Msaada wa China: Haya ni baadhi tu ya masharti

Msaada wa China: Haya ni baadhi tu ya masharti

Maswali;
1. Tanzania itanufaika vipi na bandari hiyo kwa kipindi cha miaka 50 watakayokuwa wanaiendesha wachina?
2. Tanzania itakosa nini katika kipindi hicho?
3. Tanzania itacontrol vipi ubora wa ujenzi wa bandari hiyo? Kama kampuni ya kichina itashindwa kujenga kwa kiwango kinachotakiwa, nini kitafanyika?
4. Tanzania itahusika vipi na kupatikana kwa mkandarasi wa kichina?
5. Kama gharama za ujenzi kwa kampuni za kichina zitakuwa significantly above kampuni zingine duniani, Tanzania itakuwa na uwezo wa ku-appeal?
6. Baada ya miaka 50 ya wachina kuiendesha, wanatakiwa waiache bandari hiyo katika hali gani? Je, kama itakuwa haipo kwenye viwango vilivyokubaliwa, Tanzania itafanya nini?
7. Katika matumizi ya bandari hiyo kwa miaka 50, Je, Tanzania na watanzania wataruhusiwa kuitumia kuingiza na kutoa bidhaa? Nani atapanga bei ya huduma hiyo?
8. Endapo Tanzania akipata hizo hela na kuamua kuilipa China siku yeyote kabla ya kuisha hiyo miaka 50, yapi masharti husika?
Wachina watakuwa wanalipa kodi (na kiasi gani) kwa serikali ya Tanzania kwa kipindi hicho cha miaka 50 watakapokuwa wanaiendesha?
9. Endapo uhitaji wa matumizi kwa bandari zingine zilizopo ndani ya km 200 utaongezeka, bandari hiyo ya Bagamoyo inaahidi kutoa huduma hiyo kwa niaba, bila kuathiri wahitaji?
10. Endapo uwepo wa bandari hiyo utaathiri utendaji wa bandari zingine, hasa upatikanaji wa wateja, je Serikali ya China itafidia hilo kwa kipindi cha miaka hiyo 50? (hapa namaanisha kuwa serikali ya Tanzania inaweza kupoteza mapato kwa wateja watakaoamua kuhamia bandari ya Bagamoyo, ambayo itakuwa inaendwshwa na wachina)...
 
Nimefurahishwa sana na mtoa hoja pia nmefurahishwa sana na mjibu hoja kwa kulitumia jukwaa vizuri
 
Basi tujengee wewe hiyo bandari bila masharti

Kah!! My GOD!! Wewe Bwana LUKOSI kumbe una Mawazo finyu kiasi hiki. Elimu yako ni ya wapi kutokuweza kupambanua hoja na kuijadili badala ya kutoa majibu mepesi mepesi kama ya Mh Wasira wa "MAGAMBA"?
 
Hii ua pengine jenga Bagamoyo itatumaliza sisi wengine. bagamoyo-Bagamoyo. Nia hii si njema. Kwanini hili lisiwe kuendeleza na kupanua hata bandari zilizopo.
 
Basi tujengee wewe hiyo bandari bila masharti

Nadiriki kusema kuanzia nijiunge jf hii ndo pumba kali kuliko zote..nakusamehe bure maana sijui umri wako ila akili hizi ni akili za mtoto wa chekechea..
 
Inawezekama kuijenga wenyewe bila mashart, ila wakubwa hawata kula 10% sasa, ndio maana wanaingia mikataba ambayo atapata chake mapema, kisha atambaeeeeee

Basi tujengee wewe hiyo bandari bila masharti
 
Mkuu mikataba ambayo haikupitia bungeni ijadiliwe ionekane kama ina maslahi kwa taifa letu, unategemea nini???? Tumeuzwa mazima mazima tukae tukijua hilo, sijui tutapata faida gani, Bagamoyo kuna reli ya kusafirisha mizigo au ni mtindo wa maroli ya kina Ritz1????

Hivi
kwani bunge ni nini hasa mbele ya serikali yetu-kwangu nadhan ni mkutano tu wa kujadili matumiz na kidogo tu kujadil mapato
 
Hata kwako nyumbani kama hujaonesha ujasiri kwa mumeo au mkeo lazima kuna vidume au vidumu watakupindua tu! hakuna lisilo wezekana........viongozi wetu wanajali maslahi yao tu, mfano sioni sababu ya kuuingiza nchi katika madeni kujenga bandari mpya bagamoyo, wakati tuna bandari 3 ambazo hatuzitumii ipasavyo?....... sasa wenzio wanajaribu kujenbga hoja, wewe umekiwsha kijakatia tamaaa? ovto kabisa

niki kuita mfuu ntakuwa sijakosea....ila kiukweli unawaza kwa kutumia kalio....
 
Basi tujengee wewe hiyo bandari bila masharti
ukiwa na njaa unakuwa na uwezo wa kufikiri kama zuzu, ww huoni kwamba watanzania hatutakuwa na bandari kwa miaka 50. Jaribu kuficha upumbavu wako Lukosi
 
Kama masharti ndio hayo imekuaje yakaitwa masharti nafuu? Miaka 50 ya Wachina kuendesha hiyo bandari ni mingi sana. Hii ina maana gani? Lazima tuwe makini hapa.
 
Mbona hayo ni masharti ya kawaida kabisa. Ingekuwa nchi za Magharibi ingekuwa zaidi
 
Wote waliosaini na kukubali masharti hayo wanajijua hawatakuwepo baada ya hiyo miaka 50

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
hivi kama haya yaliyo andikwa hapa ni kweli, wewe unaona hiyo ni sawa, hiv wewe ni timamu kweli? unafanya utani katika maslai ya taifa, wewe lazima unamatatizo makubwa sana, labda tu kilicho andikwa kiwe si ukweli!


Hata kama yaliyoandikwa sio kweli hilo sio jibu la mtu mwenye ubongo
 
Mkuu mbona nasikia ameshaanza kujenga bandari kavu pale kwa babu yake,yaani hawa jamaa naona wameamua kufunga

kazi kabisa yaani tz imekuwa yao!..
Mkuu mikataba ambayo haikupitia bungeni ijadiliwe ionekane kama ina maslahi kwa taifa letu, unategemea nini???? Tumeuzwa mazima mazima tukae tukijua hilo, sijui tutapata faida gani, Bagamoyo kuna reli ya kusafirisha mizigo au ni mtindo wa maroli ya kina Ritz1????

 
Back
Top Bottom