Msaada: Ushauri kuhusu hii mirathi

Pips Man

JF-Expert Member
May 9, 2014
1,438
2,000
Wakuu ipo hivi,

kwetu tulizaliwa wawili tu mimi mkubwa na mdogo wangu wa kike, nipo naishi dodoma pamoja na familia yangu yaani naishi na mke wangu mama na mdogo wangu.

Mzee wangu alifariki miaka 3 iliyopita hivyo aliacha baadhi ya mali km nyumba 3 na mashamba, nyumba mbili zipo dodoma hizi hazina shida wala mashamba tunayamiliki bila shida yoyote balaa lipo kwenye nyumba moja ambayo ipo Dar es Salaam Sinza.

Hapo Sinza ilipo iyo nyumba ndio mzee wangu alipozaliwa kwao walikuwa wawili tu wote wakiume yeye mzee wangu akiwa ni kitinda mimba cha mama yk (bibi yangu). Upande wa ba mkubwa kaka yake mzee yeye anawatoto watatu wawili wa kiume mmja wakike..

sasa ipo hivi mnamo mwaka 2006 bamkubwa na mkewe warifariki kwenye ajali ya basi walikuwa wakiishi kilimanjaro watoto wao walikuwa wakubwa wakujitegemea..hivyo baada ya kufariki wazazi wao watoto waliuza mali moja baada ya nyingine za kwao hadi zikaisha licha ya kuonywa sana na kukalipiwa na mzee..

Sasa ikawa wamebaki mzee wangu na bibi mwaka 2009 mzee aliibomoa nyumba yote ya bibi maana ilikuwa ni zile nyumba za udongo zilizopo mjini alijenga nyumba mpya na kisasa kabisa pale kwa bibi (mama yk) kwa muda mfupi nakumbuka maana hapo nilikuwa nae mzee kipindi tunasimamia ujenzi. kwa kweli bibi na mzee wangu walifurahi sana, mwaka 2012 bibi nae akafariki hivyo mzee wangu akawa kabaki mwenyewe kwao.

Kwakuwa alijua tabia za watoto wa kaka yk za tamaa hakuwaruhusu wale watoto kukaa pale badala yk mzee aliweka wapangaji na kuacha viumba viwili kwa ajili ya kufikia endapo ndugu yyte ataenda dar basi maisha yameenda hivyo mwaka 2017 mzee nae alifariki sasa tumebaki watoto na mama..

Process za mirathi tulifanya na msimamizi wa mali hizo ni bi mkubwa pamoja na nyumba ya sinza ambapo kwenye mirathi imeandikishwa km mali ya mzee wangu, mwaka jana mtoto mmoja wa bamkubwa alihamia hapo sinza familia yk bila ya kuomba ruhusa kwa mama kwa kuwa ni ndugu hatukuwa na wasiwasi maana tuliambiwa alikuwa na hali ngumu kiuchumi..

Sasa ndugu hawa wanadai nyumba bora iuzwe maana wao hawana faida nayo ingawa wanaishi bure kodi za wapangaji hawapokei wao wakati eneo ni la bibi na baba yao anayo haki hapo.

Wakuu hili swala limetuvuruga hapa home.... kisheria tena za mirathi limekaaje hili kabla hatujafanya maamuzi magumu...
naombeni ushauri wenu maan mm ndio nategemewa nimpe mwongozo bi mkubwa nimestuck..
 

amu

JF-Expert Member
Aug 8, 2012
15,124
2,000
Kosa alilofanya ni hilo kujenga eneo la ukoo.

Hiyo ni mali ya yote watoto wa bamkubwa wanahusika.

Marehemu bibi yako alifurahi sababu alijua watoto wake wote na wajukuu wamepata nyumba nzuri alifurahi zaidi kwa kujuwa wale waliouza mali za marehemu baba yao wamepata la kusitirika.

Anyway kuna wataalam watakuja kusema mambo ya kukimbia mirathi n. K

Mimi kiroho safi tu tungeuza tukagawana mara mbili watoto wa bamkubwa kivyao na sisi kivyao.

Halafu sisi kama hatujajenga tunagawana kila mtu akaanze yake au tunaunganisha hela tunajenga nyingine ya familia.

Mwisho wa siku huyo mtoto wa bamkubwa anayeishi Sinza atatufata tu tumsitiri makazi(hapa ingetegemea ningeamkaje)
 

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
6,356
2,000
Unahangaikaje na kilaza huyo. Mwambie kama hawezi kuishi hapo aondoke akafanye maisha mahari kwengine. Ameomba kuja kuishi hapo. Hiyo nyumba sio mali yao hata kidogo, wameshatapanya mali ya baba yao imetosha.

Hiyo ni mali ya baba yako maana ndie aliijenga. Msaada mnaweza kuwapa ni kuwaacha waishi hapo tena kama vipi waambie tu walipe kodi. Maana hawana adabu. Na siku wakikuletea kelele.

Nenda kituo cha polisi wape mpunga kidogo waje wamchukue wamlambe makofi wakamuweke ndani mwezi m'moja akitoka atakuwa anakuamkia kabisa.
 

Drizzle

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
4,077
2,000
Sasa hivi wamelala, subiri waamke watakupa majibu ya kukuongoza kwenye jambo lako.
 

Buffet

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
599
1,000
Mzee wako alikuwa anataka kuwadhulumu watoto wa kaka yake, kumbuka hapo ni kwa bibi na babu yenu, kwanini yeye ajitwaliea na kuelekeza mke wake (mama yenu) awe anahusika na eneo hilo ili hali hakulitafuta na mke wake hilo eneo? Mali hajatafuta yeye,nn kilimtuma ajenge kwny eneo la ukoo bila kushirikisha warithi wengine?

Sasa wewe unadhani hao watoto wa baba yenu mkubwa ni kukaa bure kwny nyumba ya babu yao huku wakishuhudia faida zingine zinaishia kwny familia ya baba yao mdogo pekee, ujinga aliofanya Mzee wenu ashukru watoto wa kaka yake wana moyo wa kuvumilia, huo upuuzi alofanya saivi mgeshachinjana,bado hamjachelewa.

Nyie watoto tafuteni maridhiano na ndugu zenu kuepusha mengi,msimsikilize mama yenu maana hahusiki kwa vyovyote na hiyo mali (hakuchuma na mume wake wala siyo jasho la mume wake), acheni kuwadhulum ndugu zenu, mtakuja kuumizana na familia itasambaratika, baba yenu alikusudia kudhulumu.
 

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,484
2,000
Mkuu Pips Man , kwakuwa mirathi husika ni nyumba inakupasa kwanza kujua kuwa mmiliki wa kiwanja ambapo nyumba imejengwa ndiye, kisheria, mmiliki wa hiyo nyumba. Ingawa maelezo yako hayako wazi sana kuhusu nani hasa ni mmiliki wa kiwanja husika ambapo nyumba bishaniwa imejengwa, naamini kuwa kiwanja kilikuwa cha babu/bibi yako.

Hapo, mtiririko wa mirathi unaanza. Mosi, warithi wa babu ni bibi na watoto wake. Warithi wa bibi ni watoto wake aliowaacha wakiwa hai. Vivyohivyo hadi mwisho. Kama mtoto anafariki kabla ya baba au mama yake (kama ilivyokuwa kwa baba yako mkubwa), marehemu huyo husemwa 'ameikimbia' mirathi. Yaani, hajawahi kurithi kwa mama yake.

Hatahivyo, kwakuwa baba yako mkubwa ameacha watoto kiungwana ni kuwagawia sehemu ya mirathi hiyo hata kama baba yao hajawahi kurithi kwa mama yake (iwapo kama kiwanja ni cha bibi). Hapo damu huwa na nguvu katika kupata sehemu ya mirathi. Kama kiwanja tangu mwanzo kilikuwa ni cha babu, watoto wa baba yako mkubwa wana sehemu yao kwenye mirathi hiyo moja kwa moja.

