Msaada tunaomba Mhe. Paul Makonda atusaidie, Kampuni ya Jog imechukua fedha za wawekezaji

lizeli

Member
Jan 23, 2016
28
13
Ndugu zangu,

Naamini hapa jamvini watu wa aina mbalimbali na nyeti wanasoma jumbe hizi.

Kampuni ya Jog Agri-Consult & Solutiions (T) Ltd chini ya wakurugenzi wake Grace Mzoo (Mkurugenzi Mtendaji) pamoja na Jackson Bwire pamoja na Mhasibu wao Cecilia Bukukura imechukua pesa za wawekezaji wa Papai tangu mwaka 2017-2018.

Kampuni ilijinasibu sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwenye makanisa, kwenye vyombo vya habari (Televisheni za Tz pamoja na Radio - mara ya mwisho Jackson Bwire alisikika Clouds akinadi kampuni). Jog chini ya Wakurugenzi wake imejinasibu kuwa inapokea pesa (Tzs million 9 kwa ekari moja) kutoka kwa mkulima/mwekezaji yoyote yule kwenye eneo la Papai halafu itafanya yafuatayo:

- Kukodisha ardhi
- Kuweka miundo mbinu yote (ikijumuisha drips pamoja na kuchimba visima vya kumwagilia papai)
- Kununua Pembejeo (mbolea za organic na dawa zote zinazohitajika
- Usimamizi wa kitaalam (ukijumuisha kupima udongo katika maabara Nairobi, kuweka vibarua nk)
- Kusaidia wawekezaji/wakulima kupata bima ya mazao
- Tayari wana mkataba na mnunuzi kutoka nchi za nje na kwa hiyo papai zikishakomaa watanunua kwa Tzs1000 kwa papai kutoka shambani na hivyo kumlipa kila mwekezaji
- Na mengineyo mengi

Watu na vikundi mbalimbali wakiwemo wajane, wastaafu, wajasiriamali, vikundi vya ujasiriamali/uwekezaji/fellowship walijiunga na kulipa fedha (Jumla ni Zaidi ya Tzs milioni 200) kwa kampuni ya Jog chini ya wakurugenzi waliotajwa hapo juu lakini hadi leo hii ninavyoandika ni zaidi ya miaka miwili (2) hakuna aliyelipwa na ukipiga simu zao hawapokei, ukienda ofisi zao pale Mwalimu House zimefungwa.

Juhudi za kufuatilia zimefanyika kama ifuatavyo;-
- Kuwapigia simu na kutuma sms (hakuna anayepokea simu wala kujibu ujumbe)
- kwenda ofisini kwao Mwalimu House - tukakuta ofisi imefungwa na wameweka namba za simu ambazo ndio hizo hawapokei
- Kwenda kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga - Alikiri kupata malalamiko kutoka kwa watu wengine pia kuhusu Jog lakini akashauri tukaripoti DSM ambako Kampuni imesajiliwa
na Wakurugenzi wanaishi
- Kuripoti Polisi Mkoa wa Ilala/Kariakoo
- Kuutafuta uongozi wa Wilaya ya Ilala labda watatusaidia (hatujafanikiwa)

Tunaomba Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam utusaidie kwani watu wengi walichukua mikopo Benki ili kuwekeza lakini wameshindwa

Asanteni
 
Makonda ndye Police au Mahakama? Wakati mnawekeza mlimshirikisha makonda?

Nchi inabidi iendeshwe kisheria bana sio kila kitu ku-pull strings.

Iyo ni very simple. Police watawatafta na kuwafungulia kesi, mahakama itafanya kazi yake.
 
Asante
 
Mkiwapata wakodisheni wafi.raji kabla ya kuanza mazungumzo. Pia kilimo sio story za abunuasi, jifunzeni siku nyingine. Milioni 9 ungenunua shamba lenye miche ya miti ya mbao hapa ludewa baada ya miaka 10 uko mbali.

Asante
 
Hayo ni matunda ya KILIMO CHA WHATSAP

Tulienda mpaka shambani ndugu yangu. Shamba tulionyeshwa na matrekta yalikuwa kazini pamoja na vibarua, na viongozi wa kijiji pale Kimazichana walikuwepo kutuonyesha kuwa mwekezaji wanamfahamu. Tulipenda tulime kwenye mashamba yetu lakini Swala linakuja kwamba wenyewe walisema hawaruhusu ulime shambani kwako kwa ajili ya kudhibiti ubora.

Lakini nashukuru pia kwa jibu lako
 
Hata hivyo mna moyo sana. Usawa huu wa magu mnatoa 9m kirahisi rahisi kwa jina la uwekezaji? Mlishafika kufhakiki mashamba kabla hamjawekeza? Naiona QNET nyingine hapa, kupitia ninyi
 
Hawa watu ni watu hatari kwa tulivyosikia. Nimesikia pia wana kesi Arusha ya Green Beans lakini pia kuna kundi lingine la Papai Phase1 wanahangaika kutafuta kurudishiwa pesa yao. Wanatumia wanasheria nguli na ukizingatia watu wengi pesa imeenda hofu kuwa hata Mwanasheria wa hawa walalamikaji anaweza aka-collude na Mwanasheria wa Kampuni ili kuchelewesha na pengine kutopata haki kabisa.

Wawekezaji wanatoka mikoa mbalimbali ya Tanzania; Iringa, Dodoma, Geita, Mwanza, Dar, Pwani nk.

Naamini hapa hata kama sio leo ipo siku wahusika watasikia/wataona na watatusaidia.

Asante.
 
Tulienda mpaka shambani ndugu yangu. Shamba tulionyeshwa na matrekta yalikuwa kazini pamoja na vibarua, na viongozi wa kijiji pale Kimazichana walikuwepo kutuonyesha kuwa mwekezaji wanamfahamu. Tulipenda tulime kwenye mashamba yetu lakini Swala linakuja kwamba wenyewe walisema hawaruhusu ulime shambani kwako kwa ajili ya kudhibiti ubora.

Lakini nashukuru pia kwa jibu lako
Poleni mkuu.
Ilitakiwa muanze kushituka kuanzia hiyo hatua niliyoweka bold. Utapeli ulianzia hapo 👆👆👆. Ubora unaweza kudhibitiwa pahala popote pale regardless ni shamba lao ama la mwenzao, provided wataalamu wa kazi hiyo ya kudhibiti ubora wapo muda wote.
 
Tulienda mpaka shambani ndugu yangu. Shamba tulionyeshwa na matrekta yalikuwa kazini pamoja na vibarua, na viongozi wa kijiji pale Kimazichana walikuwepo kutuonyesha kuwa mwekezaji wanamfahamu. Tulipenda tulime kwenye mashamba yetu lakini Swala linakuja kwamba wenyewe walisema hawaruhusu ulime shambani kwako kwa ajili ya kudhibiti ubora.

Lakini nashukuru pia kwa jibu lako
Hakuna mtu wa kwenda kukulimia then akutafutie soko halafu akuite haya boss njoo uchukue pesa yako wkt huo wewe umeweka kende home tu unaangalia zako movie/tamthilia za kutafsiriwa kwa kiswahili.

Pesa sio rahisi hivyo.
 
Ingekuwa yule mkuu wa mkoa wa Dodoma ingekuwa faster tu,namuelewa sana yule,
 
Ukiitwa firsan ujue wewe ndio fursa MTU kirahis tu unatoa m9 kwa kauli za motivational speaker

Ungefuatilia kwanza kujua hyo kampun imewah Fanya mrad gan mkubwa au was kat na ikafanikiwa

Ndio yaleyale watu wamefugishwa sungura na mwishowe wakaachwa

Mwingne humu alifugishwa majoka huko bagamoyo sasa yanataka kumla yeye

WATANZANIA TUWE TUNAFUATILIA MAMBO KUZIJUA KAMPUNI ZA HOVYO KAMA HAO JOG
 
Makonda ndye Police au Mahakama? Wakati mnawekeza mlimshirikisha makonda?

Nchi inabidi iendeshwe kisheria bana sio kila kitu ku-pull strings.

Iyo ni very simple. Police watawatafta na kuwafungulia kesi, mahakama itafanya kazi yake.
Mleta thread nae ni msomi unaambiwa...
 
Back
Top Bottom