Msaada wa kumroga aliye Senegal, amenitapeli TZS 5 Millioni

Msaada wa kumroga aliye Senegal, amenitapeli TZS 5 Millioni

Vya mbali vinagharama zake na wajinga ndio waliwao, umeliwa baba Shukuru tu M/Mungu
 
hiyo program inaitwa make money from home, wanachofanya ni ku copy template na ku edit kidogo kisha wanatafuta pumbav jama wewe na kuwapiga, ushakula za uso ndugu
 
Duh! Pole sana, yaani hv hv serious ww ulituma hzo pesa?

Hawa jamaa wamejaa kibao kila mahali, binafsi walianza kunisumbua kitambo sana zaidi ya miaka imepita sasa kabla hata Facebook haijapata umaarufu.

Pole sana ndugu! Huna haja ya kumroga kwani hilo ni fundisho kwamba usitume pesa kwa mtu usiemfahamu
 
Weka maji ktk kisoda kisha hakikisha umeyaoga hayo maji mwili mzima huku ukitamka jina lake na unachotaka kimtokee! Hii itafanya kazi kama utafanikiwa kuoga mwili mzima maji hayo ktk hicho kisoda kimoja!
 
Graduate huyu!

Kwanza aliyekuibia ni dume - zile picha huwa sio zao. Harafu unafikiri uchawi wako utamfikia huko alipo? No wonder alikuliza kirahisi. Upo nyuma sana.
 
Kama kweli mtoto wa chuo kikuu uliona zile msg ndeeeefu zilizokuwa zinatumwa kwa email ya kila mtu na ukaona umetusua pole yako.. Na kwa taarifa yako wale ni wanigeria matapeli..hapo kama ni kweli umelizwa tulia tu na usahau kwani hakuna unachoweza kufanya...ukienda kwa mganga utapigwa tena kama milioni na hutaona matokeo utazidi kula hasara.. jifanye tu ni duka limeungua kwa moto na huna bima kubali hasara songa mbele..
 
Omba msaada kwa mzee wetu pendwa mch. GWAJIMA anawajua watu wote
 
Wewe halali yako kabisa kupigwa,hela tayari anayo iko kny accnt unadanganywa kui activate. Au ndo ulifuate ule msemo wa toa hela upate hela. Ila hapo sio mbaya hutapigwa tena kaka
 
Duu!! five millions? kwa msomi wa chuo unamtumia mtu hivi hivi, utakuwa unatoks kolomije tu
 
Matapeli hawarogeki huko mi kuzidi kupoteza hela ingekuwa wanarogeka kampuni nyingi zinatangaza donge nono kwa kumtafuta mtu aliyesepa na mpunga kwenye magazeti so uchawi ungekuwa deal kwenye organisation structure za kampuni nyingi mchawi angekuwepo kama
 
Salam wakuu.

Naomba ushauri wa namna ya kumroga mtu ambaye yupo nchi ya nchi ya Tanzania. Kuna mdada mmoja nilianza kuwasiliana nae mapema mwaka juzi nikiwa Chuo Kikuu Mzumbe,anatokea Senegal.Alianza kwa kuniomba urafiki facebook, nikamkubalia.Alionekana kuwa mwenye umbo zuri na sura nzuri sana.

Ikafikiwa hatua akasema yupo kambi ya kulelea watoto waliopatwa na majanga ya wazazi wao,na yeye akiwa mmoja wapo. Kwa historia yake, alisema babaake alikuwa meneja wa benki kule Sudan kusini lakini baadae aliuawa na kuacha kiasi kikubwa sana cha pesa benki, US$ 20,000,000.(Dola milioni ishirini).

Tukakubaliana mm nitume hela milioni 5 za hapa kwetu kwa ajili ya kuactivate akaunti ya babaake ili hela hizo zichukuliwe. Alisema mm ningepata mgao wa TZS 150,000,000 na alishakubali kuja kuishi hapa Tanzania ili tuoane maana yeye hana ndugu tena.Walikufa kwa machafuko. Nilipambana sana na hali hii ilivyo, nikatuma TZS 5,000,000 (kwa mfumo wa dollar). Cha kushangaza, hata simu aliyokuwa akiitumia kuwasiliana na mm, haipatikani. Hata mlezi wao hapatikani.

Naombeni mbinu mpya ya uchawi ili nimrogee hukohuko.Siwezi kukubali hela yangu ikapotea hivyohivyo mm.Sikubali kabisa.

Msaada please.

Nawatakia jioni njema

UNATAPELIWAJE KIRAHISI HIVYO?
 
Mkuu hadi Leo unatapelewa na watu hawa? We wa wapi Au Hom matombo?
 
Aaaah mkuu kama ni huyo imekula kwako. Me mwenyewe alinijaribu nikamshtukia mapema.

Yani haiwezekani mtu anataka eti akutumie hela alafu wewe ndo uanze kumtumia ela. Aliniambia kuna us dolla 3.8mil nchini scotland eti nimfanyie msaada wa kuziingiza kwenye account yangu alafu atakuja kuzichukua huku tanzania. Yeye yupo kambini hawezi kufanya hivo.

Tumeenda mwisho wa siku wanataka niwatumie mil12. Nikaona msinitanie nyie sitapeliwi kizembe.
 
Utapeli wa mda mrefu sana miaka ya 2007 inaonekana kwenye mitandao umeingia hv karibuni
 
Kweli aisee utapewa ni wa muda sana Jamaa sijui alikuwepo wapi hajaupata ukiingia kichwa kichwa unaweza sema zali la mentali hili
 
Mimi ni mkristo na kwenye maandiko Matakatifu ndani ya Biblia Takatifu kina mstari umeandikwa usimdai mtu uliyemkopesha kama hataki kulipa deni Mwachie Mungu atashughulika nae
kiongozi unaweza weka kitabu na aya kwa kutusaidia
 
Back
Top Bottom