Msaada: Natokwa na harufu mbaya sana sehemu za siri

Enol

Senior Member
Aug 24, 2018
113
86
Habari wadau wa Jf,

Mimi ni kijana wa kiume 28yrs old.Tatizo langu kubwa imekuwa ni harufu nzito na mbaya inatoka sehemu zasiri(yaani haivumiliki).Yaani suruali na boxer nikivaa siku moja ya pili nikirudia harufu inazidi zaidi.

Nateseka sana na hii hali jamani na nimeishi nayo kwa miaka mingi tangu 2006 mwezi wa kumi nikiwa form one. Ilianza tu ghafla nikawa nasikia harufu flani kwa mbali baadae ilienda inaongezeka na ikawa nzito kiasi cha kutumia maisha yangu kutoroka sana shule maana darasani nilikuwa nakaa kwa tabu sana.

Harufu huwa inazidi inapotokea nimepiwa na jua au kukaa sehemu yenye joto basi hata nikienda kaa sehemu harufu huwa nzito na ni mbaya saa zingine ni mithili ya kiatu kichafu cha mtu mwenye miguu ya fangasi.

Lakini nikiangalia kwenye pu...mb hakuna hali yoyote ya ugonjwa ila nashangaa harufu inatoka kali mno na nikiwa uchi huwa siisikii ila napotia nguo basi naanza kuisikia harufu.Kikubwa huwa nikikaa basi joto kwenye p***mb huwa kubwa sana kiasi mpaka kiti nilichokalia ukigusa panakuwa na joto sana.Hata nikioganikivaa basi naisikia kwa mali na kadri mda unavoenda basi inazidi kuwa kali na nzito kiukweli ni mateso makali mno kisaikolojia nayapata kiasi cha kukata tamaa na nawaza kujitoa roho mda mwingi.

Yaani ikitokea nikatumia maji kuchamaba toileti aisee nikishavaa basi harufu hyo huzidi ni kama nakuwa nimeongezea kiasi kwamba nashindwa hata kaaa na watu kazini.nimekuwa kama mu anaetembea kiukweli.

Nimejaribu kutumia limao,ndimu lakini wapi na ukitumia pafyume au vitu vya marashi huko aisee hali ndio huwa mbaya mno yaan nazalisha harufu mara mia zaidi ya awali.

Nimeshajaribu dawa za fangasi lakini wapi na hata hao fangasi sina ila n basi tu na madawa mengi ya hospitali haijasaidia.Hospitali nimeenda mara nyingi na wanasema sina tatizo lolote lile.

Nateseka sana mno nashindwa hata kukaa kwa amani mbele za watu hata ma ofisini kiasi kwamba maisha yangu yamekosa thamani naishia kuwaza kujiua tu.

Na hali hii ilianza ghafla tu mpaka nahisi nilirogwa maana sikuwaga nayo kabla ya 2006 mwezi wa 10 huko shuleni.Huenda kosa langu ilikuwa ni kuwa smart class tu.

Nimehangaika mno sijapata njia ya kujikomboa kwa hii miaka 12.
naombeni kwa yoyote anaeweza kunisaidia nipate suluhisho ili maisha yangu yawe na thamani maana naona mungu kanijalia vitu vingi ila nimewekewa kimoja cha kufanaya maisha yangu yasiwe kitu tena bali kifo tu ndio nakiona sasa.

Poleni kwa gazeti lakin ndio hayo napitia mtanzania mwenzenu.

Mshana Jr,watalaamu wengine na yeyote yule mwenye njia naombeni msaada wenu. kwa sasa njia yoyote nitafanya ili nitoke hii hali maana si maombi wala dawa zimenisaidia aisee na nilishawahi kwenda kwa mgannga flani nae akala tu hela hakunisaidia alinambia nimerogewa mynama anaitwa fungo ila sikutibika.
===

USHAURI ULIOTOLEWA NA WADAU WA JF
Unapotoka kuoga usivae nguo mpaka maji yote mwilini yakauke. Ukivaa nguo kabla ya maji kukauka mwilini (hasa hasa sehemu za siri ) itasababisha maji kujifyoza kwenye nguo na kizalisha harufu ya uvundo.

Harufu itakua inaongezeka kadri muda unavyoyoma kwa sababu ya joto linalosababishwa na huo uvundo na kufanya sehemu hizo zitoe jasho kwa kasi kubwa. Unaweza ukakaa karibu na feni kabla ya kuvaa nguo ili mwili uwe mkavu kwa 100% ndipo uvae nguo
---
Nimeshangaa unaposema huwa unarudia suruali na boxer.

Asee kurudia boxer ni kosa kubwa sana. Hiyo tu inaweza kukuletea harufu za ajabu. Suruali pia kama ndo utaratibu wako kurudia basi usirudie kwa mfuatano. Yaani ukiivaa leo usiiva kesho itundike ipate hewa na uje uivae walau baada ya siku mbili.

Kitu kingine unapaswa kuoga si chini ya mara mbili kwa siku.

Pia unapojiitawaza jitahidi ujitawaze kwa sabuni basi kama waona harufu ni kali.

Kuna tatizo kubwa kwa sisi wanaume kutokijuiosha katikati ya makalio vizuri na hii hupelekea wanaume wengi kuwa na harufu kali makalioni au chini ya pumbu pale.
---
Usafi tu ndo dawa mkuu.

Jitahidi ku shave chini kila wkend alafu pakaa mafuta ya nazi. Badilisha aina ya boxer/chupi unazotumia. Pendelea kutumia za cotton tu na usirudie. Yaani ukivaa leo kesho vaa nyingine safi ile ifue vzr na uanike juani.

Usivae nguo nyingi ndani ya trouser. Unakuta mtu anavaa boxer, kaptura, pensi na suruali hapana. Baa boxer then suruali au chupi then suruali basi. Hakikisha unaoga asbh na jioni alafu tumia medicated soap zinasaidia sana kukata jasho. Ukioga jisugue kwa dodoki pia. Pia kunywa maji mengi. Fanya hvyo kwa wiki tu then leta mrejesho japa... Pole

Sent using Jamii Forums mobile app
---
Pole sana mdogo wangu Enol. Naomba ufanye haya, ambayo binafsi nilifanya baada ya kupatwa na tatizo linataka kufanana na lako. Chukua Nazi 2 kwa kuanzia. Vunja na kuna Nazi zote kisha tengeneza tui. Liache tui mpaka cream ijitenge na maji. Kisha chukua hiyo cream jipake sehemu yote ya siri na pembezoni (kwenye mapaja).

Jipake vizuri kabisa asubuh mara baada ya kuoga, na uendelee na shughuli zako. Jioni pia jipake na lala kwa amani kabisa. Na cream inayobaki uwe unahifadhi kwenye jokofu.

Au kama unamfahamu anayekamua mafuta ya Nazi bila kuyachemsha, kachukue na ufanye hivyo. Nina hakika na naamini utapona vizuri kabisa. Pole sana.
 
Kaka pole sana kwa unapotia..hilo ni jini na uchawi umetupiwa na Damu na jina la Yesu pekee yake ndio mkombozi wako.. tafuta kanisa lolote ambalo wanamwamini Yesu kwa dhati utapona... ni swala la dkk chache sana wala husikate tamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabla ya kwenda huko bado ana nafasi ya kutibiwa na akapona kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka pole sana kwa unapotia..hilo ni jini na uchawi umetupiwa na Damu na jina la Yesu pekee yake ndio mkombozi wako.. tafuta kanisa lolote ambalo wanamwamini Yesu kwa dhati utapona... ni swala la dkk chache sana wala husikate tamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Muelekezeni dawa sio huo ujinga. Suala la yesu ni suala la ki imani je inakuaje kama yeye si mtu wa imani hiyo? Nyie ndo mnaowashaurigi watu waache kutumia arv bali wamtumainie yesu. Upumbavu kabisa.
 
Nimeshangaa unaposema huwa unarudia suruali na boxer.

Asee kurudia boxer ni kosa kubwa sana. Hiyo tu inaweza kukuletea harufu za ajabu. Suruali pia kama ndo utaratibu wako kurudia basi usirudie kwa mfuatano. Yaani ukiivaa leo usiiva kesho itundike ipate hewa na uje uivae walau baada ya siku mbili.

Kitu kingine unapaswa kuoga si chini ya mara mbili kwa siku.

Pia unapojiitawaza jitahidi ujitawaze kwa sabuni basi kama waona harufu ni kali.

Kuna tatizo kubwa kwa sisi wanaume kutokijuiosha katikati ya makalio vizuri na hii hupelekea wanaume wengi kuwa na harufu kali makalioni au chini ya pumbu pale.
 
Nimeshangaa unaposema huwa unarudia suruali na boxer.

Asee kurudia boxer ni kosa kubwa sana. Hiyo tu inaweza kukuletea harufu za ajabu
Kwa binadamu wa kawaida kurudia suruali ni kawaida.rejea sare za shule.tatizo ni harufu isiyovumilika.ukijitawaza yaani ni balaa hata nitumie nini.harufu inakuwa nzito sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom