achengula
JF-Expert Member
- Jul 30, 2009
- 369
- 63
Ndugu wana JF, nina blogu yangu ya mifugo hapa SEKTA YA MIFUGO TANZANIA nilikuwa nataka kuiboresha kwa kuweka picha mwanzoni mwa home page. Nataka niweke picha za mifugo hapo mwanzo lakini zijae yaani from left margin to right margin. Nimejaribu naona zinakaa upande wa kusho na hivyo hazivutii, nimeona baadhi ya watu wameweka nimejaribu kuwacontact wanielekeze sijapata majibu. Hivyo hapa nategemea wataalamu ni wengi nitapata msaada. Mfano ni blogu ya Francis Godwin (Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima) yeye ameweka picha na nyingine zina animate, tena nyingi kabla hufikia sehemu ya kupost habari. Natanguliza shukrani wakuu.