Wapendwa wana JF na wataalamu wa mambo ya harufu.
Mimi huwa sihisi/sisikii harufu ya aina yoyote toka niwe na fahamu sasa sijui kama ni tatizo au ni kawaida kwa baadhi ya binadamu.
Toka nikiwa shuleni nitasikia wenzangu wanalalamika kuna mtu kajampa ambapo mie sijasikia sauti ya kijampo nashangaa naamua kujumuika nao kulalamika.
Kuna siku wife alinishangaa alivyonikuta ndani nimekaa wakati kulikuwa na harufu ya panya alieoza.. Nikasingizia naumwa mafua, akamtafuta akampata.
Ukweli huwa sisikii harufu yoyote nikiwa peke yangu nakula nikibanwa najampa. Huwa nashangaa utasikia mtu anakwambia kuna maharage au viazi vinaungua.
Au kuna stafeli humu ndani limeiva n.k. Huwa najiuliza wao wanatambuaje? Wataalamu naomba mnifahamishe kama ni tatizo nini tiba yake, na kama sio tatizo nifanye nini ili nisikie hizo harufu?
Kuna wakati nikipita sehemu chafu utasikia tumbo linauma na kichwa kugonga.
Natanguliza shukrani wakuu..