Kiufupi ni hivi nilivamiwa njiani kwa sababu nadaiwa na microfinance Moja ambayo mahakama tayari iliamuru nilipe deni Hilo mwezi 6 lakini kabda ya huo mwezi kufika nilikutana na mmoja wa hiyo microfinance akawapigia simu wenzake mawili wakaja eneo ambao nipo, wakataka kunipora funguo ya pikpiki yangu ili waondoke na pikipiki yangu, baada ya kuwakatalia kuwapa funguo ndipo wawili wakaniangusha chini mmoja akanikaba shingo wakati mwingine ananipiga ndipo nilipotoa kitu cha ncha kali na kumjerui yule aliyenikaba shingo ili aliachie, baada ya kumkata akaniachia na damu zikaanza kumtoka, wakaondoka na pikipiki yangu, ndipo na mimi nikapata wazo la kuwahi kituo Cha polisi kutoa taarifa hiyo.