Msaada: Nipo njia panda juu ya mahusiano yangu

Msaada: Nipo njia panda juu ya mahusiano yangu

Aisee we jamaa umenichekesha sana. Afu unakuta mkengele umeleta fujo afu ukimwomba akusaidie kuutuliza anakutolea nje.... wakati mita kumi toka alipo wako kama 8 hivi ambao wako tayari kukusaidia bila shuruti.

Makengele ni kama maendeleo... hayana chama
Mzee baba kweli ujue,na wadada wengi hawajui tu ni makosa sana kumnyima mwanaume hasa jamii ya asprin,gudume,zero iq n.k vitu vinavyopatikana mtaa wa pili tu hapo. Uanaume ni mgumu sana kwa kweli,jamaa alikuwa anamalizia testing

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee baba kweli ujue,na wadada wengi hawajui tu ni makosa sana kumnyima mwanaume hasa jamii ya asprin,gudume,zero iq n.k vitu vinavyopatikana mtaa wa pili tu hapo. Uanaume ni mgumu sana kwa kweli,jamaa alikuwa anamalizia testing

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaa dah... ma mi umenijumuisha na hao mabazazi???
 
Hapo ni kwamba tu umeweza kufaham hayo uliyoyaona, maana yake alikuwa bado yupo kweny stage ya kujaribu kuagana na maisha aliyokuwa nayo, issur ndogo sana, watu wanafumaniana wameshaoana na maisha yanaendelea bila shida, kwako yeye ni mchumba japo tayr mnaishi pamoja, kuishi pamoja kabla ya ndoa pia ndo changizo la hayo, usingekuwa unaishi naye usingeyafaham haya ambayo kimsingi hayana faida yyte kwako...huwa tunasema kisaikolojia usipende kuyafaham ya mwenzio yanayoumiza, achana nayo....so go on..haina haja ya kuanza kujiuliza maaswal mengi.

Endelea na mchakato wako, fanyeni ukaribisho huo...lkn hii issue unaifaham mwenyewe na usipende sana kuitangaza, kaa nayo mwenyewe piga moyo konde endeleen na maisha.

Kila mwanadamu ana mapungufu, ukisema leo unaachana na huyo unatafuta mwingine, mapunguf ya mwingine yanaweza kuwa ni changamoto zaid ya hayo uliyoyaona...hakuna mwanaume utamkuta mkamilifu, uliyepewa tunzs yeye, penda yeye...tena mwambie mume wangu hata ufanyeje mm nitakupenda tu wewe ni wangu, u will see....then achana na kumkumbusha...inasemwa pia kuliongelea jambo mara kwa mara unalipa nafasi....achana nalo...wala usilikumbushe ...Muombee mchumba wako...una nafasi nzur sana...kumbuka Esther ktk Biblia na mfalme Ahausuero. Ulilonalo leo ni dogo kuliko alilonalo mwenzio.
 
Kama nnamuona huyo mchepuko anavofurahia, yaani kwa paniki hili anajua soon unakaa pembeni anaingia yeye.

My advice, ndoa ziko chache sana kipindi hiki na kila ndoa inachangamoto. Pambana umtulize huyo jamaa yako na ndoa itatulia vzr kbsaaaa.
 
Kama nnamuona huyo mchepuko anavofurahia, yaani kwa paniki hili anajua soon unakaa pembeni anaingia yeye.

My advice, ndoa ziko chache sana kipindi hiki na kila ndoa inachangamoto. Pambana umtulize huyo jamaa yako na ndoa itatulia vzr kbsaaaa.
 
Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake, kwa mantiki hiyo yawezekana umempigia ile kujitambulisha akaona afanye yake akuumize au awaachanishe ashike yeye hiyo nafasi, ulikosea kumtafutaa sanaaaa na hivyo ulimpa nafasi ya kuharibu, furahia matokeo ya matendo yako

Don't hunt what you can't kill.
Huyu dada naye baadhi ya nut zimelegea kidogo kwenye nguzo ya medula obolongata,unawezaje kumuita Mshindani wako na kumuingiza chumbani kufanya uchambuzi kujua kama kweli alitakaswa katika kitanda hicho,hapo kafanya hovyo kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakushauri fanya maamuzi magumu ili kuokoa nafsi yako.
1. Achana nae ili ukauguze maumivu na apate kupona. Na wakati unafanya maamuzi yako, kumbuka tu usiwaze kuhusu aibu ama fedheha itakayo kupata kwasababu tayari alikuwa mmepanga kwenda kutoa mahari kwa wazazi.
2. Msamehe na hakikisha unasamehe kabisa huku ukimuomba Mungu akutie nguvu ili uvuke salama katika kipindi hiki kigumu sana unacho pitia. Na ukimsamehe hakikisha unafuta na usikumbuke wala kuzungumzia lolote kuhusu tukio ambalo limetokea, na tena vumilia pasipo kujali amekukisea nini na lengo lako liwe ni kugakikisha unaona unaishi na mumeo na mnajenga familia njema.

Jioni nikiwa naelekea huko mipango, nitapita hapo nje kwenu nikuone kama unaendelea vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anayeenda kutolewa mahari ni wewe, si ndio? Kwa mantiki hiyo atakayeolewa ni wewe...

Sasa sababu za kupaniki ni nini? Hivi nyie wasichana ni lini mtakuja kuamini mwanaume ni jasiri asiyeacha asili take? Asili ya mwanaume ni kumiliki mwanamke zaidi ya mmoja.

Hebu piga moyo konde endelea kula raha na huyo jabali. Maisha ni hayahaya tena mafupi sana.

Mme wako ni pale unapokuwa naye.

Babu nimemaliza narudi kitandani
Babuuu 😀😀
 
Ila wanaume Mungu anawaona jamani, me juzi yamenikuta kama yako.

Na sijui kashtukia kitu gani kila muda anataja ndoa tu me nam-zoom tu, sikubali sikatai nipo katikati maana nishajua siyo mume bora kwangu.
Sasa we mwache huyo uje ukutane na kipanga mwingine. Utamkumbuka nakuambia. Usije sema sijakuonya
 
Dada weka kautulivu kidogo tu utapata uelekeo mzuri tu. Kuchagua samaki mmoja katika bahari sio kazi ndogo. Wanaume tuna kazi ngumu mno katika hili,kaacha wengi na huyo aliyetuma sms ni mmoja tu kati ya waliokuwa katika bahari.

Hebu jipige kifuani jiambie mimi ndo mchaguliwa na mliwa wa milele. Nikwambie ukweli ukijivuruga hapo jamaa hana cha kupoteza kwa sababu ana akiba ya kutosha kabisa,atavua samaki mwingine na wewe ulianziwa process ya kutolewa magamba utatupwa baharini ukapambane na wenzio.
Kikubwa ungea nae kiupole kwa hekima na busara na si kumsimanga sana utakuwa unaharibu mchezo mzima.

Kikubwa zaidi nikupe kasiri kadogo dada angu" ukipewa uume na kuwa mwanaume japo kwa wiki moja tu utaona tunavyopata shida na hii mikengere yetu". Mtuombee tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahahahaha kwa kweli umenifurahisha mkuu .
 
Back
Top Bottom