Msaada wa Kisheria: Hati ya nyumba ya familia ilitumika kukopewa mkopo CRDB pasipo famila kujua

Mzungujr

Member
Mar 14, 2016
13
6
Mzee(Baba) alitumia Hati ya Nyumba ya familia kukopea mkopo CRDB Milion 9 pasipo wanafamilia kujua(alikopa kwa siri bila kufata utaratibu) na sahihi ya mke(Mama) ilifojiwa.

Kama familia tumegundua baada ya marejesho kukwama ambapo alikuwa tayari kabakiza deni la Milion 6 na Laki 3. Mpaka sasa mkataba wa marejesho umeisha na nyumba inataka kuuzwa na mzee mwenyewe kakimbia na watu wa benki tayari wamegundua walifanya makosa ila wanatukandamiza kwa sababu hatujui sheria vizuri.

Naombeni msaada wa kisheria, nifanyeje?
 
Tumia huo ushauri hapo juu ndugu ndiyo suluhu ila muwe na uhakika kama mama hakupiga saini zuio litafanyika
 
Mkipata Mwanasheria mzuri mtashinda hiyo kesi. Bank ilibidi waongee na mama ili kuhakikisha naye anakubaliana na mumewe kuitumia nyumba ili kupata bank. Bank hawakufanya hivyo na baba yenu akafanya forgery kujipatia pesa nyingi kwa njia ya udanganyifu. Poleni sana, mgangamare msikubali kupoteza nyumba yenu kirahisi rahisi.
 
Duh?
Nyumba inauzwa kwa kukopa 9mil tu??
Hebu changamka weka zuio mahakamani huku ukitafuta suluhisho mkuu!!
 
Tumeweka pingamizi tayari mahakaman na CRDB hawajatoa jibu juu ya pingamizi hilo,na kilichotushangaza zaidi tarehe 27 June 2016 (Jumatatu iliyopita) walipita na kipaza sauti mtaani kwetu wakitangaza mnada wa nyumba na kesho yake tarehe 28 June 2016 walikuja nje ya nyumba wakapaza sauti eti wapo na mteja hapo na nyumba imenunuliwa tayari kwa Milion 10 wakawasha gari nakuondoka,Sasa nashindwa kuelewa inakwaje wanafanya iv na kesi bado ipo mahakamani.
Iv walivyofanya ni sahihi au ?
Na kesho tarehe 4 July 2016 ndo siku iliyokuwa imewekwa na mahakama kwenda kusikiliza majibu ya pingamiz
 
Waongo hao nyumba haiwezi kuuzwa bila mnada wa hadhara. Haiwezekani mtu ajitokee tu na mteja aseme walishapata mteja. Pili kabla ya kuuza nyumba walitakiwa watoe notisi ya kusudio la kuuza nyumba
 
Back
Top Bottom