Msaada wa kuondoa tattoo

Unasemaje kabahatika kwenda wakati anayo tattoo? Kitendo cha kuwa na tattoo tu ni sababu tosha kuwa hutajiunga na jeshi lolote hapa Tz, na kujichoma na pasi haitamsaidia maana hata makovu makubwa huwa hayatakiwi.
Ko makovu makubwa likiwa fogo
 
Mwambie atafute kazi nyingine, jeshi sio kazi, wanaenda kuuliwa kama kuku nchi za watu wanapokwenda kulinda amani kama Kongo, somalia na sudan afu inabaki kuwa Siri ya jeshi, hawasemagi.

Afu wanapelekwa pelekwa ovyo kama wafungwa, sheria ni ndio Kila kitu ndio mkuu, hata ubakwe ndio mkuu
 
Mwambie kama alitaka kula ubwabwa ila akaweka mahindi jikoni badala ya mchele basi ale hicho hicho kitakachoiva maana ni miujiza ndo itageuza mahindi kuwa mchele unless fedha ipo amwage mahindi atoke nje akalete mchele.
 
Pole yake,
2014 tulikua mujibu tulimkuta afande mmoja anatatoo kubwa Mkononi, tukawauliza wale maafande wadogo wakasema huyu aliingia kwa kipaji cha boxing miaka ya zamani , huyo mdogo wako na yeye ataenda kwa kipaji cha boxing au Shadow7 sa meja inawezekana
 
Nisimfiche kwa sheria za bakabaka haiwezekani. Japo ya Mungu mengi
 
Karibia clinic yangu nitamfuta bure.

Tunawakumbusha watoto na wadogo zetu msiendeshwe na utandawazi. Ni aheri usemwe mshamba kuliko gharama za kuthibitishia jamii kuwa wewe ni msasa.
 
Pale nafsi ya 3 umoja inapotumika kuelezea Tatizo la Nafsi ya 1 umoja

Hii ndio JF
 
Pole mkuu

Ila be in touch na wachora tattoo wakubwa hao hao neo wanakuwaga na real remedies za kufuta tattoo

Ikiwa UPO DSM wacheki Instagram katika DM zao.
 
Huyo ni unfit
Sheria za jeshi haziruhusu tattoo au makovu makubwa mwambie afanye mishe nyengine tu asipoteze muda.
 
Acha avune ujinga wake
 
Anayefikia hatua ya kujichora tatuu, anakosa sifa ya kujiunga na jeshi lolote la ulinzi la nchi yetu.
Majeshi ya ulinzi ni idara nyeti zinazohitaji kuajiri watu wenye nidhamu ya hali ya juu.

Jeshi sio ajira ni kujitolea kuilinda nchi na mali zake.
 
Kuchora tattoo ni maamuzi yanayohitajo akili kubwa sio mihemko maana majuto yake ni mengi.
Otherwise waachie wenzetu wa majuu huko ni kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…