Msaada wa mawazo

Msaada wa mawazo

Yani mpaka nimecheka utadhani mazuri...kama hataki kuomba msamaha na akijua kabisa bila msamaha hakuna ndoa jueni tu kuwa binti alishabadili mawazo along the way na ameshukuru kwa kupata sababu ya kumpiga jamaa chini...

Ukute hata hiyo message ni ya kupika ili jamaa aachie ngazi...

Bora waachane mapema kuliko kuanza ndoa na ugomvi from day one..

Huwa najiuliza ile ndoa ya Kim K ilodumu muda mfupi ni nini kiliwafanya waoane at first place...? na ukute plausible reason ni kuogopa fedhea kwa kuwa wameshatangaza na miaandalizi yalishafanyika...



kama kupotea ameshapotea,hilo la kuomba msamaha tumeongea mpaka ....yaani sijui ni nini hiki
 
Mna uhakika ni kweli anahusiana na huyo dr? Manake kama nna maswittie kibao naweza kujaza coaster. Ukinilazimisha niombe radhi wakati sio kweli nitagoma pia!
kama kupotea ameshapotea,hilo la kuomba msamaha tumeongea mpaka ....yaani sijui ni nini hiki
 
Nimekumbuka nguvu za giza....teh teh teh...mama yangu alifunga novena kipindi nakaribia kuolewa...mimi nilikuwa namshangaa tu...madai yake you never know kuna watu wanga unashangaa bwana harusi anagoma kuja church...teh teh teh
 
Nimekumbuka nguvu za giza....teh teh teh...mama yangu alifunga novena kipindi nakaribia kuolewa...mimi nilikuwa namshangaa tu...madai yake you never know kuna watu wanga unashangaa bwana harusi anagoma kuja church...teh teh teh

haaahaaaa maisha haya jamani...kweli changamoto nyingi
 
Mna uhakika ni kweli anahusiana na huyo dr? Manake kama nna maswittie kibao naweza kujaza coaster. Ukinilazimisha niombe radhi wakati sio kweli nitagoma pia!

ukweli anaujua mwenyewe...kwetu anakataa hana mahusiano na doc
 
Hiyo sms ni ishara tosha kuwa Dokta hana chake tena kwa huyo Manzi....

Pia mkimlazimisha kuomba msamaha ilhali ni kweli hajatenda kosa, only for the sake of ndoa mtamfanya awe na kinyongo..

Wapeni nafasi wajiamulie wenyewe mustakabali wao, mkilazimisha sana ndoa mjiandae kwa lawama huko mbeleni.
 
Rudisheni tu michango. kama tatizo ni mesej mbona inaonyesha biharusi hana uhusiano na dk? Kama hawaaminiani ni bora kutokuoana. Mwaka juzi nilirudishiwa mchango siku chache kabla ya harusi ya family friend. Maharusi watarajiwa tu ndo wanaojua kisa cha kukimbia kufunga ndoa. Waligoma kata kata kusema kilichowakuta. Leo hii watu wameshasahau.
 
Hiki ni kipindi kigumu sana.....binti aendelee kukataa kuwa hamfahamu lakin aombee msamaha coz imetokea kwenye cm yake na hata yeye mwanaume inaweza mtokea.

Hiyo ndoa ikipeperuka katika misingi hiyo ya binti kuonekana si mwaminifu basi kuolewa kwake itakuwa historia
 
Vaislay hata ufanyeje hauwezi suluhisha hili tatizo kwani kwani hao walengwa hawaitaki suluu! Na tatizo kubwa lipo kwa huyo mdogo wako!

Mapenzi ni uaminifu. Na mdogo wako ameshauondoa! I bet mdogo wako anatenda ndio anafikiri!

Kuwa na mahusiano kabla ya mahusiano sio kosa! Kosa ni kuwa na mahusiano ndani ya mahusiano!

Alipaswa aweke wazi kwamba huyo alikuwa mtu wake, na aeleze kwamba kwa sasa hana time nae thus why jamaa ameleta sms yenye content ya ukumbusho!

Anyway, kwa vile maji yakishamwagika...
Mwambie ajirudi na akubali ujinga, confession ni kitu kibaya, but not always, it depends the circumstance of the case! Mwambie asikariri!

Na ikiwa atakubali na kukonfess now, then akataliwe mtie moyo huyo hana heri naye thus why Mungu kaepusha.
 
Nilikuwa nasoma na kusikia ishu za kina Vicky Kamata lakini leo limefika mikononi...

