Elimu ya Kinywa: Usafi wa meno na kinywa kwa ujumla, sababu, kinga na tiba za harufu mbaya

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,252
113,645
Napenda sana meno meupe na yaliyopangika vizuri. Na kwa bahati nzuri nimejaaliwa kuwa na vyote viwili pasipo na msaada wa dental braces wala retainers. Na meno ya njano njano huwa yananichefua kabisa.

Usafi wa kinywa kwangu ni jambo muhimu kupita maelezo. Nikisafiri na kuwa mbali na nyumbani kwangu huwa nasononeka kiaina kwa sababu huwa nashindwa kufanya usafi wa kinywa vile ambavyo nifanyavyo nikiwa kwangu.

Hivyo basi, kwa manufaa ya wengi, nimeonelea vyema kuanzisha uzi huu ili kuweza kubadilishana mbinu na maarifa mbalimbali yahusuyo usafi wa kinywa.

Kwa aliye na swali lolote kuhusu huo usafi, kwa moyo mkunjufu kabisa unakaribishwa kuuliza.

Aliye na ufahamu au maarifa yoyote yale yanayoweza kuwafaa wengine, nawe karibu sana. Unaweza kuchangia kwa kutuambia ni bidhaa gani unatumia, vitu [zana] unavyotumia, mganga [dentist au orthodontist] yupi wa meno ambaye hupendelea kwenda, na mengineyo mengi.

=========
1582623931992.png


1582623970142.png


3f113f14239e5579756b9c92c7fc9770_XL.jpg


Afya ya kinywa ina umuhimu mkubwa zaidi ya unavyoweza kufikiria na kwa ujumla inaweza kutoa ufahamu kuhusiana na jinsi afya yako ya mwili ilivyo. Kuelezewa uhusiano uliopo kati ya afya ya kinywa na afya ya mwili mzima kunasaidia kufahamu umuhimu wa kutunza kinywa na hasa meno na fizi. Kama zilizo sehemu nyingine za mwili, kinywa nacho kimejaa bakteria ambao wengi wao hawana madhara.

Kwa kawaida mfumo wa kulinda mwili na utunzaji mzuri wa kinywa kama vile kupiga mswaki na kutumia uzi kuondoa uchafu katika meno kunaweza kudhibiti bakteria walioko kinywani wabakie katika hali ya kawaida na kutodhuru kinywa. Lakini bila kutunza vyema kinywa, bakteria hao wanaweza kusababisha maambukizo na kusababisha meno kuoza na maradhi ya fizi.

Afya ya kinywa inajumuisha siha na namna ya utunzaji wa sehemu zote za mdomo hasa meno na fizi. Mbali na kinywa kutuwezesha ipasavyo kula, kuzungumza na hata kuwa na muonekano mzuri wa uso, meno na fizi zinapaswa zisiwe zimedhurika na kuwa na matatizo kama vile meno kuoza, magonjwa ya fizi, kung'oka meno na mdomo kunuka.

Kuoza meno na meno kuwa na matundu ni matatizo ya kinywa yanayoshuhudiwa sana miongoni mwa watu. Sababu zinazoweza kuzuia matatizo hayo ya meno ni kudumisha usafi wa kinywa, kupata fluoride ya kutosha na kutokula kwa wingi vyakula vinavyoweza kudhuru meno na kusababisha matundu.

Afya ya meno na kinywa kwa ujumla inahusiana na afya ya mwili mzima kwa njia tofauti. Kwanza kabisa uwezo wa kutafuna chakula na kukimeza ni muhimu ili mwili uweze kupata virutubisho muhimu vya kujenga mwili. Halikahalika kuwa na kinywa chenye matatizo kunaweza kuathiri namna mtu anavyozungumza na hata kujiamini kwake. Matatizo ya meno yanaweza kumsababishia mtu gharama kubwa ya matibabu na ukarabati wa meno.

Sababu zinazoweza kuathiri afya ya kinywa
Uimara wa meno na fizi unatofautiana kati ya mtu na mtu, na umbo la taya, mdomo, meno na hata kiasi cha mate. Hayo yote ni mambo muhimu yanayoweza kuainisha kwa nini baadhi ya watu meno yao yanaoza zaidi kuliko wengine. Baadhi ya meno yanaweza kuwa na vishimo na nyufa zinazoweza kuruhusu bakteri na tindikali kupenya kwa urahisi na baadhi ya wakati umbo la taya huweza kuzuia meno yasisafishike vizuri na kuondoa vyema uchafu kinywani.