Kitakachotofautisha mgawo ni mchango wa kila mhusika kwenye ujenzi wa nyumba hiyo. Mahakama au Serikali yoyote huzingatia hili la utofauti wa mchango unaosababisha utofauti wa mgawo. Hivyobasi, hao watoto wa baba yako mkubwa wanahusika moja kwa moja na mirathi hiyo kama kiwanja kilikuwa cha babu yako. Kama ni kiwanja cha bibi, wanahusika kama watu wa damu moja na nyinyi.
Aione: Mkuu sana Mwifwa
 

Sim Card

JF-Expert Member
Dec 30, 2019
530
1,000
Hakuna haja ya kumbeleza mtu hiyo ishu iko clear aliyeomba kukaa hapo ndiye analeta chokochoko zote either aamue kukaa hapo kwa masharti au aondoke. Halafu muwe mnaandika kisheria watu siku hizi ni wababe anaweza kuja kukaa hapo halafu later akasema ni kwake na hakuna la kumfanya.Mkimaliza mgogoro muweke wazi kisheria.Haiwezekana unakaribishwa mahali halafu unaanza visa.Fukuza mbali akatafute maisha huko ni mtu mzima huyo anawatega.
 

zipompa

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
6,048
2,000
Hao mabwana (watoto wa ba mdg ) wana husika na mirathi kwa maana ile nyumba haikuwa ya baba yako bali ya bibi yenu ila alijengewa na baba yako (mtoto alimjengea mama yake).

cha kufanya tafuteni hela baada ya hapo tangaza kuiuza muinunue nyie na familia yenu na muwape mgao familia ya ba mdg (wazo gumu)

ama waache wakae hapo bure huku mkiwapa mgao wa kodi maana wana haki nayo pia maana ni nyumba ya bibi yao (japo ilijengwa na ba mkubwa wao kama zawadi kwa bibi yao yaani mama yake).

NB.hao jamaa wana haki kwenye iyo nyumba na wana haki ya kupewa mgao wa kodi na kukaa hapo pia
 

Pips Man

JF-Expert Member
May 9, 2014
1,438
2,000
Mzee wako alikuwa anataka kuwadhulumu watoto wa kaka yake, kumbuka hapo ni kwa bibi na babu yenu, kwanini yeye ajitwaliea na kuelekeza mke wake (mama yenu) awe anahusika na eneo hilo ili hali hakulitafuta na mke wake hilo eneo? Mali hajatafuta yeye,nn kilimtuma ajenge kwny eneo la ukoo bila kushirikisha warithi wengine?...
Uzuri wake bibi alichukia tabia walizozionyesha wajukuu zake za kutapanya mali baada ya mwanae (baba mkubwa) kufariki hivyo bibi aliandikisha ile nyumba km ya mzee na asisumbuliwe na saini waliwekeana na mashaidi ni watendaji wa mtaa ingawa mmoja wa walioweka saini nae ni marehemu pia.
 
  • Thanks
Reactions: amu

Pips Man

JF-Expert Member
May 9, 2014
1,438
2,000
Mkuu Pips Man , kwakuwa mirathi husika ni nyumba inakupasa kwanza kujua kuwa mmiliki wa kiwanja ambapo nyumba imejengwa ndiye, kisheria, mmiliki wa hiyo nyumba. Ingawa maelezo yako hayako wazi sana kuhusu nani hasa ni mmiliki wa kiwanja husika ambapo nyumba bishaniwa imejengwa, naamini kuwa kiwanja kilikuwa cha babu/bibi yako...
Asante sana ndugu mselewa kwa ushauri wako unzuri ingawa uzuri wake bibi alichukia tabia walizozionyesha wajukuu zake za kutapanya mali baada ya mwanae (baba mkubwa) kufariki hivyo bibi aliandikisha ile nyumba km ya mzee na iliandikwa asisumbuliwe na saini waliwekeana...mashahidi ni watendaji wa mtaa wa kipindi hicho.
 

