Msaada tafadhali: Mbu wananisumbua!

Msaada tafadhali: Mbu wananisumbua!

platozoom

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
9,548
Reaction score
11,538
Sina hakika kama ni jukwaa sahihi, lakini kwa sababu ni makutano ya Watu wengi naamini nitapata ushauri.

Hapa kwangu kuanzia mwezi uliopita kumekuwa na mbu wengi hasa ndani ya nyumba. Niliamua kutumia dawa ya kuua wadudu aina ya rungu kwa ajili ya kuwaua lakini haijafua dafu. Unaweza kupuliza jioni na kufunga milango yote lakini ukirudi usiku unawakuta!!

Kuna mtu akanishauri kutumia dawa aina ya 'Hit' lakini hakuna matokeo mazuri!! Ukipuliza wanatulia lakini baada ya kama masaa mawili hali inajirudia.

Kimsingi kuzunguka nyumba yote na hata kwa majirani hakuna madimbwi labda tu nyasi na maua ya bustani.

Naomba ushauri nitumie dawa gani au nifanye njia gani kuwaangamiza kwa sababu wakuwa kero sana hasa usiku wakati wa kuperuzi net.

Ahsanta.

Nb: Naishi Dar.
 
Ngoja nisicheze mbali na huu uzi, maana jana tumbu tutatu tumepenya kwenye net tumenisumbua. Nikifungua kabati yaani utafikiri ni sebuleni kwao.
 
Unatakiwa kufanya fumigation. Usisahau chambers za choo pia, zifunuliwe na kupulizwa dawa kwa ndani. Wakati wa fumigation wapige dawa hadi ukutani. In residual effects.

kuna mshkaji anafanya fumigation bei rahisi sana. Inafaa kwa mtu asiependa kutumia net.
 
Ngoja nisicheze mbali na huu uzi, maana jana tumbu tutatu tumepenya kwenye net tumenisumbua. Nikifungua kabati yaani utafikiri ni sebuleni kwao.

Yaani hata mimi imenishangaza, jana kabla ya kwenda 'kuosha macho' nilipiga dawa ya 'Hit' ya nafikiri robo nzima, mpaka kuzunguka nyumba. Lakini nimerudi usiku nakutana nao sitting room!! nikaishia kusonya tu...............na wana bahati.........!!!!
 
Mkuu hao mbu huwa wanazaliana nyakati za mvua, kwa kuwa umesema mazingira ya nje ni salama nakushauri utafute dawa ya kuchanganya na maji uiweke kwenye pump ya kunyizia uipige nyumba nzima, hao mbu huwa na tabia ya kukaa kwenye zenye unyevunyevu hasa jikoni kama vyombo vya maji yapo wazi, nguo zilizotundikwa, chooni na bafuni, pia kwenye makochi hasa sofa.

Nimekushauri utumie dawa hiyo(kaulize duka la pembejeo na dawa za mifugo) kwani hizi za special spray hazina nguvu sana ya kuangamiza mazalia ya mbu.
 
Unatakiwa kufanya fumigation. Usisahau chambers za choo pia, zifunuliwe na kupulizwa dawa kwa ndani. Wakati wa fumigation wapige dawa hadi ukutani. In residual effects.

kuna mshkaji anafanya fumigation bei rahisi sana. Inafaa kwa mtu asiependa kutumia net.

Tuwekee namba yake ya simu ya biashara hapa. Si unaona hata Kaunga mbu watatu tu wamemtoa jasho..............Na maendeleo haya ya kisasa unafikiri hata yale mambo yetu yatafanyikaje net imezunguka kila wakati kitanda kizima!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hao mbu huwa wanazaliana nyakati za mvua, kwa kuwa umesema mazingira ya nje ni salama nakushauri utafute dawa ya kuchanganya na maji uiweke kwenye pump ya kunyizia uipige nyumba nzima, hao mbu huwa na tabia ya kukaa kwenye zenye unyevunyevu hasa jikoni kama vyombo vya maji yapo wazi, nguo zilizotundikwa, chooni na bafuni, pia kwenye makochi hasa sofa.
Nimekushauri utumie dawa hiyo(kaulize duka la pembejeo na dawa za mifugo) kwani hizi za special spray hazina nguvu sana ya kuangamiza mazalia ya mbu.

Inawezekana wanazaliana chooni, kwa sababu kama ni vyombo huwa napika kwa msimu!