Kiwango na namna mate yalivyo pia huweza kuathiri uozaji wa meno. Kwa mfano matundu na nyufa huwa haziko sana katika meno ya mbele ambako kuna mate mengi ikilinganishwa na meno ya nyuma. Bakteria wote walioko kinywani wanaweza kubadilisha wanga kuwa tindikali lakini aina ya streptococci na Lactobacili wana uwezo mkubwa wa kutengeneza tindikali.

Kuwepo kinywani vijidudu vya aina hii huongeza uwezekano wa meno kuoza. Baadhi ya watu wana kiasi kikubwa cha bakteria wanaosababisha meno kuoza kuliko watu wengine na hii ni kutokana na kuzembea katika kutunza na kuimarishwa usafi wa kinywa.

Wataalamu wanatwambia kuwa, usafi wa kinywa na matumizi ya dawa za meno zenye fluoride hupunguza kasi ya meno kuoza. Usafi wa meno ni pamoja na kupiga mswaki kila siku kwa kutumia dawa za meno zenye flouride, kutumia uzi wa meno kusafisha eneo lililo kati ya meno, kuchokonea meno kwa kijiti ili kundoa mabaki ya chakula na kufanyiwa uchunguzi wa meno mara kwa mara.

Flouride huzuia kupungua madini katika molekuli za meno, kuongeza madini hayo kwenye meno na kuimarisha meno ili yasiathiriwe na tindikali. Matumizi ya fluoride kwa kiwango kinachotakiwa huzuia na kudhibiti matundu kwenye meno.

Flouride inaweza kupatikana kutoka katika maji ya kunywa na baadhi ya vinywaji vilivyoongezwa mada hiyo. Pia mada hiyo hutiwa katika dawa za mswaki, geli na dawa za kusafishia kinywa. Katika baadhi ya nchi mada ya fluoride huongezwa hata katika chumvi na maziwa.

Kiwango cha flouride katika maji ya kunywa na vyakula kinapaswa kuzingatiwa kwa mujibu wa mahitaji ya mwili. Suala hili ni muhimu kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 6 ambao meno yao bado yanakua. Kutumiwa sana au kwa kiwango kikubwa mada hiyo husababisha matatizo katika enamel au mfupa wa jino hali inayojulikana kinaalamu kama kama fluorosis.

Vyakula na athari yake katika kuoza meno
Ijapokuwa katika nchi nyingi kuoza meno kumekuwa kukiambatanishwa na matumizi ya fluoride na utunzaji wa kinywa, aina ya vyakula anavyokula mtu pia ni jambo muhimu linalochangia meno kuoza. Jinsi chakula chenyewe kilivyo kwa mfano kama kinanata na kung'ang'ania kwenye meno pia husababisha meno kuoza. Vyakula vinavyong'ang'ania kwenye meno kama vile bisikuti na crips huongeza uwezekano wa kuoza meno kwani hubakia juu ya meno kwa muda mrefu zaidi kuliko vyakula vingine.

Pia vyakula vyenye sukari zinazoyeyuka kwa haraka husafishwa kwa wepesi kinywani na mate, na kila vyakula vyenye wanga vinavyokaa muda mrefu kinywani na kuzunguka meno, ndivyo bakteria wanavyopata fursa zaidi ya kutengeneza tindikali na kuondoa madini katika meno. Kila tunapokula vyakula vyenye wanga, bakteria walioko kwenye kinywa huanza kutengeneza asidi suala linalopelekea meno kuoza.

Mwenendo huu huendelea hadi baada ya dakika 10 hadi 20 baada ya kula au kunywa. Katika kipindi tusichokula au kunywa mate huzimua tindikali na kusaidia kurejesha madini katika meno. Iwapo vyakula au vinywaji vitaliwa mara kwa mara na kinywa kisipate muda wa kurejesha madini kwenye meno, hapo ndipo meno huanza kuoza.

Kwa ajili hiyo tunashauriwa kutokula na kunywa wakati wote na pia kupunguza kula vyakula vyenye wanga na sukari kwa uchache tusile vyakula hivyo zaidi ya mara 6 kwa siku. Pia tunashauriwa kuhakikisha kuwa tunapiga mswaki meno kwa kutumia dawa za meno zenye fluoride, kwa uchache mara mbili kwa siku.

