Nsennah
JF-Expert Member
- Jan 9, 2021
- 1,560
- 1,085
Habari ndugu wana sheria! Ningependa kujua jambo moja kuhusu urithi wa mali za marehemu kwenye scenario hii! Kuna mzee mmoja alioa kwa ndoa na kupata watoto wa kwenye ndoa na mmoja nje ya ndoa. Mzee huyo na mkewe baadae wakawa hawaishi pamoja kwa zaidi ya miaka 20 ingawa hawakupeana taraka. Mzee baadaye aliaga dunia akiwa anaishi peke yake kwenye nyumba yake, swali langu la msingi ni; Je, mkewe ana haki ya kurithi mali za marehemu kama mjane?