Godbless taarifa yako ni ya uwongo na uzushi. Nasema hivyo kwasababu zifuatazo:
Kwenye mradi huo Serikali ya Tanzania haichukui mkopo wowote kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo..... Laiti ingekuwa inachukua mkopo mkataba husika ungesainiwa baina ya Serikali na Benki ya Exim ya China au benki nyingine yoyote au serikali ya china. Mkataba uliosainiwa ni baina ya Serikali na Kampuni itakayowekeza kwenye ujenzi wa bandari na eneo huru la viwanda. Kampuni hiyo CMHI ni moja ya makampuni makubwa duniani yanayowekeza kwenye bandari. kampuni hii inamiliki bandari 5 kati ya bandari kubwa 10 duniani.
Hoja ya pili ya kwamba makampuni ya China ndio yatajenga, haikutajwa kwenye mkataba wowote.....Godbless unabashiri tu. Hata hivyo, mwekezaji huyo anao uhuru wa kuchagua kampuni yoyote ile duniani kujenga bandari hiyo. Vigezo vitakuwa ni uwezo, ujuzi, uzoefu wa kujenga bandari na sio swala la uzalendo. Ni vigezo vya aina hiyo vinatumiwa na makampuni mengi nchini kama vile NSSF,PSPF, UTT na Tanroads kuchagua wakandarasi.....na mara nyingi wameishia kuchagua wakandarasi wenye uwezo na sio uzalendo. Tunachotakiwa ni kuwajengea uwezo wakandarasi wetu waweze kushindana na wenzao wa China. Wapo wakandarasi wazawa ambao wameanza ku teamup na wageni ili kupata uzoefu. Hiyo ndio njia bora ya kusonga mbele.
Tatu, madai ya kutakiwa kuendesha bandari kwa miaka 50 sio kweli. Kama Serikali imechukua mkopo kama Godbless anavyodai, iweje wachina waendeshe bandari? Si mtu ukichukua mkopo wajibu wako ni kulipa mkopo kwa aliyekukopesha? Wajibu huo wa kuendesha bandari unatokea wapi? Hapa ndio hoja ya godbless ya kwanza inagongana na hoja ya tatu. Ukweli ni kwamba kilichosainiwa juzi ni Framework Agreement inayotoa mwongozo na kuelezea wajibu wa kila upande katika mazungumzo ya kufikia mkataba wa kuanza kutekeleza mradi wenyewe. (Framework agreement lays down terms and conditions for future contracts). Hivyo hawajafikia mahala pa ku determine uwekezaji huo unafanyikaje, mgawanyo wa hisa ukoje, gharama ya mradi ni zipi? Zinalipwaje? zinarejeshwaje? In the process patakuwa na mikataba mingi tu baina ya mwekezaji na mamlaka ya bandari, Mamlaka ya EPZA, Tanesco, Tanroads, Railways etc
Nne, hoja ya kwamba kusiwepo bandari nyingine yoyote ni uwongo na uzushi mtupu. Nasema hivyo kwasababu tayati kwa umbali huo zipo bandari zinazo function-Tanga, Dar es salaam na Zanzibar. Mkataba huo hauwezi kuweka kipengele cha aina hiyo kwasababu kikiwepo maana yake hata Zanzibar ambapo kuna independent jurisdiction katika masuala ya bandari nao wasijenge au kuendeleza bandari.
Hoja ya tano, juu ya upanuzi wa gati 13 na 14 ya bandari ya dar es salaam imenisaidia kufahamu msingi wa thread hii ya Godbless. Huyu bwana inaonekana ni wale majeruhi wa lile dili la ujenzi wa gati 13 na 14 ambalo walitaka kazi ya usd 100 million ifanywe kwa usd 200 million. Waziri mzalendo Omar Nundi alistukia dili hilo, akalisimamisha.......wale wote walioahidiwa mgawo na waliokula mgawo wa awali mpaka leo hawaamini deal lao limekufa na wanajaribu kupinga kila mradi ambao utafanya deal lao liwe irrelevant.
Mikataba iliyosainiwa wala haina hila zozote.....ni mikataba straight. Kama haujasoma sema ufafanuliwe badala ya ku speculate