Mmomonyoko wa meno
Mmomonyoko wa meno ni kuharibika tishu ngumu ya juu ya meno kutokana na acidi bila kuathiriwa na bakteria wanaosababisha meno kuoza. Kuna vyakula na vinywaji vingi vyenye tindikali katika lishe zetu na kuna uwezekano suala hilo likatuathiri. Kwa mfano kupendelea sana kula vyakula au kunywa vinywaji vyenye tindikali husababisha mmomonyoko wa meno. Tatizo hilo lisiposhughulikiwa huweza kuathiri ufanisi wa kinywa na hutofautiana baina ya watu.

Ili kuepukana na tatizo hilo tunashauriwa kujiepusha kupenda sana kunywa vinywaji au kula vyakula vyenye acidi na kupiga mswaki kwa uchache mara mbili kwa siku kwa kutumia dawa ya mswaki yenye fluoride. Pia tunashauriwa kutopiga mswaki mara tu baada ya kunywa au kula chakula chenye acidi kwani kufanya hivyo huweza kuyafanya meno yaharibike kutokana na kusugua meno wakati tindikali ikiwemo kinywani.

Pia ni bora tujizoeshe kutafuna chingamu au ubani mara tu baada ya kula vyakula vyenye acidi ili kufanya mate yatengenezwe ambayo husaidia kuondoa acidi mdomoni.

========
Michango ya wadau

Binafsi nilikua nina matatizo ya kinywa hasa damu kutoka kwenye fizi(involuntary gum bleeding) na pia kuwa na mate machungu sana pindi niamkapo asubuhi.

Nilimuona daktari akaniambia nina ukurutu kwenye meno so akaniambia tiba ni kuutoa kila baada ya miezi mitatu wakanikwangua huo ukurutu lakini haikua tiba kwa hilo tatizo langu.

Nikaenda kwa daktari mwingine akanichunguza na akaniandikia dawa ambazo kwa mshangao ni dawa za kawaida tu za antibiotic,kwa mshangao kabisa lile tatizo lilikwisha kabisa,lakini baada ya miezi kama sita lilirudia tena,niliporudi tena pale hospital kwa nia ya kumuona yule daktari kwa bahati mbaya akawa ameacha kazi katika ile hospital ikabidi nimuone daktari mwingine japo sikupenda huduma yake kwani mimi nilikwenda pale kwa nia ya kupewa zile dozi nilizotumia mara ya mwisho lakini huyu daktari mpya hakunipa na kile cheti nilikipoteza kwa hiyo sikuwa na ujanja wa kwenda kununua dawa kwenye maduka ya dawa.

kitu nilichojifunza ni kwamba tuwe tunapiga mswaki angalau mara mbili kwa siku,asubuhi kama kawaida na usiku kabla ya kulala kwani kwa kiasi kikubwa tutapunguza hili tatizo hasa la harufu mbaya ya kinywa na pia tuwe tunatumia sana mboga za majani,binafsi nikila mboga za majani hasa usiku huwa ninaamka na kinywa safi tena bila hata harufu,ni nzuri sana kutumia hebu jaribuni kula mbogamboga muone faida yake.

Mwisho,kwa mujibu wa yule daktari wa pili ni kwamba, tusipende sana kutumia mouth wash mara kwa mara kwa kuwa na zenyewe huleta kama ganzi fulani kwenye ulimi,kwa hiyo ukiitumia sana inaweza ikakupa ganzi itakayokufanya usiweze kungamua ladha kwa haraka,hii ni kwa mujibu wake lakini sina uhakika nayo kwa kuwa toka nimeshauriwa sijaitumia na ilikua mapema mwaka 2008.

Huu ndio uzoefu wangu.
----
Adui namba 1 wa meno ni sukari na sukari inakaribisha bacteria ambao wakiwa wamezoeshwa hiyo sukari basi hupiga kambi kwenye meno.

Hivyo sukari kwenye chai na vinywaji au vyakula vyenye sukari kama doughnuts, cocacola ukitumia lazima ufahamu kwamba ukienda kulala bila kupiga mswaki na kusafisha kinywa basi bacteria wataendelea kula mabaki 24/7 na ndio unaona jino linachimba.

Wenye tatizo la fizi wanatakiwa wamwone hygienist ambae atakushauri namna ya kupiga mswaki na dawa za zinazofaa kutumia.

