Msaada; Tshs 85Mil, inajenga Ghorofa??

Ndugu yangu nina mashaka makubwa kuhusu huo ujenzi unaoufikiria. Nyumba ya kwaida vyumba vitatu vya kulala, dining room, sitting room, car park, inateketeza mil 50. Fikiri upya kuhusu hilo wazo. Nakushauri pata ramani na wasiliana na contractors upate picha halisi.
 
Kaka boss wangu ni member hapa Jf na anaijua username yangu,
Akijua nina 85Mil ya kujenga ni kesi.
Najenga Kibada!!

Block Gani? Plot No. Ngapi? Njoo Full Shangwe Jumamosi Unionyeshe kiwanja chako tuweze anza mchakato wa ujenzi.isije ikawa ni promo tu ya kutafutia wachumba kule love connect,mie nina kiwanja hapo kibada cha kupima,chako kipo maeneo gani ghorofa zipo nyingi pale!!
 
Baada ya post hii, mtamuona kule MMU akitafuta mchumba!

Chambo chako nimekikubali, angalia kisije kikavuwa mapapa upanga tu.

Haaaaaaaaa hata mie nina wasiwasi isije ikawa anafanya promotion ya kula watoto wa kike wa facebook walioingia JF.
 
Ramani ningeweza ku-attach hapa but sina soft copy yake.
But Nyumba ni vyumba vinne vya kulala, viwili juu Na viwili chini.
Library juu, wakati jiko Na stoo chini.
Self container ni kimoja cha juu tu.

Mkuu nyumba yako karibu ifanane na ya kwangu kabisa tofauti tu ni kuwa ya kwangu ina study room juu, vyumba vitatu juu (kimoja kikiwa ni master) na kimoja chini ambacho ni self contained pia. Ndugu yangu ujenzi unaumiza kichwa na si mchezo. Niliambiwa kuwa makadirio ya kujenga nyumba ni laki tano kwa kila mita ya mraba mpaka finishing tena kwa kutumia mkandarasi. Nyumba yangu ni around 380 sm. Nikapiga mahesabu nikapata around Tshs. 190 mil. Kwa vile nilishapanga kutumia mafundi wa mitaani na si wakandarasi nikajua nitejenga nyumba hiyo kwa gharama chini ya hapo. Lol! Mpaka sasa nikiwa nimemaliza kupiga paa, plasta, grills za milango na madirisha pamoja na fremu za milango zaidi ya Tshs. 160 mil. zimetembea na hapo nimetumia mafundi waaminifu kwelikweli wasio wezi na mahesabu nilikagua vizuri. Pamoja na kwamba nimeezeka kwa Decra Tiles ambazo ni ghali sana na mbao zilitumika nyingi bado hiyo Tshs 85 mil. kwa nyumba yako hazitoshi kabisa mkuu asikudanganye mtu.
 
Mkuu nyumba yako karibu ifanane na ya kwangu kabisa tofauti tu ni kuwa ya kwangu ina study room juu, vyumba vitatu juu (kimoja kikiwa ni master) na kimoja chini ambacho ni self contained pia. Ndugu yangu ujenzi unaumiza kichwa na si mchezo. Niliambiwa kuwa makadirio ya kujenga nyumba ni laki tano kwa kila mita ya mraba mpaka finishing tena kwa kutumia mkandarasi. Nyumba yangu ni around 380 sm. Nikapiga mahesabu nikapata around Tshs. 190 mil. Kwa vile nilishapanga kutumia mafundi wa mitaani na si wakandarasi nikajua nitejenga nyumba hiyo kwa gharama chini ya hapo. Lol! Mpaka sasa nikiwa nimemaliza kupiga paa maka plata zaidi ya Tshs. 160 zimetembea na hapo nimetumia mafundi waaminifu kwelikweli wasio wezi na mahesabu nilikagua vizuri. Pamoja na kwamba nimeezeka kwa Decra Tiles ambazo ni ghali sana na mbao zilitumika nyingi bado hiyo Tshs mil 85 kwa nyumba yako hazitoshi kabisa mkuu asikunganye mtu.

hao mafundi wako waaminifu umewatoa wapi?
unaweza saidia contacts?
 
Ebwana mbona unanitisha Mkuu! nilikuwa nina mpango wa kujenga ghorofa kama yako, vyumba vitatu, 2 juu pamona na master na studying room, 1 chini pamoja na kitchen, dining, sitting room na garage. Kwa hayo maesabu ya 160 mio, nimeishiwa nguvu kabisa. Endeleeni na michango wakuu.
 
Wadau,
Nimebahatika kupata Tshs 85mil Kama urithi baada ya kuuza Nyumba yetu iliyoko katikati ya jiji,
Ndoto yangu ni kujenga Nyumba ya Ghorofa kupitia hela hii, Na Kiwanja kilichopimwa tayari ninacho,
Nauliza tu kwa mgao huu naweza kupata Nyumba ya Ghorofa 1 kwa mahesabu ya Fundi + Materials??

Anza wewe acha kuuliza hutafika mbali, zikitosha sawa, zikipelea utaongeza kwani hupati tena pesa? acha woga mkuu
 
Mkuu nyumba yako karibu ifanane na ya kwangu kabisa tofauti tu ni kuwa ya kwangu ina study room juu, vyumba vitatu juu (kimoja kikiwa ni master) na kimoja chini ambacho ni self contained pia. Ndugu yangu ujenzi unaumiza kichwa na si mchezo. Niliambiwa kuwa makadirio ya kujenga nyumba ni laki tano kwa kila mita ya mraba mpaka finishing tena kwa kutumia mkandarasi. Nyumba yangu ni around 380 sm. Nikapiga mahesabu nikapata around Tshs. 190 mil. Kwa vile nilishapanga kutumia mafundi wa mitaani na si wakandarasi nikajua nitejenga nyumba hiyo kwa gharama chini ya hapo. Lol! Mpaka sasa nikiwa nimemaliza kupiga paa, plasta, grills za milango na madirisha pamoja na fremu za milango zaidi ya Tshs. 160 mil. zimetembea na hapo nimetumia mafundi waaminifu kwelikweli wasio wezi na mahesabu nilikagua vizuri. Pamoja na kwamba nimeezeka kwa Decra Tiles ambazo ni ghali sana na mbao zilitumika nyingi bado hiyo Tshs 85 mil. kwa nyumba yako hazitoshi kabisa mkuu asikudanganye mtu.

Mkuu nimetafuta consultantions kutoka kwa wakandarasi, hiyo nyumba yako unayojenga (380 Square meter) ni kubwa mno kibongobongo na kama ukifanya masiahala utamaliza chenji zote. Kale kadream house kangu ni ka 250 Square meter tu.
 
Ebwana mbona unanitisha Mkuu! nilikuwa nina mpango wa kujenga ghorofa kama yako, vyumba vitatu, 2 juu pamona na master na studying room, 1 chini pamoja na kitchen, dining, sitting room na garage. Kwa hayo maesabu ya 160 mio, nimeishiwa nguvu kabisa. Endeleeni na michango wakuu.

Mkuu kuna vitu nimeongeza kwenye post yangu ya kwanza nilivisahau na bado nimesahau vingine navyo ni:- Nimeshafanya wiring, nimeshaweka ceiling board (gypsum) na nimefanya plumbing pia nimelipia milango (mninga ambayo iko kwenye mahesabu). Kwahiyo vikubwa vilivyobaki ni kuweka aluminium windows, kuweka floor tiles, Kupaka rangi, kuweka vyoo na masinki na kuweka furnitures za jikoni. Kwa mahesabu ya haraka natakiwa nipate angalau kama milioni 40 hivi kazi iishe kabisa. Kwa ujumla mil. 200 zinaisha.
Mkuu usiogope sana kwani gharama itapungua kama utaezeka kwa mabati na ukatumia kokoto za kawaida ila ngumu.
 
Mkuu nimetafuta consultantions kutoka kwa wakandarasi, hiyo nyumba yako unayojenga (380 Square meter) ni kubwa mno kibongobongo na kama ukifanya masiahala utamaliza chenji zote. Kale kadream house kangu ni ka 250 Square meter tu.

Mkuu kama ulikuwepo vile. Chenji imeisha kabisaaaaa na sasa najikusanya. Nikiona vipi itanibidi nichukue hata mkopo benki nimalizie. Mkuu na hapo niliipunguza maana mchoraji alinichorea eti ananiwekea family lounge juu nikamwambia toa. Pia vyumba vyote alivifanya self contained nikamwambia hapana. Kwahiyo chini kuna chumba kimoja (self contained), lounge, dining, jiko, stoo, choo cha public na laundry. Juu kuna vyumba 3 (kimoja ni master), choo cha public na study room.
 
Ramani ningeweza ku-attach hapa but sina soft copy yake.
But Nyumba ni vyumba vinne vya kulala, viwili juu Na viwili chini.
Library juu, wakati jiko Na stoo chini.
Self container ni kimoja cha juu tu.
Mkuu hii ni nyumba kubwa sana kuweza kuijenga kwa tzs 85m. Chumba cha kulala cha kawaida ni kama 12 sq na kama ni self container kitakuwa na angalau 16 sq m. Hivyo vyumba vinne vya kulala tu vitachukua karibu ukubwa wa 52 sq m. Choo na bafu za kushare juu na chini kwa pamoja vitachukua kama 9 sq m. Sebule ya kawaida itakuwa na ukubwa wa 20 sq m. Dining ya kawaida ukubwa wa 10 sq m. Jiko ukubwa wa 12 sq m na stoo ukubwa wa 9 sq m. Library nayo itachukuwa karibu 12 sq m. Kwa hiyo kwa jumla ni ukubwa wa 124 sq m. Corridors na vibaraza vingine vinaweza kuwa karibu 20% ya hii 124 sq m (i.e. about 24 sq m) na hivyo nyumba nzima kufikia karibu 150sq m. Sq m moja kuijenga mpaka kumaliza kwa kiwango cha chini kabisa sio chini ya laki sita! Ukitaka kiwango cha 'kawaida' sq m moja haiwezi kupungua laki nane. Tena hapa umebana haswa na kusimamia kwa sehemu kubwa wafanya mwenyewe.

Kama una source nyingine ya funds si vibaya ukaanza na kiasi ulicho nacho kwani sio haba!
 
Mkuu nimetafuta consultantions kutoka kwa wakandarasi, hiyo nyumba yako unayojenga (380 Square meter) ni kubwa mno kibongobongo na kama ukifanya masiahala utamaliza chenji zote. Kale kadream house kangu ni ka 250 Square meter tu.

Mkuu kwa 250 sm ukiwa na Tshs. 150 mil. unamaliza vizuri kabisa. Omba tu nondo na simenti zisiendelee kupanda bei kwa kasi.
 
Mkuu nimepanga kujenga kwa awamu, nitajenga kwa awamu 5 na kila awamu nataka nitumie 30mio, yaani nitaanza na msingi wa gorofa pamoja na kupandisha kuta za ground floor 30 mio, awamu ya 2 nitamalizia kuta za ground floor na kumalizia zege la kuanza first floor na kupandisha kuta za first floor 30 mio. Awamu ya 3 nitaendelea na kumalizia kuta za first floor kisha nitaanza kuweka kazege sehemu dogo ya paa la first floor 30 mio. Awamu ya 4 nitaezeka vigae kwa sehemu ya paa la first floor na kufanya wiring, plumbing 30 mio. Mwisho nitaweka fremu za madirisha, milango, kupiga plasta, rangi, gymsam na kuweka PVC. kale ka 150 mio katakuwa kamekwishilia mbali.
 
Sawa mkuu. Ila awamu hiyo ya kwanza ni aghali zaidi ya hizo zinazofuata kwa maana utahitaji nondo za kutosha kusuka msingi na nguzo za kubeba hiyo first floor. Pia utahitaji simenti nyingi sana kumwaga jamvi na kujenga nguzo na kununua matofali ya kujengea msingi na kuinua hizo kuta za ground floor. Pia awamu zisiwe na interval kubwa sana maana bei za material zinabadlika kwa kasi mno. Huwezi kuamini nilianza na bei ya Tshs. 13500 na nikamaliza na bei ya Tshs 15,000 kwa mfuko wa kilo 50 wa simenti na ni ndani ya miezi kama 6 tu. Nondo nazo zilibadilikia bei mara kwa mara na zikavuruga makadirio kabisa hasa kipindi kile shilingi ilipokuwa inaporomoka kwa kasi hadi kufikia Tshs 1811 kwa USD 1.
Otherwise I wish you all the best mkuu.
 
Block Gani? Plot No. Ngapi? Njoo Full Shangwe Jumamosi Unionyeshe kiwanja chako tuweze anza mchakato wa ujenzi.isije ikawa ni promo tu ya kutafutia wachumba kule love connect,mie nina kiwanja hapo kibada cha kupima,chako kipo maeneo gani ghorofa zipo nyingi pale!!
Kipo block 10 mtu wangu,
Jana nlienda kule vitu nlivyokuta ni balaa.
Hata ikabidi nifikirie upya ramani nliyo nayo.
Watu wamedondosha vitu vya kufa mtu
 
Mkuu hii ni nyumba kubwa sana kuweza kuijenga kwa tzs 85m. Chumba cha kulala cha kawaida ni kama 12 sq na kama ni self container kitakuwa na angalau 16 sq m. Hivyo vyumba vinne vya kulala tu vitachukua karibu ukubwa wa 52 sq m. Choo na bafu za kushare juu na chini kwa pamoja vitachukua kama 9 sq m. Sebule ya kawaida itakuwa na ukubwa wa 20 sq m. Dining ya kawaida ukubwa wa 10 sq m. Jiko ukubwa wa 12 sq m na stoo ukubwa wa 9 sq m. Library nayo itachukuwa karibu 12 sq m. Kwa hiyo kwa jumla ni ukubwa wa 124 sq m. Corridors na vibaraza vingine vinaweza kuwa karibu 20% ya hii 124 sq m (i.e. about 24 sq m) na hivyo nyumba nzima kufikia karibu 150sq m. Sq m moja kuijenga mpaka kumaliza kwa kiwango cha chini kabisa sio chini ya laki sita! Ukitaka kiwango cha 'kawaida' sq m moja haiwezi kupungua laki nane. Tena hapa umebana haswa na kusimamia kwa sehemu kubwa wafanya mwenyewe.

Kama una source nyingine ya funds si vibaya ukaanza na kiasi ulicho nacho kwani sio haba!

Kaka nimekupata sawia,
So kwa mahesabu yako Nyumba hiyo inaweza kula minimum Tshs600,000 x 150Sqm = Tshs 90Mil.

Mahesabu haya yanahusisha bati, plasta, plumbing, wiring, etc????
 
Yes, lakini kama nilivyosema hiyo ni ya ubora wa chini. Na pia huo ukubwa unaweza kuwa tofauti kutegemea na ramani yako ilivyo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom