Msaada wa kisheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa kisheria

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by GRACE KIRUNDWA, Jun 16, 2010.

 1. G

  GRACE KIRUNDWA New Member

  #1
  Jun 16, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  habari zenu,

  ninaomba msaada wa kisheria

  * kwa mfano umeolewa ukamkuta mwanamume na nyumba aliyoridhi kwa mzazi wake .
  kama kiwanja ni kikubwa ukijenga nyumba nyingine ni kosa? . Je utakuwa na haki huko baadaye

  asante sana
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Karibu sana Grace uwanjani. Wasubiri wataalam wa sheria watafika hima kukusaidia swali lako. Sisi wengine tunakukaribisha tu jamvini.
   
 3. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Sina shaka ugeni umekufanya hata ukapotea jukwaa. Hili ni la mambo ya Elimu lakini hapana shaka!.

  Kimsingi labda kwa usahihi zaidi ungekuwa wazi unaposema "haki yako baadae" una maanisha kuwa hiyo ndoa yenu haina maisha marefu?. Je, unampango wa kuachana hapo baadae?.
  Vinginevyo, tafsri kujua utakuwa na haki au huna iwapo ndoa itavunjika, kutendana au kuachana kabisa inategemea na aina ya makubalinao kati yenu. Kwa kawaida mali katika ndoa inapofika kwenye suala la mali kila mmoja wenu haki yake inazingatia mchango wake katika kuipata mali husika. Mali ambayo mwanandoa anaweza kusema ana haki nayo ni ile tu ambayo imapatikana katika kipindi cha ndoa na kwa jitihada za pamoja (yaani wakati wawili akiwa wanaishi pamoja).
  Sheria haizuii mtu kumiliki mali binafsi ndani ya ndoa, mali inaweza kuwa tu ya wanandoa wote iwapo mtakubalina iwe hivyo hata kama ilipatikana na mmoja wenu kabla ya ndoa.

  Kwa ufasaha zaidi, kujua kama utakuwa na haki au lah, ni vyema pia ungeweka bayana iwapo hicho kiwanja cha urithi bado huyo mume anakimiliki peke yake (yaani si mali ya ndoa?) na Je, hiyo nyumba ambayo ulikuja kujenga umejenga peke yako au kwa jitihada zenu waote wawili?.

  Ikiwa yeye ana kiwanja na wewe umejenga nyumba juu ya hicho kiwanja, pasipo kuwepo makubalinao tofauti ya hapo, kisheria maendelezo uliyofanya juu ya hicho kiwanja ndio sehemu ya haki yako naye yake ni gharama za hicho kiwanja tu. Hivyo kwa maana nyingine ni kuwa hiyo ni mali ya pamoja kati yenu lakini hii itahitaji zaidi ufafanuzi wa kina kuhusu aina ya makubaliano yaliyo kati yenu na pia vielelezo vya kuthibitisha mchango wa kila mmoja wetu.
   
 4. L

  Lady JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Karibu grace, nijuavyo mimi ardhi hiyo kama ina hati, baada ya kuoana, hiyo ardhi inakuwa "martimonial property" inamilikiwa na wote wawili na wote wawili mnakuwa na haki sawa.
  Labda tusikie na wadau wengine wanasemaje.
   
 5. Elisante Yona

  Elisante Yona Senior Member

  #5
  Jun 16, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 130
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wasiliana na wataalamu wanaotoa msaada wa kisheria wanaoitwa NOLA hapa Dar es salaam wapo Sinza mkabala na Hongera baa,

  Mikoani wapo Mwanza,

  Asante
   
Loading...