Hayo maduka ya uzunguni yanaweza kuwa na dawa aina mbalimbali hasa za Uingereza (GlaxoSmithKline - GSK) zenye kazi mahsusi kushughulikia meno likiwemo tatizo la unjano.

Mbali ya dawa maarufu ya Colgate kuna dawa zingine maalum kama vile Oral- B White, Oral B expert, Sensodyne, Pronamel, Corsodyl Daily Original Toothpaste 75ml na Colgate MaXWhite.

Hygienist anashauri namna ya kuondoa uchafu kwenye meno na matabaka au plaque na kuepusha kuoza kwa meno au tooth decay. Pia anashauri vyakula vya kuepuka kula ambavyo vinaharibu meno kwa kasi ya ajabu kama vile chips mayai, vinywaji baridi kama bia na soda.

Hii inasaidia sana kwa wale ambao wana matatizo ya meno ambayo mengine ni ya kurithi.
 
Kiutalaam kabisa, mtu inakupasa kutumia mswaki kwa muda gani?

Muda pendekezwa wa wataalamu ni miezi mitatu. Ila ni vizuri kuangalia mswaki wako na kuona una hali gani kabla hata hiyo miezi mitatu haijatimia. Na kama unaona unahitaji mswaki mpya basi unaubadilisha.

Unawezaje kuwa na meno meupe kabisa kama meno yako yana unjanonjano?

Hapa nadhani inategemea na sababu ya huo unjano ni nini.

Kama sababu ni unywaji wa kahawa, unywaji wa mvinyo, uvutaji sigara, n.k, basi ni kuacha kutumia vitu hivyo kwa wingi huku ama ukienda kwa tabibu wa meno ili yakasafishwe au ukitumia bidhaa za kufanya meno yako yawe meupe.

Ila kama sababu ni ya kuzaliwa nayo basi hapo inakuwa ngumu sana.
 
Nimekuja kugundua Tz tunatumia dawa za meno fake tofauti na Kenya ambao wanatumia dawa nzuri za meno. How to overcome this ili kuepuka madawa fake ya meno? Ambayo hayasaidii hali ya usafi katika kinywa zaidi ya kuozesha na kuleta maumivu.
 
Napiga mswaki mara mbili kwa siku asubuhi na usiku kabla ya kulala, pia baada ya kupiga mswaki huwa nasukutua mdomo kwa kutumia mouth wash ya listerine.

Dawa za meno ambazo naona ziko vizuri ni Colgate, sensodine na close up ila ni muhimu kununua original.
 
Nimekuja kugundua tz tunatumia dawa za meno fake tofauti na Kenya ambao wanatumia dawa nzuri za meno. How to overcome this ili kuepuka madawa fake ya meno? Ambayo hayasaidii hali ya usafi katika kinywa zaidi ya kuozesha na kuleta maumivu

Kama unataka dawa nzuri ze meno jaribu kwenda kwenye supermarkets kama Village supermarket [Mbezi beach, Oysterbay, na Masaki kama sijakosea] na Shoppers supermarket [Mikocheni - Mwai Kibaki Rd, Masaki - Haile Selassie Rd, na Mbezi Beach - Kanisa Rd].

Hao najua kwa uhakika bidhaa zao nyingi huwa wanaleta kutoka Uingereza na ni za ubora wa hali ya juu.
 
Kama unataka dawa nzuri ze meno jaribu kwenda kwenye supermarkets kama Village supermarket [Mbezi beach, Oysterbay, na Masaki kama sijakosea] na Shoppers supermarket [Mikocheni - Mwai Kibaki Rd, Masaki - Haile Selassie Rd, na Mbezi Beach - Kanisa Rd].

Hao najua kwa uhakika bidhaa zao nyingi huwa wanaleta kutoka Uingereza na ni za ubora wa hali ya juu.
Shukrani sana kwa kunitajia maeneo, nilikuwa nanunua dukani aisee.
 
Napiga mswaki mara mbili kwa siku asubuhi na usiku kabla ya kulala, pia baada ya kupiga mswaki huwa nasukutua mdomo kwa kutumia mouth wash ya listerine. Dawa za meno ambazo naona ziko vizuri ni Colgate, sensodine na close up ila ni muhimu kununua original.

Kiongozi, kupiga mswaki mara mbili ni jambo jema sana.

Ila hata upige mswaki mara 10, hiyo peke yake tu haitoshi.

