Msaada usafiri kutoka Morogoro kwenda Butiama

E-smart

Senior Member
Aug 31, 2022
179
337
Wakuu kama title inavyosema, nahitaji kusafiri kutoka Morogoro kwenda Butiama karibu na chuo cha Mwalimu Julius Nyerere University of Agriculture and Technology, kwa anayefahamu bus ninalotakiwa kupanda, pamoja na routes za kupitia kufika hapo naomba anisaidie pleasešŸ™.
 
Unakwenda kijiji cha Butiama kwa Nyerere yalipo makao makuu ya wilaya?

Kama ndio, uliza basi zuri linalokwenda Tarime utashuka Kyabakari, pale kuna tax na Bodaboda uamuzi ni wako utapelekwa Butiama.

Unapotokea Mwanza mabasi hayapiti Butiama hivyo ni lazima ushuke hapo Kyabakari ndio upande Bodaboda au tax nauli ya kawaida tu watakupeleka hapo Butiama.

Route ni Morogoro, Dodoma, Singida, Igunga, Nzega, Shinyanga, Mwanza to Musoma.
 
Sahihi.Hapo kwenye Kiabakari atasema anashuka Nyamisisye.
 
Panda bus la Dar -Tarime au Dar- Musoma ukifika njiapanda ya Musoma Tarime shuka . Au fika stand Musoma kapata coaster za kwenda Butiama
 
Nieleze kwanza hicho Chuo kipo sehemu gani?
Kipo Butiama kama alivyoeleza.Anaweza kufika hapo Makutano na kupata usafiri unaopita katikati kuiacha njia ya Mwanza na kuelekea Butiama moja kwa moja.Au akaendelea kutoka Makutano na kuelekea hadi Nyamisisye.Halafu atafute usafiri kwenda moja kwa moja Butiama kupitia Nyankanga.Hapo vipi?
 
Hii shida yote ya nini wakati akipanda basi la Tarime na kushuka Kyabakari anapanda Bodaboda tu kwenda Butiama, ni kwa nini ajisumbuwe na mzunguko usiokuwa na tija yoyote?
 
Kipo Butiama kama alivyoeleza.Anaweza kufika hapo Makutano na kupata usafiri unaopita katikati kuiacha njia ya Mwanza na kuelekea Butiama moja kwa moja.Au akaendelea kutoka Makutano na kuelekea hadi Nyamisisye.Halafu atafute usafiri kwenda moja kwa moja Butiama kupitia Nyankanga.Hapo vipi?
Unaweza kunielekeza straight natokea MOROGORO napanda bus la kwenda wapi nashukia wapi na naelekea wapi Ili kufika hapo butiama, just short and clear boss wangu fanya hivyo asee.
 
Zingatia mambo haya utafika salama.
1. Panda gari ya dar - Musoma.
2. Ili ufike mapema zaidi, epuka kupanda magari yanayopitia mwanza, yanachelewa zaidi. Panda Magari ya route ya Dar, morogoro (ulipo) dodoma, singida, igunga, nzega, shinyanga, maswa, bariadi, bunda, Musoma.

In this case, magari ya Kampuni ya Kapricon ndo yanapita route hii na yanafika mapema zaidi kule. Jaribu kuuliza magari ya Abood hapo moro yanapita route ipi.
3. Changamoto yako ni kuwa, utafika kuanzia saa 8: 30 usiku ( iwapo hutapitia mwanza) au zaidi ya hapo. So wewe utakubali kulala Musoma ili kukicha ndo uende huko butiama kwa kutokea musoma, maana usiku huo ukiteremkia njiani, hutapata usafiri wa kwenda butiama.

Kila la kheri.
 
Unakwenda kijiji cha Butiama kwa Nyerere yalipo makao makuu ya wilaya?

Kama ndio, uliza basi zuri linalokwenda Tarime utashuka Kyabakari, pale kuna tax na Bodaboda uamuzi ni wako utapelekwa Butiama.

Unapotokea Mwanza mabasi hayapiti Butiama hivyo ni lazima ushuke hapo Kyabakari ndio upande Bodaboda au tax nauli ya kawaida tu watakupeleka hapo Butiama.

Route ni Morogoro, Dodoma, Singida, Igunga, Nzega, Shinyanga, Mwanza to Musoma.
Umenichanganya boss, bus napanda la kwenda Tarine au la kwenda Mara ?. Umenielekeza as If napafahanu kindaki ndaki boss wangu, unaweza kunielekeza kwa kifupi tu natoka na bus la Morogoro napanda bus linaloenda mkoa Gani ? Kisha nashukia wapi na napanda gari la kuelekea wapi tena Ili nifike hapo butiama ? Short and clear my boss
 
Panda bus la Moro - Musoma au Moro - Tarime, shuka sehemu kituo kinaitwa Sabasaba......mwambie boda akupeleke Mwl Nyerere Agriculture University au iliyokua Oswald Mang'ombe High School
 
Hapo Morogorogo bus la Nyehunge unaliona.

Kiujumla panda Magari ya Musoma.
Kwa sababu unafika usiku kwanini usifike msoma stendi kabisa ulale kesho yake utafute gari za butiama.

Mara ni nyumbani, saa nane usiku sidhani ukishukia kiabakari utapata huduma hitajika vizuri. So kama basi linafika usiku nenda nalo hadi Musoma stend kabisa.
 
Mkuu si anafika usiku mkali huyo. Ni vyema tumsaidie pia na muda anaofika
 
Hapo Morogorogo bus la Nyehunge unaliona.

Kiujumla panda Magari ya Musoma.
Kwa sababu unafika usiku kwanini usifike msoma stendi kabisa ulale kesho yake utafute gari za butiama.

Mara ni nyumbani, saa nane usiku sidhani ukishukia kiabakari utapata huduma hitajika vizuri. So kama basi linafika usiku nenda nalo hadi Musoma stend kabisa.
Kesho yake uunge za Butiama
 
Yes, panda gari ya Moro ... Musoma, zinafika usiku sana na hali ya ugeni itakuwia ugumu kufika chuoni.

Ushauri
Nenda hadi Musoma mjini, pakikucha ulizia magari yanayoenda Buhemba(haya yanapita kwenye geti kabisa la Mwl Nyerere Un), au panda magari yanayoenda Butiama then shukia Butuguri then daka boda anakupeleka chuoni chap
 
Back
Top Bottom