Cheef Baroka

JF-Expert Member
Mar 24, 2020
303
1,000
Mkuu Pips Man , kwakuwa mirathi husika ni nyumba inakupasa kwanza kujua kuwa mmiliki wa kiwanja ambapo nyumba imejengwa ndiye, kisheria, mmiliki wa hiyo nyumba. Ingawa maelezo yako hayako wazi sana kuhusu nani hasa ni mmiliki wa kiwanja husika ambapo nyumba bishaniwa imejengwa, naamini kuwa kiwanja kilikuwa cha babu/bibi yako...
Umepita vizuri sana kaka.. Na pia walichelewa sana kufungua mirathi Mahakamani ambayo ingewaainisha warithi wote na msimamizi wakatambulika kisheria
 

Cheef Baroka

JF-Expert Member
Mar 24, 2020
303
1,000
asante sana ndugu mselewa kwa ushauri wako unzuri ingawa uzuri wake bibi alichukia tabia walizozionyesha wajukuu zake za kutapanya mali baada ya mwanae (baba mkubwa) kufariki hivyo bibi aliandikisha ile nyumba km ya mzee na iliandikwa asisumbuliwe na saini waliwekeana...mashahidi ni watendaji wa mtaa wa kipindi hicho.
Wosia ambao unabagua warithi au unagawnya mali pa bila ulinganifu huwa hauzingatiwi kisheria.

Ila kwa picha inayoonekana hapo kwa mujibu wa maelezo yako hao ndugu zako wapo kishari, na kama mtu kanuwia shari we mkwepe. Ikiwezekana pigeni hesabu thamani ya nyumba hiyo utoe fungo lenu ili lile fungo lao uwalipe wawe hawamo na ubaki mmiliki halali kisheria.

Ila kama na hapo hawataki basi uzeni2 mana mtaanza kurogana, kushtakiana, na kufanyiana fitina ambayo itagharimu muda/gharama nyingi kuliko hata thamani halisi ya nyumba hiyo.
 

Pips Man

JF-Expert Member
May 9, 2014
1,438
2,000
Wosia ambao unabagua warithi au unagawnya mali pa bila ulinganifu huwa hauzingatiwi kisheria.

Ila kwa picha inayoonekana hapo kwa mujibu wa maelezo yako hao ndugu zako wapo kishari, na kama mtu kanuwia shari we mkwepe. Ikiwezekana pigeni hesabu thamani ya nyumba hiyo utoe fungo lenu ili lile fungo lao uwalipe wawe hawamo na ubaki mmiliki halali kisheria. Ila kama na hapo hawataki basi uzeni2 mana mtaanza kutokana,kushtakiana, na kufanyiana fitina ambayo itagharimu muda/gharama nyingi kuliko hata thamani halisi ya nyumba hiyo.
Asante kwa ushauri mkuu..
 

Cofta

Member
Aug 6, 2017
87
1,000
Pips Man
Kwa mtazamo wangu kabla ya nyumba kuunganishwa kwnye mirathi ya baba yenu palipaswa kufunguliwa shauri la miradhi ya bibi yenu ili ile nyumba ambayo ilikuwa ya bibi iweze kupatiwa msimamizi halali ambae ndio angetoa muongozo sahihi wa namna bora yakugawa miradhi kwa waridhi waliokuwa wamebakia.

Binafsi naona haikuwa sahihi kuunganisha nyumba ile ya bibi pamoja na mirathi ya baba yenu kwakuwa hapakuwa na mgawanyo wa miradhi ile ya bibi ambae alitangulia mbele ya haki na hiyo ndo changamoto ambayo inafanya watoto wa baba yako mkubwa kujichukulia maamuzi mbalimbali kadri ya hisia zao.
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
27,136
2,000
Mkuu, uzeni hiyo nyumba na kisha mgawane. Sijisikii kuandika mengi, lakini ushauri wangu kwako ndio huo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom