Fanya hiviii....nenda kwenye maduka ya pembejeo uliza dawa inaitwa dudukili 10WP ambayo huwa inakuwa kwenye kipaketi cha 62.5g pamoja na doom ya maji ambayo inakuwa kwenye kichupa kidogo, tafuta bomba la kupiliza dawa, tia dudukili yote katika maji ya lita 10 na doom kwa kipimo utakachoandikiwa .. nadhani ni 20mls, koroga tia kwenye bomba puliza ndani darini, kwenye milango, madirisha na sehemu zilizojificha, kisha nje , kwenye mashimo ya vyoo, majani nk, ukiwaona mbu au mende ndani ya nyumba yako nitafute unitie viboko!! Haina harufu naa gharama yake hafiki elfu 12 kwa zote isipokuwa bomba ambalo unaweza kuazima.....hili tatizo lilinifanya nishindwe kuangalia tv kwangu ila siku hizi huwa nalala sebuleni nikiangalia tv...mimi nimezipata katika duka la hill - boko - dsm, kwa walio karibu na maeneo hayo
.....kazi kwenyu
Mie na mbu na nzi mbali mbali hupambana nao kwa kutumia Expel na miaka yote haijawahi kuniangusha.
Sina hakika kama ni jukwaa sahihi, lakini kwa sababu ni makutano ya Watu wengi naamini nitapata ushauri.
Hapa kwangu kuanzia mwezi uliopita kumekuwa na mbu wengi hasa ndani ya nyumba. Niliamua kutumia dawa ya kuua wadudu aina ya rungu kwa ajili ya kuwaua lakini haijafua dafu. Unaweza kupuliza jioni na kufunga milango yote lakini ukirudi usiku unawakuta!!
Kuna mtu akanishauri kutumia dawa aina ya 'Hit' lakini hakuna matokeo mazuri!! Ukipuliza wanatulia lakini baada ya kama masaa mawili hali inajirudia.
Kimsingi kuzunguka nyumba yote na hata kwa majirani hakuna madimbwi labda tu nyasi na maua ya bustani.
Naomba ushauri nitumie dawa gani au nifanye njia gani kuwaangamiza kwa sababu wakuwa kero sana hasa usiku wakati wa kuperuzi net.
Ahsanta.
Nb: Naishi Dar.
Asante kwa namba, hopefully hujamwambia aweke cha udalali juu
Asante, ila harufu ya dawa huwa kali, nna mpango wa kuwa napulizia nje tu, ndani napiga dawa.
Kingine ni kujizoeza utaratibu wa kufunga milango na madirisha, japo huchosha ila inasaidia.
kweli uwezo wetu wa kufikiri umefikia hapa,waweza kuta wewe ni msomi mzuri tu ila kamdudu kadogo kama mbu kanakufanya uje jf au unasubiri msaada kwa hisani ya watu wa marekani
harufu inavumilika bwana kwa siku mbili tu. mie nikiona nzi ama mbu ndani najiskia kama kichaa kinapanda hivi.
Afu nzi wana kiburi, akiwa mmoja lazima akuhamishe chumba kama umelala, analamba vibaya, utadhani unalambwa na pampazi alovuliwa mtoto.
Nitajaribu kutumia huyo wako labda dawa yake ni user friendly, kuna wengine dawa zao zinanuka kama deep ya kuoshea ng,ombe(kuna mmoja alinifanyia paka wangu wote wakafa)
Unafuga paka (s)?
Ndo maana upo online mpaka usiku mnene........!!! Unafanya survey.
Dont study me, you won't graduate!!! I wont study you
Mkuu hao mbu huwa wanazaliana nyakati za mvua, kwa kuwa umesema mazingira ya nje ni salama nakushauri utafute dawa ya kuchanganya na maji uiweke kwenye pump ya kunyizia uipige nyumba nzima, hao mbu huwa na tabia ya kukaa kwenye zenye unyevunyevu hasa jikoni kama vyombo vya maji yapo wazi, nguo zilizotundikwa, chooni na bafuni, pia kwenye makochi hasa sofa.
Nimekushauri utumie dawa hiyo(kaulize duka la pembejeo na dawa za mifugo) kwani hizi za special spray hazina nguvu sana ya kuangamiza mazalia ya mbu.
nilikuwa sijaiona hii----ngoja nikajaribu kutafutaFanya hiviii....nenda kwenye maduka ya pembejeo uliza dawa inaitwa dudukili 10WP ambayo huwa inakuwa kwenye kipaketi cha 62.5g pamoja na doom ya maji ambayo inakuwa kwenye kichupa kidogo, tafuta bomba la kupiliza dawa, tia dudukili yote katika maji ya lita 10 na doom kwa kipimo utakachoandikiwa .. nadhani ni 20mls, koroga tia kwenye bomba puliza ndani darini, kwenye milango, madirisha na sehemu zilizojificha, kisha nje , kwenye mashimo ya vyoo, majani nk, ukiwaona mbu au mende ndani ya nyumba yako nitafute unitie viboko!! Haina harufu naa gharama yake hafiki elfu 12 kwa zote isipokuwa bomba ambalo unaweza kuazima.....hili tatizo lilinifanya nishindwe kuangalia tv kwangu ila siku hizi huwa nalala sebuleni nikiangalia tv...mimi nimezipata katika duka la hill - boko - dsm, kwa walio karibu na maeneo hayo
.....kazi kwenyu