awe anakuja kulipia ofisini asipolipia unamsitishia huduma hiyo kwa urahisi.Sasa ni njia gani na vifaa vipi nitakavyoitumia ili chaneli hizo ziwezekupatikana ktk mfumo wa VHFau UHF???
   
 20. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #20
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu nadhani hiyo utahitaji kuwapa decoder box wateja wako. Channel za bure haziwi encrypted So hata kama hjalipa montly charge zitaflow tu na taziona tu tu lakini channnel za kulipia zinakuwa encrypted na protocol na idadi ya siku kadi ifanye ya denctyption inakuwa kwenye ile card. Zikiisha siku alizolipia kadi ina disabale decrpytion channel za kulipia. ( Yaaani mfumo wa malipo kama wa DSTV decoder)

  But ecryption/ decryption ni system nyingine tena alafu ni complex na kwa bongo nadhani wengine tutaweza kukuchaua labda utumie teknolojia kali sana ambayo itakugharimu sana

  But ngoja wataalam waliobobea waje washushe maujuzi yao
   
Loading...