Msaada wa kumroga aliye Senegal, amenitapeli TZS 5 Millioni

Msaada wa kumroga aliye Senegal, amenitapeli TZS 5 Millioni

Pole sana, nilishatumiwa sana hizo sms. Na inawezekana hayuko senegal kama unavyosema. Naskia wengi ni wanigeria
 
Mimi walisha wai kunitokea kwastaili hiyohiyo kwanza anaonba urafiki fb ukikubali anakutumia kwa. Email ukiingia kingi anajifuta fb hapondipo anadili nawewe in private. Kwamimi alipo fikia nimtumie pesa hapo ndipo nikaanza kumchunguza kupitia google.com. ndipo nilipo gundua kuwa ni matapeli wa kimataifa.anajifanya refugee kumbe sio polesana ulitakiwa kufanya uchunguzi kwanza kabla yakutuma pesa kumbuka duniani hakuna pesa ya burebure.
 
Yaani, ulivyoanza tu ndiyo umeharibu kabisaa!

Kwa sababu, tatizo lako ni umbo na uzuri wa huyo msichana, ulikuwa unazitoa hela kwa kuangalia muonekano wa msichana. (Ulizitoa, siyo kumsaidia bali kupata umbo lake ).

Pia, pole sana kwa kushindwa kuelewa kuwa kuna wezi wa mtandaoni kuanzia miaka ya 2000s

Nampongeza sana huyo mdada, kwa kukukomesha ndiyo ukome kabisa.

Umevuna sawasawa na ulichopanda!
 
Salam wakuu.

Naomba ushauri wa namna ya kumroga mtu ambaye yupo nchi ya nchi ya Tanzania. Kuna mdada mmoja nilianza kuwasiliana nae mapema mwaka juzi nikiwa Chuo Kikuu Mzumbe,anatokea Senegal.Alianza kwa kuniomba urafiki facebook, nikamkubalia.Alionekana kuwa mwenye umbo zuri na sura nzuri sana.

Ikafikiwa hatua akasema yupo kambi ya kulelea watoto waliopatwa na majanga ya wazazi wao,na yeye akiwa mmoja wapo. Kwa historia yake, alisema babaake alikuwa meneja wa benki kule Sudan kusini lakini baadae aliuawa na kuacha kiasi kikubwa sana cha pesa benki, US$ 20,000,000.(Dola milioni ishirini).

Tukakubaliana mm nitume hela milioni 5 za hapa kwetu kwa ajili ya kuactivate akaunti ya babaake ili hela hizo zichukuliwe. Alisema mm ningepata mgao wa TZS 150,000,000 na alishakubali kuja kuishi hapa Tanzania ili tuoane maana yeye hana ndugu tena.Walikufa kwa machafuko. Nilipambana sana na hali hii ilivyo, nikatuma TZS 5,000,000 (kwa mfumo wa dollar). Cha kushangaza, hata simu aliyokuwa akiitumia kuwasiliana na mm, haipatikani. Hata mlezi wao hapatikani.

Naombeni mbinu mpya ya uchawi ili nimrogee hukohuko.Siwezi kukubali hela yangu ikapotea hivyohivyo mm.Sikubali kabisa.

Msaada please.

Nawatakia jioni njema
Hahahahahahahahahahahahahahahahahahaahahahahahhahahaahahahaahah i really can't help but laugh hahahahaahah any way i may have only three words for you [emoji117] YOU ARE STUPID.
 
Salam wakuu.

Naomba ushauri wa namna ya kumroga mtu ambaye yupo nchi ya nchi ya Tanzania. Kuna mdada mmoja nilianza kuwasiliana nae mapema mwaka juzi nikiwa Chuo Kikuu Mzumbe,anatokea Senegal.Alianza kwa kuniomba urafiki facebook, nikamkubalia.Alionekana kuwa mwenye umbo zuri na sura nzuri sana.

Ikafikiwa hatua akasema yupo kambi ya kulelea watoto waliopatwa na majanga ya wazazi wao,na yeye akiwa mmoja wapo. Kwa historia yake, alisema babaake alikuwa meneja wa benki kule Sudan kusini lakini baadae aliuawa na kuacha kiasi kikubwa sana cha pesa benki, US$ 20,000,000.(Dola milioni ishirini).

Tukakubaliana mm nitume hela milioni 5 za hapa kwetu kwa ajili ya kuactivate akaunti ya babaake ili hela hizo zichukuliwe. Alisema mm ningepata mgao wa TZS 150,000,000 na alishakubali kuja kuishi hapa Tanzania ili tuoane maana yeye hana ndugu tena.Walikufa kwa machafuko. Nilipambana sana na hali hii ilivyo, nikatuma TZS 5,000,000 (kwa mfumo wa dollar). Cha kushangaza, hata simu aliyokuwa akiitumia kuwasiliana na mm, haipatikani. Hata mlezi wao hapatikani.

Naombeni mbinu mpya ya uchawi ili nimrogee hukohuko.Siwezi kukubali hela yangu ikapotea hivyohivyo mm.Sikubali kabisa.

Msaada please.

Nawatakia jioni njema
Mkuu huyo sio msenegal wala nini hao ni scammers kutoka nigeria. Facebook hawapo sana kwa miaka hii ila mitansao mengine ya kijamii wamejaa
 
Huo wizi umeelezewa sana tena ulikuwepo sana 2012 lkn bado unatapeliwa tuu mkuu
 
Ndio kujiunga mitandaoni karibuni... Subiri kuna mwengine atakuja atakwambia babake alikuwa mfalme aliuliwa na anataka akutumie hayo mabilioni
 
Dah mamaeeee walai[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] wajomba wengii umu ndani[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] karaghabaooooooooooooooo.
 
Back
Top Bottom