Asante kwa ushauri. Ila ukinipa jina la hiyo dawa itakuwa vizuri nisije kununua sumu mbaya, si unajua hawa Wafanyabiashara wetu na utaalam
 
Yan kumbe ili tatizo tunalo wengi ngoja nisubir washaur ili na mm nipate kujikinga
 
Hahaha mimi sijawahi kutumia net kabisa nikiwa sehemu zenye joto.

their number is +255714007350

usisahau kubisha bei hadi akome. Ukipiga dawa unawarranty ya walau miezi 6 bila mbu wala kitorondo.
Tuwekee namba yake ya simu ya biashara hapa. Si unaona hata Kaunga mbu watatu tu wamemtoa jasho..............Na maendeleo haya ya kisasa unafikiri hata yale mambo yetu yatafanyikaje net imezunguka kila wakati kitanda kizima!!

. Usisahau kubisha beiusi
 
Last edited by a moderator:
Kuna mzee mmoja alikwapua dawa ya mbu pale Sinza super markiti. kama kuna mwenye namba yake atusaidie
 
Hizo zote ni boshini ni bora dawa ya kuchoma unawasha saa mbili za usiku hadi alfajir lakini na utapata raha ya kusoma na kuchati na intanet bila shida lakini huwa hawafi ni kuwafukuza ndani tu na kwa sasa zimekuja dawa zengeni mpya za kuchoma na hizo ziko kwenye kipakiti na hizo pia ni boshini na bei yake huwa vitatu kwa buku na unachukuwa kopo na unakoleza na mkaa hiyo nayo shida tuu
 
Au unaweza wewe mwenyewe kufanya fumigation.....fanya hivi tafuta dawa ya ngao inayotumiwa kuwekwa kwenye vyandarua.......nunua ya kutosha ,nunua na chupa ya kupulizia ,,,,pulizia ukutani na kwenye madirisha ya nyumba yako.....nyumba nzima mbu hatasogea.......
 
Asante, ila harufu ya dawa huwa kali, nna mpango wa kuwa napulizia nje tu, ndani napiga dawa.

Kingine ni kujizoeza utaratibu wa kufunga milango na madirisha, japo huchosha ila inasaidia.

Hahaha mimi sijawahi kutumia net kabisa nikiwa sehemu zenye joto.

their number is +255714007350

usisahau kubisha bei hadi akome. Ukipiga dawa unawarranty ya walau miezi 6 bila mbu wala kitorondo.

. Usisahau kubisha beiusi
 
Au unaweza wewe mwenyewe kufanya fumigation.....fanya hivi tafuta dawa ya ngao inayotumiwa kuwekwa kwenye vyandarua.......nunua ya kutosha ,nunua na chupa ya kupulizia ,,,,pulizia ukutani na kwenye madirisha ya nyumba yako.....nyumba nzima mbu hatasogea.......

Hapo sawa.
Nitaitumia hiyo kama ikishindikana namtafuta dalali King'asti anipe tena namba ya mtu wa fumigation ingawa harufu huwa inanitisha
 
Last edited by a moderator:
Hahaha mimi sijawahi kutumia net kabisa nikiwa sehemu zenye joto.

their number is +255714007350

usisahau kubisha bei hadi akome. Ukipiga dawa unawarranty ya walau miezi 6 bila mbu wala kitorondo.

. Usisahau kubisha beiusi

Asante kwa namba, hopefully hujamwambia aweke cha udalali juu
 
Asante, ila harufu ya dawa huwa kali, nna mpango wa kuwa napulizia nje tu, ndani napiga dawa.

Kingine ni kujizoeza utaratibu wa kufunga milango na madirisha, japo huchosha ila inasaidia.

Hata mimi hapo kwenye harufu ndo ishu. Lakini option ya kupiga nje ni nzuri zaidi.
Mbu wabishi hawa, imagine sasa hivi wametulia lakini ikiingia giza kidogo ni balaa, wanang'ata mikono mpaka unaona keyboard chungu.
 
Fanya hiviii....nenda kwenye maduka ya pembejeo uliza dawa inaitwa dudukili 10WP ambayo huwa inakuwa kwenye kipaketi cha 62.5g pamoja na doom ya maji ambayo inakuwa kwenye kichupa kidogo, tafuta bomba la kupiliza dawa, tia dudukili yote katika maji ya lita 10 na doom kwa kipimo utakachoandikiwa .. nadhani ni 20mls, koroga tia kwenye bomba puliza ndani darini, kwenye milango, madirisha na sehemu zilizojificha, kisha nje , kwenye mashimo ya vyoo, majani nk, ukiwaona mbu au mende ndani ya nyumba yako nitafute unitie viboko!! Haina harufu naa gharama yake hafiki elfu 12 kwa zote isipokuwa bomba ambalo unaweza kuazima.....hili tatizo lilinifanya nishindwe kuangalia tv kwangu ila siku hizi huwa nalala sebuleni nikiangalia tv...mimi nimezipata katika duka la hill - boko - dsm, kwa walio karibu na maeneo hayo
.....kazi kwenyu
 
Back
Top Bottom