Msaada wa msamiati wa neno mukhtadha

Muktadha=Mazingira.
Mf. Muktadha wa Wa eneo lile sio mzuri
Pia katika ujengaji hoja na hata matumizi ya lugha. Kwa mfano kama sentensi ina utata kwa mfano:

"Juma alimpiga John kwa sababu alikuwa amelewa."

Ili kujua ni yupi aliyekuwa amelewa tunategemea muktadha (context) wa mazungumzo.

Au utasikia "Katika muktadha huo basi hoja yako inakosa msingi kabisa"
 
Screenshot_20210218-210555.png
 
Muktadha=Mazingira.
Mf. Muktadha wa Wa eneo lile sio mzuri
Ni context.. katika mfano wako neno muktadha haliwezi kutumika.

Lazima kuwe na ulinganifu. Labda kama kungekuwa na hoja ya eneo unalolikusudia kwenye sentensi yako kuwa na mbadala.. basi kutetea hoja yako.. ungeweza kutumia neno muktadha.

Mfano eneo hilo limepangwa kutumika kwa kikao. Ila ushahidi unaonesha lina vurugu, vyoo vyake ni vichafu na hakimiliki kirahisi. Ungeweza sasa kusema.. "kwa muktadha wa usalama na usafi, eneo hili sio zuri.
 
Muktadha ni jumla ya vitu, viumbe na hali inayowezesha uwepo wa tukio ama hali fulani mahususi. Mfano, muktadha wa shuleni ni mjumuiko wa majengo, mwanafunzi, Walimu, yanayopaswa kufunzwa, muda n.k. Zingatia kwamba mazingira siyo muktadha bali ni kijisehemu tu kinachoweza kuunda muktadha. Vivyo hivyo muktadha siyo mazingira.
 
Back
Top Bottom