Obama wa Bongo
Kuna mambo mawili nayaona hapa.
1. Inawezekana alikuwa kwenye mahusiano, ameshika ujauzito, sasa anataka auhalalishe kwako na muendelee na utaratibu wenu wa ndo.
Ushauri: Nenda Pharmacy, nunua vipimo kama viwili, mwambie apime ujauzito. Hii itakuondolea shaka juu ya hili.
2. Binadamu tunatofautiana kimaumbile. Inawezekana mwenzako anajisikia hamu ya tendo la ndoa. Ameamua kuwa muwazi kwako, badala ya kuwa anapoozea pembeni, anataka wewe ummalizie haja zake na hiyo Dec 2014 anaiona kuwa ipo mbali.
Ushauri: Ukiwa baba au mume mtarajiwa, kaa na mke/mchumba/mpenzi wako. Msaidie kwa ushauri na ikibidi mharakishe kuwa pamoja baada ya kubarikiwa kanisani na kufanya sherehe ili muishi kama wana ndoa.
Conclusion:
Unatakiwa kui-manage hii hali. Usijiingize kwenye malumbano, heshimu hisia zake. Lakini pia unatakiwa uwe makini na ushauri wa kwanza hapo juu, kwani ilishawahi mtokea rafiki yangu.
Mwanamke alishinikiza ndoa haraka, walikuwa hawajawahi fanya tendo la ndoa. Ndoa ikafungwa. Baada ya mwezi shemeji akatangaza mimba. Baada ya miezi 4 wazazi wake wakamhitaji arudi nyumbani kwa sababu ya mambo ya kimila akijifungulie kwa bibi yake kijijini. Tukamwambia mshikaji akatae. Akakataa asiende. Ndani ya miezi 6 shemeji akaenda kujifungua hospitali. Mume akaduwaa na kabla hajaingia kumwona mtoto ndugu wa shemeji (mke) wakawahi kumtoa hospitali. Wakasingizia ni njiti. Mume na mimi tukafuatilia walikompeleka, tukakuta mtoto yupo poa na mwenye afya njema. Hatukusema kitu, tukaondoka na hapo ndio ikawa mwisho wa ndoa, mwanamke hakurudi kwa mume wake, na mume akendelea na hamsini zake.