Wenyeji wa Dar esalaam msaada wenu

Wegr

JF-Expert Member
Apr 27, 2022
224
579
Poleni na harakati za siku nzima,

Ndugu zangu kesho natarajia kusafiri kutoka mkoani kuja Dar, nitakuwa hapo kwa siku 14 kikazi.

Eneo la kazi litakuwa (JNIA) Julius Nyerere International Airport,

Vitu ninavyopenda kujua na kuelekezwa ni pamoja na,
Kutoka stand nitakapofikia kwenda hapo airport usafiri upo wa moja kwa moja au ni panda shuka(umbali)

Nikiwa maeneo jirani na airport kuna nyumba za kulala eneo jirani ama?

Sijawahi kufika kabisa napenda kujua mengine mengi

Asante
 
Umbali au ukaribu hutofautiana maoni ya watu, mi naweza sema mbali wewe ukaona karibu, ila usafiri unapatikana masaa 24 hivyo ni wewe tu utumie daladala, mwendokasi au uber.

Mi nakushauri tu usipande bodaboda na kama una mke mpige mashine vizuri leo ili asiingie majaribuni wakati wewe utakua umeshaingia majaribuni hapa dar pia usipande bodaboda ikiwa hakuna ulazima.
 
Nimekupata mkuu
 
Karibu sana Dar es Salaam mkuu huku usafiri ni wa uhakika 24/7 unaweza kupanda daladala, bajaji, bodaboda,au Uber ni wewe tu na maamuzi yako.
Lodge zipo za kutosha ila kuwa makini sana na huu mkoa kilakitu kinapatikana akili yako tu.
 
Karibu sana Dar, haina mchana wala usiku ni wewe unaamua unataka usiku uwe ni upi na mchana hali kadharika. Tunza afya yako, epuka kupanda boda boda kukiwa na ulazima basi request bolt boda, ni salama zaidi. Epuka wale wanaendesha wakiwa wame ning'iniza kanda2 pembeni, utaacha jina
 
Poleni na harakati za siku nzima,

Ndugu zangu kesho natarajia kusafiri kutoka mkoani kuja Dar, nitakuwa hapo kwa siku 14 kikazi.

Eneo la kazi litakuwa (JNIA) Julius Nyerere International Airport,

Vitu ninavyopenda kujua na kuelekezwa ni pamoja na,
Kutoka stand nitakapofikia kwenda hapo airport usafiri upo wa moja kwa moja au ni panda shuka(umbali)

Nikiwa maeneo jirani na airport kuna nyumba za kulala eneo jirani ama?

Sijawahi kufika kabisa napenda kujua mengine mengi

Asante
We ni mshamba kama baba yako kwa avatar
 
Karibu sana Dar, haina mchana wala usiku ni wewe unaamua unataka usiku uwe ni upi na mchana hali kadharika. Tunza afya yako, epuka kupanda boda boda kukiwa na ulazima basi request bolt boda, ni salama zaidi. Epuka wale wanaendesha wakiwa wame ning'iniza kanda2 pembeni, utaacha jina
Nawezaje kuRequest hiyo bolt boda mkuu, huwa wanapita mimi naweza kumuita tu kama boda wa huku kwetu ama unakua na app?
 
Ni app una download playstore na rahisi ku request huko hata bei utalipia halali kuliko wakikuona mgeni sehemu fupi wanakupiga bei kubwa
 
Mkuu ukisikia wadau hapa wanavyoupamba huo mji utadhani unaingia New York City kumbe....

Kwanza kabisa ukifika jiandae kupokelewa na joto likiambatana na fukuto la hewa nzito na harufu mbaya iliyochanganyika na uvundo kila mahali utapopita. Mitaa ni michafu kila mahali ni vibanda, vigenge, vidukaduka, vimiavuli, nk

Pili utakutana na rundo la watu wamesongamana kila mahali na wenye sura chachu za kukata tamaa wasio na nuru yoyote wala matumaini ya maisha. Wengi wao ni mishen town hawana kazi wala hawaijui kesho yao. Wana hasira balaa kila mda ni kutukana matusi ya nguoni na maneno mengi kama cherehani. Kila mahali ni vurugu na kelele za magari, bodaboda, bajaji, nk

Tatu utapokelewa na foleni na hapo wenyeji wanakuambia ndio imepungua kwa sasa afadhali.

Cha kukushauri jitahidi upate hoteli nzuri ya gharama iwe full AC kinyume na hapo hata kulala hutalala na mpaka zije ziishe hizo siku
14 utakua huna hamu kabisa na hilo jiji.

Nikutakie kila la heri.
 
Pamoja mkuu
 
Dar ni ya kawaida mno ila jambo kuu la kuzingatia ni matapeli.

Wengi ya wakazi wa Dar kazi yao kubwa ni kubangaiza mjini hivyo kila mtu na kila kitu kwao ni fursa. Usipende sana kuomba kuuliza kuuliza kila unaemuona maana ukizubaa wanaweza kukuliza hata boxer uliyovaa.

Zaidi ya hapo wewe ni mtu mzima mengine utayapambanua kadri ya unavyoyaona na kukabiliana nayo.
 
Back
Top Bottom