Mdogo wangu alitaraji kufunga ndoa hivi soon shughuli zoote mnazozijua za maandalizi zilifika ukingoni...
Siku nne zilizopita nilipata simu ya Mume mtarajiwa akiniambia alikuta mesej ya mdogo wangu akitumiwa na daktari aliyemtibu kipindi flani akiwa anaumwa...ikisema " swit mbona umekiwa kimya mda mrefu"
mume akuuliza mke mtaraji kulikoni bibie akachomoa...
mume akaelewa...sasa gafla yule mume kaibuka kusitisha ndoa kwa madai tu hataki kuolea watu...
Ndugu wa familia tumejaribu kuongea na binti amtake radhi mwenzie binti nae kaibuka hataki kosa wanaume anajidai mkoloni..

Vichwa vinasugua na nywele kunyonyoka hatujui hata lakufanya garama zilizotumika kuandaa..michango ya watu yaaaani.....hoooooiiii

nisaidieni mawazo kunusuru hili balaaa...ndoa imebakiza siku chache tu ...

Wanatia hasira. Haya ndo matatizo ya kulazimishana ndoa. Msg kitu gani bana?. Sema watakua wamerushiana maneno hadi mwanaume akaogopa.

Amejiuliza hatujaoana amekua hivi je tukioana. Mara nyingi Midomo michafu na maneno makali ya wanawake yamewafanya wanaume wasifikirie ndoa. Mwanaume anapenda kuona mke wake anamheshimu na kumnyenyekea. Wanaume hawataki wanawake wababe. Inaonekana Mdogo wako kakolea kwa dokta hata mbele haoni. Hata mimi ndoa inaweza vunjika dakika chache kabla ya kuingia kanisani kama hutataka kujishusha.

Tutavumiliana lakini sio maswala ya kuvuana chupi. Nakua mkali sana. utanitukana, nipiga ,nidhalilisha, yaani mambo yote unayo utanifanyia ntachukulia poa. lakini mambo yanayo husu sex tutatoana roho. Yaani upeleke malaya wako kitanda ninacho lalia nivumilie? hapana. mia
 
pole vislay kwa hali hiyo unayopitia ila kumbuka kuwa ndoa ini mpango wa Mungu hivyo
msilazimishe waoane halafu baadaye ije kuwa majuto ni mjukuuu

kama imetokea hivyo mkalishe mdogo wako ongea naye kiundani ujue tatizo liko wapi
kwani hizi simu hiz zinasababisha mambo mengi kuharibika na hususani kama kutatokea
kitu kwa mdogo wako mwambie ajue alichofanya si chema kuwa na mahusiano ndani ya
mahusiano hata Mungu naye anachukizwa na dhambi hiyo kwanini afanye hivyo?

hivi anajua kuwa yeye ni hekalu la Mungu na si vyema kufanya dhambi iilhali umeshajicommit
mahali fulani kwanini anamkwaza mwenzake kiasi hicho? kaa nae ongea naye ujue ukulikoni
 
Kwanza jamaa ni jembe, napenda wanaume wenye msimamo ambao hawayumbishwi ukisema no ni no. Mimi sipendi watu waongo akishaaribu protocol zangu basi imepita, jamaa achane naye huyu mwanamke ni tapeli tuu atakuja kumsumbua.
 
Mnachokifanya nikujaribu kunusuru hadhi ya familiya hakuna lingine.
Katika issue hii kama huyo jamaa alikuwa tayari kuombwa radhi then mambo yaendelee basi mdogo wako alipaswa kufanya haraka,maana kama ningekuwa mimi jamaa mpira ungeishia hapo
Pia mdogo wako atambue ikiwa ndoa itayeyuka na watu wakarejeshewa michango, ndiye atakaye poteza jina lake litanuka.
 
Hatuwezi kulazimisha hapo mkuu kitumbua kimeingia mchanga. Tushukuru shetani kajidhiirisha mapema kabla yakiapo chandoa. Cha msinngi hapo kama wamejijua kwamba hawawezi kuishi pamoja vunjeni kamati tu.

I miss you sana vaislay.
 
ukweli anaujua mwenyewe...kwetu anakataa hana mahusiano na doc

Jamani heri nusu Shari kuliko shari kamili, msiwalazimishe, wapeni muda kusolve hiyo issue ikishindikana rudisheni michango ya watu
 
Nadhani Mwanaume yupo sahihi! Nimeshasema ni Heri kuahirisha safari kuliko kupanda gari bovu. Unaweza ukaoa ukaendelea au ukarudi nyuma! Tafadhali angalien upya Lakini kwa nini Binti ana kiburi??? Ukiona mwanamke anabehave vile jua nyuma yake ana option B. So mtemeni
 
Kwasababu muoaji katoa sababu na ana ushahidi sioni tatizo kufanya maamuzi ya kusitisha ndoa.
Hili swala jaribu kulibeba kama wifi au mdogo wa huyo kaka ndio utajua jinsi inavyo kuwa au vaa viatu vya muoaji halafu ufikirie.

Kwangu amechukua uamuzi wa busara na sahihi.
Pole sana.
 
Back
Top Bottom