Msaada wa maana na sifa za maeneo ya kiutawala!

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,865
5,686
Naulizia vitu hivi hapa wakuu;
1. Halmashauri ya wilaya
2. Halmashauri ya manispaa
3. Halmashauri ya mji
4. Halmashauri ya jiji
5. Maana ya 'halmashauri'

Hili ni jukwaa la kujifunza na kuelimika, naomba nielimishwe kuhusu hoja hizo hapo juu ambazo mpaka sasa nazijua kwa mazoea tu ya kuzitamka basi lkn si kwa kuzichambua.....isitoshe kutoa elimu kwa mtu ni ibada tosha kabisa kwa Muumba, yaani Mola.

Ahsanteni na mbarikiwe sana!
 
Halmashauri (kutoka neno la Kiarabu) ni kikundi cha watu ambao wamechaguliwa au kuteuliwa wafanye kazi ya kuongoza, kutawala, kutunga sheria, kushauri na kuelekeza mambo.

Pia ni chombo cha kiutawala chenye mamlaka kiasi fulani kuendesha shughuli za kiutawala za eneo husika kama vile wilaya au mji.[1]@wikipidia
 
Halmashauri ya wilaya ikiendelea kiuchumi na kimiundo mbinu hubadilika jina kwenda Halmashauri ya Manispaa na halmashauri ya Manispaa ikiendelea Zaidi hujulikana Halmashauri ya mji na Maendeleo ya mji yakiendelea zaid huitwa halmashauri ya jiji nadhan nimejaribu kujibu Kwa kadri ya uwelewa wangu mdogo
 
kuongezea pia muondo wa kiutawala wa halmashauli ya wilaya unaanzia ngazi ya vijiji, wakati manispaa,mji na jiji huanzia ngazi ya mtaa
 
Halmashauri ya wilaya ikiendelea kiuchumi na kimiundo mbinu hubadilika jina kwenda Halmashauri ya Manispaa na halmashauri ya Manispaa ikiendelea Zaidi hujulikana Halmashauri ya mji na Maendeleo ya mji yakiendelea zaid huitwa halmashauri ya jiji nadhan nimejaribu kujibu Kwa kadri ya uwelewa wangu mdogo
Mji na jiji hapo umechanganya
 
Naulizia vitu hivi hapa wakuu;
1. Halmashauri ya wilaya
2. Halmashauri ya manispaa
3. Halmashauri ya mji
4. Halmashauri ya jiji
5. Maana ya 'halmashauri'

Hili ni jukwaa la kujifunza na kuelimika, naomba nielimishwe kuhusu hoja hizo hapo juu ambazo mpaka sasa nazijua kwa mazoea tu ya kuzitamka basi lkn si kwa kuzichambua.....isitoshe kutoa elimu kwa mtu ni ibada tosha kabisa kwa Muumba, yaani Mola.

Ahsanteni na mbarikiwe sana!
Iko Hivi:
Kuna kitu kinaitwa Mamlaka za Serikali za Mitaa ambao umegawanyika kama ifuatavyo;
*Halmashauri za Majiji.
*Halmashauri za Manispaa.
*Halmashauri za Miji na.
* Halmashauri za Wilaya.
Halmashauri ni chombo kwenye ngazi ya jamii ambacho kinaundwa kisheria kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii kwa kushirikiana na Serikali kuu.
Halmashauri inaundwa na Madiwani ambao huchaguliwa kwenye uchaguzi Mkuu kutoka kila Kata kwenye eneo husika kwa maana ya wawakilishi wa wananchi na idadi yao inatokana na idadi ya Kata na Madiwani wa viti maalum.
Kiongozi wa Madiwani ambae huchaguliwa miongoni mwa Madiwani ni Mwenye kiti wa Halmashauri kwenye halmashauri ya Wilaya na Mji au Mstahiki Meya kwa maeneo ya Jiji na Manispaa.
Msingi wa haya ni Katiba na sheria 287,288,289.
Mkurugenzi Mtendaji ndiye anakuwa Katibu wa Halmashauri husika.
Kwa leo japo kwa uchache,kama kuna maswali unaweza kuulizia.
 
Back
Top Bottom