jaap
JF-Expert Member
- Dec 25, 2018
- 4,209
- 5,459
Mzee wetu kasha fariki kaacha wake wawili na watoto 8 kila mke ana watoto wanne. Mzee kaacha nyumba moja na kiwanja kimoja na shamba. Nyumba moja anaishi mke mdogo na kiwanja kimoja, mke mkubwa watoto wake wamejenga nyumba, wanaishi na mama yao, na kwenye shamba wao wanafanya shughuli zao za kiuchumi.
Tatizo linakuja kuhusu kugawana mali za marehemu kwa wake zake wawili. Mke mkubwa anajipa mamlaka ya kugawa mali na kusema nyumba iuzwe na shamba kila mtoto atakayetaka kufanya shughuli za kiuchumi aende kufanya na kiwanja walicho jenga. Watoto wake wawili na familia mbili ziende kuishi pamoja.
Sasa mke mwingine yeye anataka shamba ligawiwe kwa mke mkubwa na mke mdogo, na nyumba kama itauzwa basi na kiwanja walicho jenga watoto wa mke mkubwa nacho kiuzwe. Mke mdogo anashangaa kwanini watoto wanajenga kwenye kiwanja cha baba yao bila ruhusa ya baba yao na wanajua baba yao anawake wawili. Na kuna kiwanja ambacho ni cha familia zote mbili. Naomba ushauri wa kisheria ili kila mke apate haki yake bila mmoja wao kupunjwa.
Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app