Msaada wa Haraka Tafadhali: Ungonjwa wa akili

njamayo

Senior Member
Jan 6, 2012
150
40
Habari wana JF,

Kijana wangu wa kiume wa miaka 16 alianza kulalamika anaona madudu madudu toka mwaka 2016. Tulimpeleka MNH kitengo cha magonjwa ya akili. Ikaonekana alikuwa na stress na ndo maana limempata la kumpata.
Ni hivi: kuna kipindi anaona vitu visivoelezeka, yeye anasema anaweza kueleza akiwa ktk hiyo hali tu. inachukua km sekunde 30 inaisha. baada ya hapo anakuwa kawaida. hiyo hali ikimtokea aliye karibu hawezi kugundua chochote hata kama akikuambia tizama. pia ikitokea anakuwa anajisikia vibaya. kwa ufupi ni kuwa hana maelezo ya kujitosheleza. na bado anapata tiba hapo MNH.
Basi kama kuna mwanaJF mwenye uzoefu au habari ya hili naomba msaada please.

asanteni,
njamayo
 
Mtafutieni na tiba mubadala vtu vingine vigumu si vya kuonekana kwa macho ya ugali haya. Hafu kuona vtu visivo vya kawaida huhitaji macho ya rohoni chunguzeni asili yenu ooooh. Pia fanyeni ibada
 
Hayo anayo o a kwabkipindi hicho ndiyo dalili tosha kabisa kuwa stress inampelekea jamaa kuwa na ugonjwa wa amili kamili.IWAPO MUHIMBILI INAKUWA NGUMU MLETE MIREMBE DODOMA NDIO HOSPITALI YA RUFAA UA MAGONJWA YA AKILI NA KICHWA HUTA JUTA NA PIA ILIPONE VYEMA HAPASWI KUACHA KUMEZA DAWA HADI PALE DAKTARI ATAKAPO ONA INAFAA
 
Magonjwa ya akili hayana tiba labda km amerogwa anaweza pona kuna wataalam wa kienyeji,ila km yamejileta ynyw hawezi pona
 
Magonjwa ya akili hayana tiba labda km amerogwa anaweza pona kuna wataalam wa kienyeji,ila km yamejileta ynyw hawezi pona
Nyinyi ndiyo mnapotosha jamii. Magonjwa ya akili ni kama magonjwa ya mwili yakipata tiba sahihi hupona. Tiba huchukua muda mrefu, unaweza kuwa kwenye dose kwa miaka 3-5.
 
Mtafutieni na tiba mubadala vtu vingine vigumu si vya kuonekana kwa macho ya ugali haya. Hafu kuona vtu visivo vya kawaida huhitaji macho ya rohoni chunguzeni asili yenu ooooh. Pia fanyeni ibada
 
Sky Eclat,

eeh bado anaendelea na tiba ya mnh. ngoja nitafute taarifa za hapo Lutindi Hospital.

asante.

Magonjwa ya akili yanachukua muda mrefu kupona. Rudini Muhimbili au kuna hospitali ya Rutheran Lushoto inaitwa Lutindi pia wana tiba nzuri kwa magonjwa haya.
 
Hello NZURI PESA,

bado anapata tiba, hawezi acha. eeh mirembe napajua. tutatia timu ikibidi. asante.

Hayo anayo o a kwabkipindi hicho ndiyo dalili tosha kabisa kuwa stress inampelekea jamaa kuwa na ugonjwa wa amili kamili.IWAPO MUHIMBILI INAKUWA NGUMU MLETE MIREMBE DODOMA NDIO HOSPITALI YA RUFAA UA MAGONJWA YA AKILI NA KICHWA HUTA JUTA NA PIA ILIPONE VYEMA HAPASWI KUACHA KUMEZA DAWA HADI PALE DAKTARI ATAKAPO ONA INAFAA
 
ooh..

Mshana Jr yupo humu JF? au sehemu gani. inaweza ikawa uchawi/majini? dogo anasema ni stree tu.
Yupo humu humu JF, mtafute.

Pia nimekupa ushauri toka moyoni, sio ufikiri nimekupa ushauuri kwa kejeli au masihara mkuu, nimesikitika sana yanayo/yaliomkuta mkuta kijana wako.

Kijana mwenye miaka 16 ni ngumu sana kupatwa msongo wa mawazo (stress), kichwa chake bado hakija komaa kuwaza majukumu/starehe/mapenzi. Labda kuwe na matatizo;

1) Nyumbani kuwe na matatizo makubwa ya kifamilia. (Ugomvi baina ya mama na baba kila kukicha au anateswa sana nyumbani kupelekea kuathirika kisaikolojia).

2) Anaonewa/kupigwa/kufanyiwa mambo yasio endana na umri wake, kama vile kuteswa/kuonewa/kunyanyaswa (Rafiki zake/mtu baki/ shule bila sababbu na anaogopa kukwambia). Kupelekea yanamuathiri kisaikolojia. Jaribu kupeleleza hili pia kwa undani zaidi.

3) Maswala ya kishirikina/uchawi/majini. Vitabu vya dini vimeyataja haya na vinayatambua kua yapo na yanadhuru binaadam.

Nawasilisha,
 
Nyinyi ndiyo mnapotosha jamii. Magonjwa ya akili ni kama magonjwa ya mwili yakipata tiba sahihi hupona. Tiba huchukua muda mrefu, unaweza kuwa kwenye dose kwa miaka 3-5.
Ukweli ni kwamba hayaponi kuna jilani yangu kakaa milembe si chini ya miaka miwili lkn mpk leo nikienda kumjulia khali sioni mabadiliko
 
Ukweli ni kwamba hayaponi kuna jilani yangu kakaa milembe si chini ya miaka miwili lkn mpk leo nikienda kumjulia khali sioni mabadiliko
Inawezekana hata huko hawakumpa tiba sahihi. Magonjwa haya huhitaji hali ya utulivu na dose usiikose kila siku. Ubongo unavyofanya kazi ni kama waya umeme, matatizo huketa short. Dawa zinajenga taratibu sana short hii.
Ukiwa na mgonjwa inabidi uwe mvumilivu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom