Msaada: Tumepoteza kazi baada ya kudai haki zetu

Kama chanzo ni nyie kufuatilia sheria mkafukuzwa, basi fuatilien tena sheria hukohuko kwa mwanzo mtarudishwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tofautisha kufukuzwa kazi na mkataba kuisha...hawa mkataba umeisha sasa huwezi kumlazimisha mwajiri akuongezee mkataba..vilevile mwajiri hawezi kukulazimisha uongeze mkataba
 
Mkuu, pamoja na yote mwajiri alipewa barua ya kutopunguza au kufukuza wafanyakazi kutokana kitendo Cha wafanyakazi kudai haki zetu
Maelezo yako hajajitosherezi. Mkataba wako umefika mwisho, kama umepewa haki zako za kimkataba uwasalimie uendako. Kama umenyimwa seek a legal advice

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani tatizo ni stahiki?Kama mkataba umeisha, mwajiri ana wajibu wa kulipa stahiki zote kulingana na mkataba.

Lakini kwa kua mkataba umeisha, mwajiri halazimishwi kuendelea na wewe na huwezi prove kwamba hajakuongezea mkataba kwa sababu umepigania haki yako.

Nashauri uachane nae tafuta kazi sehemu nyingine
 
Pole kwa kila kitu nitapenda kuchangia kitaalamu kidogo na kwa kutumia sheria na kanuni zifuatazo: Sheria ya ajira na mahusiano kazini mwaka 2004, Kanuni za ajira na mahusiano kazini mwaka 2007, Minimum wage order 2013 na Sheria ya mikataba sura 345 kama ifuatavyo ila nitaanza kwa kuhoji vitu muhimu na kumalizia mpaka jinsi mlivyoanza kukosa kazi.

Ningependa kujua vitu mlivyoenda kuvidai vilikuwa ni vipi je vilikuwepo kwenye mkataba ila vilikuwa havitekelezwi ukinijibu hapa nitajua cha kuendelea pili mlipoenda mara ya kwanza ilikuwa ni wapi labour office za mkoa husika au CMA Je mlipewa hati ya usuluhisho wa hayo malalamiko na kuwekwa saini ya pande zote mbili yani muajiri na muajiriwa

Sasa tuje kwenye tatizo la 2 sasa ndilo linaloleta ukakasi kidogo kwa kutumia Kanuni za ajira na mahusiano kazini mwaka 2007 kifungu cha 4(2) kinasema hivi mkataba wa muda maalumu utakoma wenyewe endapo muda wake umefika mwisho sasa nenda kwenye mkataba wako kuna kipengele kimeandikwa termination of the contract au kuvunjika kwa mkataba kwa kiswahili

Shida hapo inatokea endapo mfanyakazi alikuwa na matumaini ya kupewa mkataba mpya hasa ule wa muda maalumu hii ipo katika kifungu cha 3 kanuni ya ajira na mahusiano kazini mwaka 2007 yani kitaalamu wanasema intention of renew of the contract with the same term and conditions

Sasa basi nini kilitakiwa kifanyike mfano mkataba ulikuwa unaisha december 2020 ilitakiwa angalau november mwanzoni itoke kitu kinaitwa NON RENEW OF THE CONTRACT NOTICE ili sasa kuondoa matumaini ya mfanyakazi kwamba ikifika december mkataba wako unapoisha hutopewa mkataba mpya hii inamuondolea matumaini ila usipofanya hivyo sheria na kanuni inasemaje

Mfano imefika december labda tarehe 10 ndo muajiri anasema bwana mkataba wako ukifika mwisho sitokupa mkataba mpya hapo anakuwa yupo nje ya muda na sheria inasema kama taarifa ya NON RENEW OF THE CONTRACT NOTICE ikitoka nje ya muda maana yake ule mkataba umekuwa renewed yani unatambulika kama umeanza upya.

nimetumia sheria moja kwakuwa maelezo yako nayo hayapo moja kwa moja sana ungeeleza kila kitu bila kuacha inamaana kila utakachoeleza kinatatulika kwa kanuni na sheria na tutafahamu hapa wote jukwaani kwamba una haki au hauna haki
 
Back
Top Bottom