Msaada wa kununua gari ndogo (IST)

Msaada wa kununua gari ndogo (IST)

Seran

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2025
Posts
11,518
Reaction score
34,577
Habari zenu,

Naomba msaada kwa mtu anayefahamu jinsi ya kuagiza gari nje, gari ndogo aina ya Ist, nimeulizia kwa makampuni ninayoyafahamu naona bei hazipishani na yard japo wanasema bei imepanda(17-18m)

Briefly, rafkiangu anataka kuagiza gari (mwenyewe)aina hiyo kupunguza gharama, bila kutumia kampuni za ndani, sijajua kwanini kafikiria hii ndio njia nzuri, ila kumsaidia zaidi nimeona nililete humu!

Wenye ujuzi karibuni!
 
Habari zenu,

Naomba msaada kwa mtu anayefahamu jinsi ya kuagiza gari nje, gari ndogo aina ya Ist, nimeulizia kwa makampuni ninayoyafahamu naona bei hazipishani na yard japo wanasema bei imepanda(17-18m)
Kama hafahamu jinsi ya kuagiza gari nje, ni bora akaenda kununua showroom, kwani kuna uhakika ananunua kitu anachokiona. Huko nje hata aagize vipi kwa ist ataokoa 2m au 1.5 kwa pesa hiyo ni kheri aepuke risk ya kuibiwa, na presha ya kufika kwa gari
 
Hiyo gari anunue hapo hapo huku akiiona mwenyewe kuagiza gari nje kuna ujanja mwingi sana na wauzaji wa nje wakigundua ni mgeni utauziwa wenyewe wanasema mbuchi kwako ni hasara kwao ni faida kwa sababu haukuweza kukagua vitu vya msingi kama wanavyofanya wauzaji wa yard..
Usijaribu kununua gari nje kama sio mtaalamu...
Ist pia hazina changamoto kama unanunua ndani na mpya isiyo na namba umiliki wa kwanza uwe wa kwenu sio iwe ishamilikiwa au namba tayari sijui unaambiwa ina E usichukue waanze kuisajiri kwenu..
 
Sawa sawa
Asante sana kwa ushauri mzuri🙏🏽
 
Akijichanganya tu kidogo atapigwa kama ngoma. Kuagiza gari ni rahisi sana ila kama hana uzoefu atajichanganya na ndio itakuwa maumivu kwake. Juzi kuna mdau alinicheki anayo 15.5m anataka ist chasis, zipo ila ikifika lazima akainyooshe body, yaani ni mbuche mbucheni. Nikajiepusha nae maana hizo ni lawama baadae.
 
Hiyo gari anunue hapo hapo huku akiiona mwenyewe kuagiza gari nje kuna ujanja mwingi sana na wauzaji wa nje wakigundua ni mgeni utauziwa wenyewe wanasema mbuchi kwako ni hasara kwao ni faida kwa sababu haukuweza kukagua vitu vya msingi kama wanavyofanya wauzaji wa yard..
Usijaribu kununua gari nje kama sio mtaalamu...
Ist pia hazina changamoto kama unanunua ndani na mpya isiyo na namba umiliki wa kwanza uwe wa kwenu sio iwe ishamilikiwa au namba tayari sijui unaambiwa ina E usichukue waanze kuisajiri kwenu..
Jibu kama la A.I vile
 
Jibu kama la A.I vile
Ni akili mingi kwenye magari nipo JHB nimetumiwa picha nzuri ya Scania kutoka Durban kinachotakiwa ni kuchukua mwewe na kwenda kuangalia live..
20260124_115524.jpg
20260124_115535.jpg
 
Ni bora mtu anayenunua IST kuliko anayenunua Alphard, Noah, Voxy au Ractis
Mkuu Tanzania sio China nenda Arusha uone Noah Sr 40 kazi za Namanga Namanga zinavyokimbia na abiria miaka yote ndio usafiri wao ni gari imara kuhusu Alphard ndio gari zinazotumika kufanya transfer ya wageni kutoka KIA mpaka Arusha ni usd 70 mpaka 80 harafu upo hapa unaziponda...
 
Hajui kitu huyo, hamna gari inafanya biashara vizuri sasahivi kama alizotaja hapo
 
Back
Top Bottom