Msaada: Kampuni ya XBasis Company Limited ni halali?

Earn the one

Member
Aug 17, 2017
84
102
Habari za uzima ndugu zangu, naomba niende moja kwa moja kwenye mada yangu kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.

Dhumuni langu la kufungua uzi huu nilikuwa naomba msaada kwa yeyote mwenyewe Kuifahamu hii kampuni inaitwa XBASIS COMPANY LIMITED maana mimi niliiyona kupitia instagram page yao nikakutana na matangazo kama mawili ya kazi nchini Dubai na Moldova, kwa maelezo yao hawa ni recruitment agencies na ofisi zao ziko mabibo makutano.

Sasa nilikuwa nataka nianze process zao ili na mimi niweze kwenda huko kwasababu hii ni ndoto yangu ya muda mrefu sana kwenda kufanya kazi nchi za watu, kwa maana wanajali sana wananchi wao hapa nchini kwetu nishakuchoka na maisha ya hapa kazi unafanya lakini unapata hela ya kula tu hata kuwasaidia wazazi inakuwa changamoto hapa sitaki kuongea sana.

Asante sana, natumaini nitapata majibu yakuridhisha sana kutoka kwenu pia kwa yeyote ambaye anajua agencies yeyote nyingne naomba usisite kuweka contacts zao hapa ili tuweze kuwasaidia na wengine wenye ndoto kama zangu pia niweka picha yenye mawasiliano ya hawa Xbasis Company Limited.

Hii ndo namba yao +255 714 334 497 Ipo Whatsapp

IMG_7380.png

Naomba kurudisha kwenu sasa wana jamiiforum.

NB: Passport ya kusafiria tayari ninayo, Asante.
 
Kawaone ofisini na wakupe reference yakueleweka kabla hujatoa hela yako.

Best of luck!
 
Umewasiliana nao whatsapp waka semaje?

Fanya mawasiliano huku unaendelea kuwafatilia

Pia fika Taesa ukajilizishe usajili wao kuhusu kazi nje ya nchi

Pia waulize kama mikataba yao ya kazi huwa mnaisajili taesa? Au mnatumia utaratibu gani?
 
Ndio wamenijibu tu niende ofisini kwao kwa maelezo zaidi nikifika huko naona nipata majibu ya haya maswali yote
 
Naelewa hayo yote ndo maana nimekuja hapa kuomba msaada kwa yeyote anaijua hii kampuni
Moldova hii hii iliyoko Eastern Europe? Uwe mwangalifu mno mno. Siku hizi matapeli wana ofisi na wanaita watu kwa usaili. Wengine wamefikia hatua ya kuweka watu kambini wakisubiri ''hewa''. Na Dubai nako, hata kama ni kweli uwe makini. Waarabu siyo watu. Hushangai kwa nini wasomali wengi wanakimbilia Europe na America na siyo Uarabuni!
 
Nenda ofisini kwao kisha ukifika jiulize yafuatayo

1. Hivi huyu dada mpokea wageni hapa ofisini yeye hataki kwenda kufanya kazi Dubai kweli??

2. Huyu jamaa aliye ofisini na moka zake na tumiwani anayejifanya incharge na kingereza kingiiiiiii cha kuunga unga kweli ndugu zake wa kuzaliwa hawaitamani Moldova kweli??
 
Sawa kiongozi nimekuelewa na niko makini sana ndo maana nimekuja kuanzisha uzi hapa
 
Nenda ofisini kwao kisha ukifika jiulize yafuatayo

1. Hivi huyu dada mpokea wageni hapa ofisini yeye hataki kwenda kufanya kazi Dubai kweli??

2. Huyu jamaa aliye ofisini na moka zake na tumiwani anayejifanya incharge na kingereza kingiiiiiii cha kuunga unga kweli ndugu zake wa kuzaliwa hawaitamani Moldova kweli??

Ngoja niende nikaone ila kuna mda ukikaa ukijiuliza haya mswali unaona kama ni kama kamchezo hivi.

Sema ngoja ni try kuliko kukaa tu maana hali si nzuri kabisa mtaani.
 
Moldova hii hii iliyoko Eastern Europe? Uwe mwangalifu mno mno. Siku hizi matapeli wana ofisi na wanaita watu kwa usaili. Wengine wamefikia hatua ya kuweka watu kambini wakisubiri ''hewa''. Na Dubai nako, hata kama ni kweli uwe makini. Waarabu siyo watu. Hushangai kwa nini wasomali wengi wanakimbilia Europe na America na siyo Uarabuni!
Nadhani ni visiwa vya Maldives vilivyoko bahari ya hindi pembezoni mwa India, ndio wana mahusiano ya kitalii na Dubai.
 
YAFUATAYO YANATIA MASHAKA:
1.HAIJASAJILIWA TANZANIA
2.HAWANA WEBSITE
3.NAMBA YA SIMU INA MAJINA YA MTU BINAFSI!

ANGALIZO:

KAMPUNI KUTO SAJILIWA HAPA TANZANIA, NI ISHARA MBAYA YA KUTOKUWEPO KWA HIZO HUDUMA.
NA KAMA ZIPO,BASI NI UTAPELI.SASA KAMA UNA SHIDA NA KUTAPELIWA ENDELEA.

WAAFRIKA, WANAPITIA MATESO MAKUBWA HUKO NCHI ZA ARABUNI.BILA MAWASILIANO YA UHAKIKA NAMBA ZA SIMU, ,WEBSITE. UNAWEZAJE KUSAIDIWA UKIWA NA TATIZO HUKO NJE?
KWANI KUSAJILI NAMBA YA SIMU KWA MAJINA YA KAMPUNI YAKO NI BEI GANI? HAKUNA GHARAMA!
SASA HIVI KUNA WATU WANA TENGENEZA WEBSITE MPAKA KWA TZS 150,000! UNAWEZAJE KUWATAFUTIA AJIRA WATU HUKO NJE NA WEWE UKASHINDWA KUMILIKI WEBSITE?

Hii email address"recruitment@xbasic.co.tz", haifanyi kazi. Haipo

NAJUA JF INAWATUMIAJI ZAIDI YA 20 MILLION.
NI VYEMA BASI WAHUSIKA WAKAJA NA MAJIBU SAHIHI.YA UHALALI WA KAMPUNI YAO.

ZAMA ZIMEBADIRIKA, UJINGA WAKO NI MTAJI WA WENZIO!
#STUKA!
 
Kiongozi kuhusu kusajiliwa sina uhakika maana bado sijafika ofisini kwao

Ila website wanayo japo haina maelezo mengi unaweka ukaipitia hapa

Na Email yao sio hiyo ni hii xbasicrecruitment2023@gmail.com
 
Back
Top Bottom