Msaada wa China: Haya ni baadhi tu ya masharti

Msaada wa China: Haya ni baadhi tu ya masharti

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2010
Posts
855
Reaction score
1,224
Wana JF,

Taarifa hii nimeipata sehemu na nimeona tushirikishane kwa nia ya kupata ushahidi zaidi juu ya Masharti ambayo Serikali ya China imetoa kwa Tanzania katika kile kilichotajwa kuwa Misaada isiyo na masharti magumu kwa nchi yetu.

"MAPYA ZAIDI YA MIKATABA KATI YA CHINA NA TANZANIA YAANZA KUBAINIKA"

Hebu soma kwa makini moja Kati ya mikataba 17 ya China na Tanzania waliyoisaini kufuatia ziara ya Rais wa China nchini Xi Jinping.

Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika vimebainisha masharti ambayo yameambatana na Moja ya Mkataba ulisainiwa ambao umelenga katika UJENZI WA BANDARI YA BAGAMOYO.
Mosi, Ili kufanikisha ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Serikali ya Tanzania itachukua mkopo wa fedha toka serikali ya Uchina.

Pili, Makampuni ya China na Injinia wao ndio watapaswa kupatiwa tenda ya ujenzi wa mradi huo.

Tatu; Serikali ya watu wa China watatakiwa kuendesha bandari bandari hiyo kwa muda wa miaka 50 ili Kurudisha mkopo uliotolewa kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.

Nne; Itatakiwa kuwa kwa umbali wa Kilometa 200 za mraba Kusini, Mashariki, Magharibi na Kaskazini kusiwepo na na bandari ya namna hiyo wala kuendeleza bandari ya namna hiyo.

Kwa maana hiyo bandari ya Dar es Salaam ,Tanga na Mtwara kwa mantiki hii hazitapanuliwa wala kuboreshwa ili kutoa nafasi ya Bandari ya Bagamoyo iwe ya kwanza kwa ubora na hii itadumu kwa kipindi cha miaka 50.

Tano; Upanuzi wa bandari wa Gati 14 wa Bandari ya Dar es Salaam umesimamishwa au utasimamishwa ili kuipa ama kuheshimu na kulinda mkataba wa wachina kwa bandari ya BAGAMOYO

Hizo ni baadhi ya dondoo za mkataba mmoja tu.

Naomba wenye taarifa juu ya hili JF watuweke wazi, maana maaana China ya Mao na Tanzania ya Myerere sio za sasa. Kuna mabadiliko makubwa sana ya sera za kiuchumi.
 
Basi tujengee wewe hiyo bandari bila masharti

Kaka unaonekana ni kijana mwenye busara na hekima. Rejea katika matamshi ya Xi na Viongozi wetu juu ya hili, Kilichotamkwa ni kwamba misaada ina masharti nafuu lakini masharti hayo hayakuwekwa bayana ili tupime unafuu wake kwa Tanzania. Sasa unapodai nijenge mimi hiyo bandari napata mashaka na hili. Tafakari kabla ya ku reply bro.
 
in short kwa wachina hakuna neno 'donor' wala 'development partner'.

Naona masharti yanafanana na yale ya bandari ya Mtwara. Membe alituhakikishia kuwa tusiwe na wasiwasi wapo makini
 
Basi tujengee wewe hiyo bandari bila masharti
Huyu bwana Lukosi ndo aina ya watu wanaoweza hata kuuza wake zao ilimradi ameona hela. Sitashangaa ikiwa huyu mtu anajiusisha na biashara yoyote haramu, ndio maana kawasaliti CHADEMA ili mafisadi wake kwenye magamba wamlinde na uchafu wake. Watu kama hawa ndio wale wanaokimbiaga vivuli vyao
 
natamani sana bandari ya mtwara. kwani kuna kilometa ngapi mtwara mpaka bwagamoyo? bandari moja ni ukiritimba. mikoa ya lindi na mtwara gharama zitakuwa juu kusafirisha mizigo. bandari ingine ijengwe mtwara. kuna mbadala wa mchina kujenga bandar? gharama zikoje? ONGEZENI BANDARI MTWARA.
 
kama kuna mtu anae jua zaidi kuhusu hili tunaomba atujuze pliz
 
Hivi kwanini hawa viongozi wetu hawana huruma na nchi yao? kama hayo ndiyo kweli yaliyomo humo basi ni ukweli ulio wazi

kwamba hao ndio wanongóa ndugu zetu meno na kucha bila ganzi.
 
Basi tujengee wewe hiyo bandari bila masharti
hivi kama haya yaliyo andikwa hapa ni kweli, wewe unaona hiyo ni sawa, hiv wewe ni timamu kweli? unafanya utani katika maslai ya taifa, wewe lazima unamatatizo makubwa sana, labda tu kilicho andikwa kiwe si ukweli!
 
Kaka unaonekana ni kijana mwenye busara na hekima. Rejea katika matamshi ya Xi na Viongozi wetu juu ya hili, Kilichotamkwa ni kwamba misaada ina masharti nafuu lakini masharti hayo hayakuwekwa bayana ili tupime unafuu wake kwa Tanzania. Sasa unapodai nijenge mimi hiyo bandari napata mashaka na hili. Tafakari kabla ya ku reply bro.
Mkuu mikataba ambayo haikupitia bungeni ijadiliwe ionekane kama ina maslahi kwa taifa letu, unategemea nini???? Tumeuzwa mazima mazima tukae tukijua hilo, sijui tutapata faida gani, Bagamoyo kuna reli ya kusafirisha mizigo au ni mtindo wa maroli ya kina Ritz1????

Basi tujengee wewe hiyo bandari bila masharti

Kwa mtu mvivu kama wewe uliyezoea vya kunyonga utaona kujenga sisi wenyewe ni kama muujiza, lakini sivyo. Vitu kama hivi vinawezekana kabisa lakini nchi inatakiwa iwe ni viongozi wenye vision na wachapa kazi, sio hawa waswahili wavivu wa pwani wanaoongoza. Ulaya kuna nchi zenye population la less than six million people na wanafanya maajabu ije kuwa sisi. Anyaway kwa wavivu kama wewe na Kikwete hiyo haitawaingia akilini kwani mmezoea bure...
 
Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika vimebainisha masharti ambayo yameambatana na Moja ya Mkataba ulisainiwa ambao umelenga katika UJENZI WA BANDARI YA BAGAMOYO.

Tano; Upanuzi wa bandari wa Gati 14 wa Bandari ya Dar es Salaam umesimamishwa au utasimamishwa ili kuipa ama kuheshimu na kulinda mkataba wa wachina kwa bandari ya BAGAMOYO

Naomba wenye taarifa juu ya hili JF watuweke wazi, maana maaana China ya Mao na Tanzania ya Myerere sio za sasa. Kuna mabadiliko makubwa sana ya sera za kiuchumi.

Mnakurupuka na kuweka thread za kuamsha hisia za wananchi? tuwekee nakala ya huo mkataba hapa tujadili vinginevyo itabakia tetesi.
 
  • Thanks
Reactions: Lui
Ndiyo mambo aliyoyakataa Mugabe. Yaani wazawa Zimbabwe walikuwa wanalima kwenye mawe(udongo usio na rutuba) halafu
wawekezaji walikuwa wanalima ardhi yenye rutuba.

Hii ni hatari kwa Tanzania.

Hivi hao waliosaini hawakuona hatari kwa siku zijazo yaani kuanzia 2014. Kweli Nchi imeuzwa kama wana JF walivyolalama

Hao wanaojiita wasomi sioni hata msaada wao miaka 50 yaani kusiwepo Bandari tena nchini hiyo ya Bagamoyo halafu wanaona sawa tu.

Nchi vitu vya kuwekwa wazi wanaficha. Kwanini Mkataba usiwekwe wazi nasi tuutolee maoni?
 
Kamakweli masharti ndio hayo, bola nibadili uraia tu bongo simahala salama kimaisha.
 
Back
Top Bottom