Mtumishi mwenye Mkataba namba Na. SMC/CW/PF.113/3 amefika Ofisini kwetu na ameomba tupaze sauti kwa niaba yake. Hii hapa historia fupi ya malalamiko yake.
Wakati wa zoezi la uhakiki wa Watumishi wa Umma 2016/2017 mwajiri wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga alizuia, kusitisha na Hatimaye kumwondoa kwenye malipo ya mshahara akiwa masomoni kwa Shahada ya kwanza katika moja ya vyuo vikuu hapa nchini. (Zingatia kuwa alikuwa na sifa zote kwenda masomoni na kwa ufadhili wa Mwajiri wake). Huyu Mtumishi alilalamikia hatua hiyo na baada ya uhakiki mwajiri alijiridhisha pasi na shaka kwamba;
1. Si Mtumishi hewa.
2. Alikuwa na Ruhusa Rasmi ya kwenda Masomoni.
CHANGAMOTO
Kwa kuwa mwajiri alishazuia, kusitisha na kumwondoa kwenye malipo ya mshahara tangu Januari 2017, imekuwa ni vigumu kumrejesha Kazini licha ya juhudi kubwa za ufuatiliaji wa mara kwa mara na kwa muda wote anazoendelea kuchukua kwa Muda wa miaka 7.
sasa! Ikumbukwe kwamba kati ya Julai na Disemba 2021, Ndugu, Jamaa na Marafiki walilazimika kumchangia Fedha za kuweka kambi Ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ili kukwamua shauri lake.
Kwa ujumla alifanikiwa kwa hatua kadhaa maana kamati ya nidhamu ilimuita kwa barua yenye Kumb. Na.SMC/CW/PF.118/6 na kumhoji kwa maneno na kwa Maandishi. Kamati hiyo iliahidi kutoa taarifa yake kwa Mkurugenzi ili nae atoe uamuzi wake kulingana na Taratibu.
OMBI LAKE KWA MAMLAKA HIZI
Anaomba Mamlaka zimsaidie kujua.
A) Mchakato uliotumika kuzuia, kusimamisha na Hatimaye kumwondoa kwenye malipo ya Mshahara January 2017.
B) Majibu ya Kamati ya Nidhamu chini ya Ofisi Mwajiri wake iliyomuita na kumhoji tarehe 11.11.2021 kwa Barua yenye Kumb.Na SMC/CW/PF.118/6
C) Endapo hatua A na B hapo juu hazikuzingatia Kanuni za Utumishi wa Umma, basi aruhusiwe kuendelea kutumikia mkataba wake wa Ajira kama ulivyo na Marekebisho yake.
D) Na iwapo alishaondolewa Kazini, ni haki ajulishwe kwa Barua Rasmi kulingana na Sheria, Taratibu na Kanuni za Kiutumishi.
IKUMBUKWE KUWA
Mheshimiwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo kwa waliokuwa watumishi hewa kurejeshewa sehemu ya iliyokuwa michango yao. Lakini kwa kesi ya Mtumishi huyu imekuwa ni vigumu maana si Mtumishi hewa na hana Barua yoyote inayoelezea hatima ya Mkataba wake vs Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Amejaribu kudai mafao yake PSSSF, Jambo hili nalo limekuwa gumu na kwa ufupi limeshindikana maana hana fao analoweza kuangukia.
TETESI ZILIZOPO KUHUSU UGUMU WA JAMBO HILI
Inasadikika kwamba Afisa Utumishi katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa wakati huo Bwana Shaphat Samuel Kaponela, alificha Jalada (Kama siyo kulipoteza kabisa) la Mtumishi huyu na hivyo kwa sasa inakuwa vigumu kwa Watendaji waliopo kufanya Uamuzi Sahihi.
Afisa huyo alichukua Uamuzi huo wa ajabu baada ya kubaini kuwa aliipotosha Mamlaka kufikia maamuzi ya kufaa. Kwa sasa Afisa huyo amehamishwa. Tunazo nyaraka nyingi kuhusiana na shauri hili na tunapanga namna ya kumsaidia huyu mwenzetu ili haki yake ipatikane maana Jambo hili limekuwa ni mateso kwake yeye na familia yake. Amerudi kwao kijijini na anajitafuta kutokea huko. Mamlaka na wadau mbalimbali mvusheni mwenzetu.