Inatakiwa pia u-floss meno yako. Yaani uyasafishe na nyuzi nyembamba ili kutoa mabakibaki ya chakula yanayonasa katikati ya meno.

Juu ya hilo unatakiwa pia ukwangue ulimi wako na kikwangua ulimi. Bakteria wengi waletao harufu mbaya kinywani hupenda kujibanza kwenye ulimi hususan kwa nyuma.

Kwa hiyo ukipiga mswaki na kufanya hayo mengine, tatizo la harufu mbaya ya kinywa utakuwa umeliweza.

Pia ni muhimu sana kuhakikisha mdomo unapata oksijeni ya kutosha siku nzima. Hivyo ni vyema kunywa maji mara kwa mara.
 
Kuna mtu wangu wa karibu sana amabe yeye hupiga mswaki kila asubui na anapolala usiku lakini hua anakua na harufu mbaya sana ya mdomo..tatizo linaweza kua ni nini na anawezaje kupata tiba ya hilo tatizo mkuu.

Kupiga mswaki tu peke yake si ufumbuzi wa harufu mbaya.

Rejea bandiko namba 12 hapo juu.
 
Asante sana kwa ushauri wako mkuu, nimewahi kutumia electric toothbrush ambayo ilikua na matokeo chanya kuliko mswaki wa kawaida.
 
Binafsi nilikua nina matatizo ya kinywa hasa damu kutoka kwenye fizi(involuntary gum bleeding) na pia kuwa na mate machungu sana pindi niamkapo asubuhi.

Nilimuona daktari akaniambia nina ukurutu kwenye meno so akaniambia tiba ni kuutoa kila baada ya miezi mitatu wakanikwangua huo ukurutu lakini haikua tiba kwa hilo tatizo langu.

Nikaenda kwa daktari mwingine akanichunguza na akaniandikia dawa ambazo kwa mshangao ni dawa za kawaida tu za antibiotic,kwa mshangao kabisa lile tatizo lilikwisha kabisa,lakini baada ya miezi kama sita lilirudia tena,niliporudi tena pale hospital kwa nia ya kumuona yule daktari kwa bahati mbaya akawa ameacha kazi katika ile hospital ikabidi nimuone daktari mwingine japo sikupenda huduma yake kwani mimi nilikwenda pale kwa nia ya kupewa zile dozi nilizotumia mara ya mwisho lakini huyu daktari mpya hakunipa na kile cheti nilikipoteza kwa hiyo sikuwa na ujanja wa kwenda kununua dawa kwenye maduka ya dawa.

kitu nilichojifunza ni kwamba tuwe tunapiga mswaki angalau mara mbili kwa siku,asubuhi kama kawaida na usiku kabla ya kulala kwani kwa kiasi kikubwa tutapunguza hili tatizo hasa la harufu mbaya ya kinywa na pia tuwe tunatumia sana mboga za majani,binafsi nikila mboga za majani hasa usiku huwa ninaamka na kinywa safi tena bila hata harufu,ni nzuri sana kutumia hebu jaribuni kula mbogamboga muone faida yake.

Mwisho,kwa mujibu wa yule daktari wa pili ni kwamba, tusipende sana kutumia mouth wash mara kwa mara kwa kuwa na zenyewe huleta kama ganzi fulani kwenye ulimi,kwa hiyo ukiitumia sana inaweza ikakupa ganzi itakayokufanya usiweze kungamua ladha kwa haraka,hii ni kwa mujibu wake lakini sina uhakika nayo kwa kuwa toka nimeshauriwa sijaitumia na ilikua mapema mwaka 2008.

Huu ndio uzoefu wangu.
 
Mwisho,kwa mujibu wa yule daktari wa pili ni kwamba, tusipende sana kutumia mouth wash mara kwa mara kwa kuwa na zenyewe huleta kama ganzi fulani kwenye ulimi,kwa hiyo ukiitumia sana inaweza ikakupa ganzi itakayokufanya usiweze kungamua ladha kwa haraka,hii ni kwa mujibu wake lakini sina uhakika nayo kwa kuwa toka nimeshauriwa sijaitumia na ilikua mapema mwaka 2008.

Huo ushauri wa mouthwash sikubaliani nao.

Tokea niko mdogo kabisa hata darasa la kwanza sijaanza nilikuwa natumia mouthwash na mpaka leo hii mbona sina tatizo la maonjo!
 
Back
Top Bottom