Msaada wa kisheria kuhusu Bima

mahirtwahir

JF-Expert Member
Jan 12, 2013
613
311
Habari waungwana.

Jamani naomba kujulishwa ninavyojua mimi kuwa Bima (Insurance) ni makubaliano baina ya mwenye mali anaehitaji bima na mtoa huduma.

Kwa kawaida kwa vyombo vya moto bima ya third party naiona haina maslahi kwa mtumiaji kutokana na taratibu zake za malipo.

Swali:
Je, ni kwa nini kuwe na ulazima wa mtu kukata bima wakati amejikubalishabakipatwa na majanga atakabiliana nayo mwenyewe?

Je, kuendesha chombo kikiwa hakina Bima kuna adhabu gani ama faini gani unapopelekwa mahakamani?

Natanguliza shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bima inaweza kuwa sio kwa ajili yako lkn kwa yule ambae chombo chako kimemsababishia matatizo. Fikiria umesababisha ajali ww ukafa halafu umenijeruhi mimi napataje msaada?

Ndio maana ni lazima chombo kikatiwe hata third party.
 
ULAZIMA WA KUKATA BIMA
1.JE, KWA NINI NIKATE BIMA?

Jibu rahisi kabisa ni kwamba unakata bima kwakuwa ni jukumu lako kisheria. Sheria ya bima za Vyombo vya Moto (Motor Insurance Act, sura ya 169) kifungu cha 4, inalazimisha
chombo chochote kile kuwa na bima kabla ya kutembea barabarani.

HIVYO BASI, Kukata bima sio amri ya Polisi bali ni jukumu la kisheria kwa mujibu wa sheria hiyo ya Bunge.

2. JE, NI AINA GANI YA BIMA NDIO AMBAYO NALAZIMISHWA
KUIKATA?

Sheria inalazimisha mtu mwenye chombo cha moto kukata bima inayojulikana kiingereza kama *THIRD PARTY*. Aina nyingine zote za bima ni hiyari kuzikata. Kwa ufupi zipo aina
nyingi sana za bima ambazo sio lazima kuzikata bali ni hiyari tu. Bima pekee ya lazima ni THIRD PARTY.

3. KWA NINI BIMA YA LAZIMA INAITWA THIRD PARTY?

Inaitwa third party kwakuwa bima hii lengo lake ni kumsaidia mtu wa tatu au mtu mwingine zaidi ya yule mwenye bima mwenyewe. Huyo mtu mwingine anaweza akawa ni abiria uliyempakia, dereva mwenzio uliyemgonga, mtembea kwa miguu uliyemgonga, au mnyama uliyemgonga barabarani au hata miundombinu.

Ni bima kwaajili ya mtu wa tatu kwakuwa mtu wa kwanza ni Kampuni ya Bima, mtu wa Pili ni Wewe mwenye chombo cha moto na ambaye ndio unakata bima, na mtu wa tatu ni YULE ANAYEDHURIKA KUTOKANA NA MATENDO YA MTU WA PILI, yaani mwenye chombo cha moto au wakala wake.

Wakala wa mwenye chombo anaweza kuwa dereva wa mwenye chombo, mtoto wa mwenye chombo, au yeyote aliyepewa kuendesha chombo hicho. Hivyo dereva kama chombo si chake, anakuwa wakala wa mwenye chombo.

Katika mkataba huo wa bima Mtu wa kwanza Kampuni ya bima) na mtu wa pili (Mwenye chombo) huingia mkataba kwa malipo kidogo yaitwayo "Premium"kwaajili. Ya mtu wa tatu asie julikana moja kwa moja

4. KWA NINI MTU WA KWANZA (KAMPUNI YA BIMA) NA MTU WA PILI (MWENYE CHOMBO) WAINGIE MKATABA KWAAJILI
YA MTU WA TATU?

Watu hawa wawili (first and second party) wanaingia mkataba kwa ajili ya mtu wa tatu, ili ikitokea mtu wa pili kamsababishia madhara mtu wa tatu. Huyo mtu wa kwanza aweze kubeba gharama au fidia za madhara yaliyosababishwa na mtu wa PILI kwa mtu wa TATU.

5. KWA NINI MTU WA TATU AKATIWE BIMA NA MWENYE
CHOMBO (MTU WA PILI)?
Mtu wa tatu (yeyote aliyepo barabarani) anakatiwa bima na mwenye chombo kwakuwa mwenye chombo ana jukumu la kumlipa fidia mtu anayemuumiza. Yaani wewe Juma(dereva bodaboda) ukinipakiza kwenye bodaboda yako ikatokea umenidodosha na mie kuumia basi ujue una wajibu wa kunilipa fidia kwa maumivu uliyonisababishia.

Au ikitokea wewe Juma umegonga chombo changu cha moto au umemgonga
mwanangu, basi ujue una wajibika kunilipa. IKIWA utakuwa na bima ya third party gharama za matengenzo ya bodaboda uliyoigonga, matibabu ya uliowagonga nk vyote
vitabebwa na kampuni ya bima.

Wewe jukumu lako litakiuwa ni kutoa taarifa tu kwa kampuni ya bima kuwa umesababisha
ajali. Lakini kama utakuwa hauna bima ya third party ina maana gharama hizi zote utazibeba wewe mwenyewe.

6. KWA NINI SASA SERIKALI IMEWEKA ULAZIMA HUO WA
KUKATA BIMA?
Serikali imeweka ulazima wa kuwa na hiyo bima kwenye vyombo vya moto ili kuwakinga wananchi wake wanaoumzwa na wenye vyombo vya moto. Pia ni sehemu ya kuwawajibisha wenye vyombo vya moto kubeba gharama za madhara waliyoyasababisha. Mwenye chombo cha moto asingepewa jukumu hili, serikali ingekuwa inaingia gharama kubwa sana kugharamia madhara yaliyosababishwa na wewe dereva au
mmiliki wako.

7. KWA HIYO JE, BIMA YA THIRD PARTY INAKUKINGA WEWE NA CHOMBO CHAKO?
Kama tulivyokwisha kuona hapo juu, jibu ni HAPANA. Bima ya third party hailipi gharama za madhara ya kuharibika chombo chako au wewe mwenyewe kuumia, bali inalipa gharama za madhara ya kuharibika chombo cha mtu mwingine au mali ya mtu mwingine kuharibika.

8. JE, ILI BIMA INISAIDIE MIMI NA CHOMBO CHANGU
NATAKIWA NIKATE BIMA IPI?
Ili usaidike wewe na chombo chako unatakiwa kukata BIMA MSETO (COMPREHENSIVE) au wengine huita BIMA KUBWA Bima hii kubwa faida yake ni kwamba kukitokea ajali wewe
ukauma, chombo chako kikaharibika na pia mali ya mtu mwingine ikaharibika na mtu mwingine kuumia, basi wote nyie gharama zitabebwa na bima hii. Bima hii bei yake ni kubwa kidogo kuliko ile ya third party. Na bima hii sio ya lazima.

9. HITIMISHO
Kwa hiyo bima ya third party sio kwaajili yako wewe na chombo chako, bali ni kwaajili ya watu wengine na mali zao, ambazo wewe unaweza kuziharibibu au kuwaumiza kutokana
na udereva wako. Kwa ufupi ndio kusema kwamba ikiwa umepata ajali kwa kumgonga mtu mwingine na chombo chako kimeumia, basi ile bima yako ya third party itamlipa yule
aliyeumia, lakini wewe haitakulipa. Gharama za kujitibia wewe binafsi na matengenezo ya chombo chako utajigharamia wewe mwenyewe. Ila kama una bima kubwa, basi itakugharamia na wewe
#NiHaki Yako KufikaSalama

Kwa mawasiliano ya mashauri zaidi ya bima 0765827355

Sent using Jamii Forums mobile app
 
de paymer,
Third party akiuliwa kwenye ajali iliyosababishwa na gari yenye bima mseto, nini stahiki za marehemu.
 
Stahiki za marehemu watapata wategemezi wake na hii itamuuliwa na mahakama. Malipo yote ya bima yanayo husisha third party mahakama lazima itoe judgement kuhusu stahiki

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kesi ipi mkuu maana kesi ya msingi ni traffic ambayo sio linganifu na kesi ya madai.

Fafanua kidogo tafadhali
 
Nisaidie kuelewa ni kesi ipi inatoa maamuzi ndugu wa marehemu walipwe nini na kampuni ya bima?

Je ni ile ambayo dereva aliyefanya ajali na kusababisha kifo au kuna kesi nyingine inapaswa kufunguliwa?
Kama marehemu ni third party na alifarikia katika ajali ya gari na hilo gari lilikua na bima ndogo or kubwa basi baada ya mahakama kutoa maamuzi wategemezi wa marehemu watanuafika na kiasi kitakachoamuliwa na mahakama kutolewa kwa wategemezi, na hicho kiasi kitatolewa na kampuni ya bima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama marehemu ni third party na alifarikia katika ajali ya gari na hilo gari lilikua na bima ndogo or kubwa basi baada ya mahakama kutoa maamuzi wategemezi wa marehemu watanuafika na kiasi kitakachoamuliwa na mahakama kutolewa kwa wategemezi, na hicho kiasi kitatolewa na kampuni ya bima

Sent using Jamii Forums mobile app
Nitajie kesi inayotoa uamuzi huu initwaje na inafunguliwa na nani.

Kesi ya awali ni ya traffic ambayo hufunguliwa na jamhuri kupitia askari wa kikosi cha usalama barabarani ambao humshitaki aliyetumia barabara kwa uzembe na kuwa chanzo cha ajali (kesi hii ni ya jinai)

Ufafanuzi tafadhali.
 
Nitajie kesi inayotoa uamuzi huu initwaje na inafunguliwa na nani.

Kesi ya awali ni ya traffic ambayo hufunguliwa na jamhuri kupitia askari wa kikosi cha usalama barabarani ambao humshitaki aliyetumia barabara kwa uzembe na kuwa chanzo cha ajali (kesi hii ni ya jinai)

Ufafanuzi tafadhali.
KUHUSU KESI ZINAZOHUSIANA NA MADAI YA BIMA.
UNACHOPASWA KUFAHAMU NI KUWA katika kudali malipo ya bima kutokana na ajali za barabarani kuna kesi mbili.Na kesi hizi zinazotokana na mazingira au mwenendo wa kampuni ya bima au mdaiwa.

Inapotokea ajali barabarani anayewajibika wa kwanza kabisa ni DEREVA, na anayewajibika wa pili ni MMILIKI. Kama mmiliki huyo huyo ndiyo dereva basi atawajibika yeye mwenyewe kwa kusababisha hiyo ajali.

AINA YA KESI.
Kesi ya kwanza ni kesi ya kitrafiki(Traffic Case).
Kesi hii hufunguliwa na askari(Jamhuri) dhidi ya dereva aliyekuwa alkiendesha gari hadi wakati wa wa wa ajali. Kimsingi kesi hii inamhusu dereva kukiuka taratibu za sheria ya usalama barabarani na kupelekea AJALI. Kesi hiyo inaendeshwa huko mahakamani na sio lazima majeruhi awepo, ukikutwa na hatia unafungwa au kulipa faini.

Kama mtuhumiwa akilipa faini basi faini hii inaingia serikalini kama mapato ya serikali sawa tu na pesa ya notification. Yule majeruhi anakuwa halipwi chochote. Maana lile ni kosa dhidi ya jamhuri.

Baada ya hapo yule majeruhi anakwenda POLISI anapewa vielelezo vya ile kesi na kupeleka katika kampuni ya bima kudai bima. Kampuni ya bima baada ya kupokea vielelezo hivyo itaamua kulipa au kutolipa kulingana na taratibu zake.

KESI YA PILI.
Kesi hii sasa ni kesi ya madai ambapo majeruhi au mwathirika wa ajali anakwenda mahakamani kufungua kesi ya madai mahakamani dhidi ya dereva kama mshtakiwa wa kwanza, na mwenye mali kama mshatakiwa wa pili, akidai fidia kutokana na madhara aliyoyapata.

Hapo ndipo atasema anadai shilingi ngapi kutokana na nini. Katika hatua hii baada ya kuona ameshtakiwa Mmiliki anaweza kuiambia mahakama kuwa gari lake lilikuwa na bima hivyo anaomba kumuunganisha kampuni ya bima (Insurer) kwenye kesi.

Na akikubaliwa atauinganisha kampuni hiyo ya bima kama mshatakiwa wa tatu kwenye kesi hiyo.

Mdai Akiweza kudhibitisha madai yake na mahakama kumkuta mmiliki ana hatia, basi ile pesa aliyotakiwa kulipa mmiliki italipwa na kampuni ya bima.

Utaratibu wa kudai fidia kupitia kesi ya madai haumlazimishi mwathirika wa ajali (mdai) kuanza kwanza kuidai kampuni ya bima ikikataa ndipo afikishe suala hilo mahakamani. Naweza kuamua kwenda moja kwa moja mahakamani mara tu ile kesi ya trafiki itakapoisha kule mahakamani.

Au anaweza kuchukua nyaraka polisi akaenda kwenye kampuni ya bima kudai fidia akaona anazungushwa au akaona anachotaka kulipwa ni kidogo kuliko madhara aliyoyapata, akaamua keuelekea mahakamani.

Ni matumaini yangu umepata mwanga walau wa aina hizi mbili za kesi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KUHUSU KESI ZINAZOHUSIANA NA MADAI YA BIMA.
UNACHOPASWA KUFAHAMU NI KUWA katika kudali malipo ya bima kutokana na ajali za barabarani kuna kesi mbili.Na kesi hizi zinazotokana na mazingira au mwenendo wa kampuni ya bima au mdaiwa...
Kwenye bima kitu inaitwa Cover note ni nini na hutumika wakati gani.
 
Means bima hawasubiri shuruti ya mahakama kulipa stahiki za wahanga au bado sijakuelewa?
Bima zote zitalipwa kwa muhanga wa janga ila Kama janga litahusishwa kwa third party basi mahakama itasubiriwa kutoa shuruti.

Kwa maana hiyo ni kwamba kama umekata bima dhidi ya chombo cha moto ukapata ajali na ulikua na bima kubwa basi kampuni ya bima itakulipa madhara yaliotokea katika gari yako ila kama ulisababisha madhara kwa mtu wa tatu (third party) basi kampuni ya bima itasubiri shuruti kutoka mahakaman ni kiasi gani huyu mtu wa tatu atapaswa kulipwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
de paymer Ahsante sana kwa somo. Tunaweza kuwa tunajua ufanyaji kazi wa "third party", lakini ulivyotiririka hapa umetuongezea mengi sana.

Usichoke na maswali yetu. Hapo mkuu kwenye kesi ya kwanza, ina maana dereva asipokutwa na hatia majeruhi hawezi tena kudai fidia?

Na vipi kuhusu zile habari za ajali kutokea na dereva kakimbia (hajapatikana), je ndiyo kusema majeruhi hawezi kudai fidia?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom