MSAADA WA KISHERIA WA ARDHI

MSAADA WA KISHERIA WA ARDHI

Frustration

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,151
Reaction score
4,141
Habari wanajf kwa ujumla. Naomba niende kwenye mada moja kwa moja kwa kuanza kutoa maelezo mafupi.
Mashamba ya familia yangu yapo kijiji jirani na mashamba hayo tuliyapata wakati huo tukiwa kijiji kimoja ila baada ya kujigawa ikawa mashamba yetu yapo kijiji kingine.
Kuna viashiria vya kutosha hadi sasa kwenye mashamba hayo kama vile miembe,mibolea na michungwa iliyopandwa na wazee wetu. Toka tuache kufanyia kazi maeneo yale panakaribia miaka 11 au 12 hadi sasa.
Hivi karibuni nimetembelea nimekuta kuna watu wanafanyia kazi i.e wamelima na nilivyofuatilia nimekuja kujua kuwa mmoja alipimiwa na serikali ya kijiji hekari 10 na wengine wanalima tu bila ya kupimiwa na serikali wala familia haijawapa maeneo hayo kulima.
Familia imewashitaki au kuwalalamikia watu wote waliokutwa katika maeneo hayo katika baraza la usuruhishi la kata kwa kosa la kulima katika maeneo yetu na kukataa kuondoka. Wao wanaeleza kuwa wanalima katika ardhi ya kijiji chao na hawawezi toka.
Mwenyekiti wao aliomba jambo liende kijijini kwakwe kwa usuruhishi zaidi na kata ikatoa siku 15 kusubiri majibu toka serikali ya kijiji jirani. Kuna siku tulialikwa kwenye kikao na tulishindwana kwakuwa wao kama serikali wanakilri kuwa eneo ni letu ila tuliyatelekeza mashamba hayo na hivyo kijiji yameyachukua kwa matumizi yake.
Pia walitushauri kama tunataka ardhi basi tuandike maombi ya kuomba ardhi kwa barua na kijiji kitatupatia kwa sharti la kupatiwa eneo lingine au palepale. Huu kama familia tumeona ni mtego ikiwa tutaandika maombi.

Naombeni ushauri wenu ikiwa serikali ya kijiji na watu wake wanadhamira mbaya na mashamba yetu, naomba muongozo wa kisheria juu ya mambo haya kwani tarehe 26 tunatakiwa tena shaurini.
Niwaombe msamaha kwa uandishi mbaya na mrefu AHSANTENI!
 
LAZIMA UWE NA CONCRETE/UMATHUBUTI WA UMILIKI WA ARDHI HIYO. MLIIPATA PATAJE.......GENESIS OF OWNERSHIP

1. Kwanini mliitelekeza ardhi hiyo muda mrefu...hili ni swali kubwa sana. KWANINI? Ardhi ya kijiji ikitelekeza kwa muda mrefu, serikali ya kijiji kupitia village assembly wana haki ya kisheria kuigawa.

2. Miaka 12 kisheria, you are time-barred kusema hii ilikuwa ardhi yangu kama uliitelekeza. HAKIKISHA MUDA WA KUITELEKEZA USIZIDI MIAKA 12...USIJE UKALOGWA UKASEMA MWAKA AMBAO MLIITELEKEZA IKIJUMUISHWA IKAWA 12 AU ZAIDI.

3. Usiandike barua dai ardhi yenu! Usiingie kwenye mtego huo mana sasa inakuwa ni fadhila na si haki yako.

MWISHO: tayarisha ushahidi madhubuti kuonesha kuwa ardhi ni miliki yenu. hii ni muhimu sana.
 
Ngoja tusubiri tupate elimu, maana ardhi za ukoo tulishaziachaga uko kijijini
 
LAZIMA UWE NA CONCRETE/UMATHUBUTI WA UMILIKI WA ARDHI HIYO. MLIIPATA PATAJE.......GENESIS OF OWNERSHIP

1. Kwanini mliitelekeza ardhi hiyo muda mrefu...hili ni swali kubwa sana. KWANINI? Ardhi ya kijiji ikitelekeza kwa muda mrefu, serikali ya kijiji kupitia village assembly wana haki ya kisheria kuigawa.

2. Miaka 12 kisheria, you are time-barred kusema hii ilikuwa ardhi yangu kama uliitelekeza. HAKIKISHA MUDA WA KUITELEKEZA USIZIDI MIAKA 12...USIJE UKALOGWA UKASEMA MWAKA AMBAO MLIITELEKEZA IKIJUMUISHWA IKAWA 12 AU ZAIDI.

3. Usiandike barua dai ardhi yenu! Usiingie kwenye mtego huo mana sasa inakuwa ni fadhila na si haki yako.

MWISHO: tayarisha ushahidi madhubuti kuonesha kuwa ardhi ni miliki yenu. hii ni muhimu sana.
Nitangulize shukurani ndugu yangu kwa ushauri wako Mungu akubariki sana.

Naungana na wewe kuwa tutaendelea kudai na sio kurudi nyuma kwa kutuma maombi ya kuomba ardhi, Nianze na swali la kwanza kwa nini tulitelekeza mashamba. Kwa kuweka uwazi ni kuwa mashamba yaliachwa baada ya zao la tumbaku kufa na kwa mashamba yale yalikuwa mazuri kwa zao hilo. Wazazi walikuwa na mashamba mengine ambayo mazuri kwa mazao kama mahindi na mpunga na mashamba haya yapo kijiji nachoishi kwa sasa.
Kwa hiyo kwa sasa mashamba hayo ni almasi kwa maharage na ufuta na soko lake lipo kwa sasa.

Upande wa umiliki kwakweli hatuna hati yoyote ile isipokuwa kuna hiyo miti ya kupandwa. Ardhi hiyo ilipatikana kwa njia ya asili ya kukagua na ndio aina kubwa zaidi ya umiliki wa ardhi kwa maeneo ya huku.
 
Basi andaa ushahidi imara kuwa miti hiyo mlipanda nyinyi, na hamkuitelekeza maana kuna miti yetu ambayo tulikuwa tunaiangalia mara kwa mara........... on/off ingawa tulikuwa hatuishi hapo. Usiseme tulipatelekeza.
 
Vipi kuhusu hoja yao ya kutofuata utaratibu ambao wao kama kijiji ilitakiwa tuwe tunalipia ushuru wa mashamba[Mchango wa maendeleo ya kijiji] kwakuwa sisi sio wakazi wa kijiji hicho
 
Back
Top Bottom