Nimeomba mkopo CRDB, kabla ya kupewa wameanza kunikata hela kila mwezi. CRDB shida nini?

test man

JF-Expert Member
Aug 13, 2016
1,013
948
Nimeomba mkopo tangu mwezi wa tatu na nikakamilisha process zote maana mimi ni mtumishi wilaya x cha ajabu mwezi wa nne wamenikata kwenye mshahara na tena mwezi wa tano wamenikata hela yangu cha ajabu hata kwenye account hawajaniwekea hiyo hela niliyokopa nimefuatilia mpaka nimechoka kila nikipiga simu wananiambia suala linashughulikiwa mpaka lini?.

Mbona bank zingine haziko hivyo na waliniambia mshahara wangu nibadilishe account nilikuwa NMB nikahamia huko CRDB mnachonifanyia mnakosea si haki kabisa kuwa hivyo mnafeli wapi?

Maana mara mniambie mtandao unasumbua Mbona mshahara mnaingiza hela na kwenye makato mko makini huu ni utapeli kabisa kutoka bank ya CRDB angalieni salary slip ya mwezi huu lkn kwenye account yangu hawajaweka hata mia ya mkopo nilioomba.
 
Sio hivyo tu, ingawa wametoa gawio huwa wanachelewa sana kuweka dividends hizo kwenye account za wanahisa tofauti na makampuni mengine!

Huduma za matawi yake mengine zimeanza kuzorota sio kama zamani; mfano ni tawi la Oystebay lilikuwa na huduma nzuri sana kabla ya mabadiliko yenu mlipomuondoa Manager JULIANA nasikia kahamia Lumumba branch!!

Alipokuwa Oysterbay watu wengi walikimbilia kufanya transactions na branch ile kwasababu management yake ilikuwa customer friendly!!! Try to improve your services to your customers.
 
Nimeomba mkopo tangu mwezi wa tatu na nikakamilisha process zote maana mm ni mtumishi wilaya x cha ajabu mwezi wa nne wamenikata kwenye mshahara na tena mwezi wa tano wamenikata hela yangu cha ajabu hata kwenye account
Wabongo tupunguze woga na kudai haki zetu Mahakamani pale tunapoona tumekosewa na umejaribu kutafuta suruhu bila mafanikio. Kwa hiki unachosema ni ushahidi tosha kuwa unaonewa ila cha ajabu huwezi kuthubutu kufika hata tu kwenye masijala ya mahakama kujua kama unaweza kuanzisha kesi udai haki yako. Mtafute Mwanasheria uende Mahakamani. Punguza unyonge Mkuu.
 
CRDB ni kweli sometime wanafeli hasa issue za mikopo kuna case nyingine mtu anachukua mkopo afu hawamkati muda unaenda mara unashangaa huwezi tena ku access account yako wanaifunga ukienda kuuliza wanakwambia ulikuwa hukatwi kwa hiyo una arrears za kulipa huo muda ambao walikuwa hawakukati sas unashangaa hilo kosa ni la nani la kwako au la kwao?

Mzozo unaanzia hapo coz ukilegea wanakata mshahara wotee na usipofutailia hutaona senti na akaunti yako itaendelea kutofanya any transactions. Sijui kuna tatizo gani malalamisho ni mengi inabidi wajipange upya au kuna janja janja fulani ya baadhi ya watumishi humo kitengo cha mikopo.
 
Wabongo tupunguze woga na kudai haki zetu Mahakamani pale tunapoona tumekosewa na umejaribu kutafuta suruhu bila mafanikio. Kwa hiki unachosema ni ushahidi tosha kuwa unaonewa ila cha ajabu huwezi kuthubutu kufika hata tu kwenye masijala ya mahakama kujua kama unaweza kuanzisha kesi udai haki yako. Mtafute Mwanasheria uende Mahakamani. Punguza unyonge Mkuu.
Yaani hii ingekuwa majuu huyu angevuta mpinga mrefu sana. Alafu benki ingechunguzwa kuona kama kuna watu wengine wamefanyiwa hivi Ili walipwe nao.

Inawezekana kuna watu wameshakula pesa ya huyu jamaa
 
Ametoka Charles Kimei ameingia Charles Kimeo
Nimeomba mkopo tangu mwezi wa tatu na nikakamilisha process zote maana mimi ni mtumishi wilaya x cha ajabu mwezi wa nne wamenikata kwenye mshahara na tena mwezi wa tano wamenikata hela yangu cha ajabu hata kwenye account hawajaniwekea hiyo hela niliyokopa nimefuatilia mpaka nimechoka kila nikipiga simu wananiambia suala linashughulikiwa mpaka lini?.

Mbona bank zingine haziko hivyo na waliniambia mshahara wangu nibadilishe account nilikuwa NMB nikahamia huko CRDB mnachonifanyia mnakosea si haki kabisa kuwa hivyo mnafeli wapi?

Maana mara mniambie mtandao unasumbua Mbona mshahara mnaingiza hela na kwenye makato mko makini huu ni utapeli kabisa kutoka bank ya CRDB angalieni salary slip ya mwezi huu lkn kwenye account yangu hawajaweka hata mia ya mkopo nilioomba.
 
Hawa ndo wasomi wetu,hawajuj umuhimu wa Mahakama,hawajui haki zao,hawajui uonevu.
Wao ni kulalamika tu. Mwananchi,mkulima,mfanyakazi,msomi wote ni kulalamika tu.
 
CRDB, hicho kilio na wilayani kwangu wanaokatwa kbl ya kuwekewa pesa ni wengi mnoo, NMB ni bank bora sn tatizo ni riba zao tu mm sizielewi
 
Wabongo tupunguze woga na kudai haki zetu Mahakamani pale tunapoona tumekosewa na umejaribu kutafuta suruhu bila mafanikio. Kwa hiki unachosema ni ushahidi tosha kuwa unaonewa ila cha ajabu huwezi kuthubutu kufika hata tu kwenye masijala ya mahakama kujua kama unaweza kuanzisha kesi udai haki yako. Mtafute Mwanasheria uende Mahakamani. Punguza unyonge Mkuu.
Huko nako unataka Mwenzako akapigwe pesa tena na wajanja wa Sheria!!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kiufupi, hawana cash.
Wanasubiri deposits ndio walipe dividends (NB. ukitangaza dividend sehemu ya faida inageuka kuwa deni, kulipa deni lazima uwe na cash). Kutoa mikopo mipya mtasuburi sana, mark my words.
 
Nenda mahakamani ila kabla tafuta mwanasheria mzuri hata malipo ya milioni tu ukishinda kesi watakulipa hela ndefu balaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom