Msaada: Tumepoteza kazi baada ya kudai haki zetu

Kwahiyo hata zile order za serikali hazina nguvu yoyote??
Mhii yaani wewe aliyekuajiri ni serikali au mtu binafsi. Mkataba ukiisha huwexi mlazimisha tajiri akuajiri tena mapenzi yake . sijui wewe unataka sheria ipi
 
Mimi sioni kosa la mwajiri. Mkataba umeisha ameamua kutoongeza. Hana kosa .haki zenu nyingine mtapata kama kawaida nadhani ila kazi ndo mwisho na hawezi lazimishwa kuwaajiri.

Heri ya mwaka mpya wadau,!! Mimi na mwenzangu Tumepoteza kazi baada ya kudai haki na stahiki zetu zilizokuwa zinabinywa na mwajiri, baada ya kufatilia sheria zinasemaje katika misingi ya kisheria na mwajiri wetu kuamriwa kurekebisha.


Mwajiri hakufanya hivyo Bali akasubiri mwisho wa mkataba akatupa barua za kumalizika kwa mkataba.

Je, wajuzi wa sheria ni namna gani sheria zinatulinda kwa namna yoyote kupoteza kwetu kazi kwa kudai haki zetu? Naombeni msaada
 
Haki atapata kaka, Mimi nipo kampuni binafsi kuna kesi kama hizo nyingi tuu, watu wanapata haki....
Ila tuu kama amekaa mda mrefu kazini na hakuwahi kupata likizo hapa anayo point, ama anafanya kazi masaa mengi kuzidi yale yaliyoainishwa katika mkataba hapo point nyingine,
Yeye anaenda tuu pale wizara ya kazi na ajira si lazima aajiri wakili maana atasimamiwa na wakili wa serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
Anataka haki zake ?

Au anataka arudishwe kazini?

Seems like anataka arudishwe kazini.

Je itawezekana?
 
Hata Shule za sekondari tu mkigoma kwa mambo ya Msingi na yenye kueleweka lazima mtafukuzwa wale vinara ama myahamishwa shule. Uongo?
 
Kumbe Mlikuwa mnachokoza mzinga wa nyuki huku mko matumbo wazi! Sasa si mkataba umeisha kwa huyo asiyetenda haki nilitegemea muende kwa wanaotenda haki sasa au kuna stahiki mnazomdai hapo sawa lakin kama issue ni kutokupewa mkataba mwingine ni kupoteza muda sababu sioni hoja yoyote convincing.
 
Muajiri alivizia mkataba umeisha ndio akawala vichwa.
Huyo jamaa ni kichwa msicheze naye, angekuwa kilaza angewafukuza katikati ya mikataba yenu ila alivumilia vitimbi vyenu mwisho wa mkataba akawatimua.
Kikubwa awalipe stahiki zenu mjiondokee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujafukuzwa, mkataba(makubaliano) mliyoingia yamekwisha muda wake. Kama kuna vitu vya kudai ni haki zako, kama kuna vitu mlikubaliana kufanyika kabla ya kuanza kazi, wakati wa ajira au baada, nenda kavidai lakini huwezi kudai ajira tena, hilo mpaka yeye akubali.

Yaani umepeana talaka na mkeo halafu unataka umfanye mke tena wakati yeye hataki! Usipoteze muda, kuna watu watakulia pesa zako humu. Mkataba umeisha, mwenzako hakutaki tena. Hayo mambo ya harakati, wengine wamerudi etc, ni secondary tu, primary ni mkataba kwisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kudai haki yako hakumzuii mwajiri kutokukuongezea mkataba, unapodai haki yako unatakiwa uwe makini sana hasa kama hauna mkataba wa kudumu maana kama una mkataba wa mda mfupi hayo ndio majanga yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni vigumu kujastifai mbele ya vyombo vya sheria kwamba umenyimwa mkataba mpya kwa sababu kama hiyo.
Hata hivyo mwajiri kama hakutaki kwa sababu yoyote ile anakuondoa tu ofisini kwake.
Nenda kwa wanasheria pale CMA watakupa ushauri nini cha kufanya.
 
Mwajiri atakulipa stahiki zako halali kama unamdai, ila mwajiri ndiye mwenye mamlaka ya kukubali kukuongezea mkataba au kutoendelea haina mjadala, usingeenda mahakamani ungekuwa tu unamuomba ili kulinda mkataba wako
 
Back
Top Bottom