Msaada: Nipo njia panda juu ya mahusiano yangu

miss chuga

JF-Expert Member
Dec 25, 2019
303
651
Habari zenu wapendwa? Poleni na majukumu, naombeni ushauri wenu katika hili maana hata sielewi nini cha kufanya Nina mpenz Wang nmeishi naye kwa miaka 4 sasa na mwezi wa 2 mwaka huu amepanga kupeleka mahari kwetu ili tufunge ndoa na nyumbani nimeshawapa taarifa kuwa kutakuwa na ugeni.

Cha kushangaza juzi usiku tumelala imeingia text kwenye cm yake ya mdada anamlalamikia kuwa yupo bize sana amemsusa hamjali Kama mwanzo kiufupi ilikuwa inamalalamiko kibao na ilionesha kuwa ni wapenzi.

Kwa usiku huo sikutaka kumwambia mpenzi wangu chochote nilichukua no za yule dada asubui nikampigia nikajitambulisha kuwa nimekuta text yake kwenye cm ya mme Wang kiukwel yule dada alishtuka akanambia kuwa mpenz Wangu alimtongoza na alimwambia hana mke na alikuwa anamleta hadi nyumban tunapoishi coz mm kuna kipindi nilisafiri mwezi mmoja.

Ila baada ya mda niliporud akawa anaenda naye gest kila akimwambia twende kwako akawa anamzungusha anamwambia kule kwangu Kuna mafundi wanapaka rangi kutakuwa na usumbufu, kiukweli niliumia sana sikuamini ninachokisikia nikamuuliza Kama ni kweli ameshakuleta hadi nyumbani ndani pakoje maana nilihisi labda ananidanganya coz sikuamin.

Kama mwanaume Wangu anaweza kuleta mwanamke mwingne kwenye kitanda ninacholala nae mm kiukweli huyu dada alinitajia kila kitu kilichopo ndani hadi rangi za mashuka sikuamini bdo nikamwambia njo kwangu akaja alipoingia ndani nikamuuliza ulivyoambiwa hana mke inamana hukuona vtu vyang vya kike humu ndani akanambia hii mikoba kwenye enga haikuwepo na viatu vyako kwenye stend sikuvikuta kwa maana hiyo inaonesha alivitoa akanambia pia na kabati la nguo alikuwa akijaribu kufungua lilikuwa limefungwa na funguo.

Baada ya hapo nilijarbu kuongea na mpenz Wangu akakataa kabisa kuwa hajafanya hivyo ila baada ya kumbana sana akakubali akaniomba msamaha sikumjibu hata Kama nimemsamehe nilimwambia kwa ulichonifanyia umeniumiza sana nitakufikiria toka hapo na maumivu makali sana kichwa kinaniuma sana sipati hata usingizi nimepoteza hisia naye kimapenzi nipo nae Ila Niko njia panda sielewi nifanyaje na nyumbani kwetu wanajua Kuna ugeni unaenda mwez wa 2 hapa sijui niachane naye au niendelee nae naombeni mnisaidie kuhusu ili jambo linaniumiza sana nahisi kuchanganyikiwa na mda alionipotezea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anayeenda kutolewa mahari ni wewe, si ndio? Kwa mantiki hiyo atakayeolewa ni wewe...

Sasa sababu za kupaniki ni nini? Hivi nyie wasichana ni lini mtakuja kuamini mwanaume ni jasiri asiyeacha asili take? Asili ya mwanaume ni kumiliki mwanamke zaidi ya mmoja.

Hebu piga moyo konde endelea kula raha na huyo jabali. Maisha ni hayahaya tena mafupi sana.

Mme wako ni pale unapokuwa naye.

Babu nimemaliza narudi kitandani
 
Ni kwel wanaume asili yao kuchepuka Ila Mimi kinachoniumiza sana kumleta huku ndani ninakoishi naye yani kila nikiona hiki kitanda maumivu yanaanza moja
Anayeenda kutolewa mahari ni wewe, si ndio? Kwa mantiki hiyo atakayeolewa ni wewe...

Sasa sababu za kupaniki ni nini? Hivi nyie wasichana ni lini mtakuja kuamini mwanaume ni jasiri asiyeacha asili take? Asili ya mwanaume ni kumiliki mwanamke zaidi ya mmoja.

Hebu piga moyo konde endelea kula raha na huyo jabali. Maisha ni hayahaya tena mafupi sana.

Mme wako ni pale unapokuwa naye.

Babu nimemaliza narudi kitandani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kwel wanaume asili yao kuchepuka Ila Mimi kinachoniumiza sana kumleta huku ndani ninakoishi naye yani kila nikiona hiki kitanda maumivu yanaanza moja

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo tatizo sio kuchepuka bali kuchepukia nyumbani???

Bora huyo kachepuka na huyo mmoja... wengine kitanda hichohicho majabali wanachepuka na mabaamedi, mahausigeli na mashemeji zao...
 
Dada weka kautulivu kidogo tu utapata uelekeo mzuri tu. Kuchagua samaki mmoja katika bahari sio kazi ndogo. Wanaume tuna kazi ngumu mno katika hili,kaacha wengi na huyo aliyetuma sms ni mmoja tu kati ya waliokuwa katika bahari.

Hebu jipige kifuani jiambie mimi ndo mchaguliwa na mliwa wa milele. Nikwambie ukweli ukijivuruga hapo jamaa hana cha kupoteza kwa sababu ana akiba ya kutosha kabisa,atavua samaki mwingine na wewe ulianziwa process ya kutolewa magamba utatupwa baharini ukapambane na wenzio.
Kikubwa ungea nae kiupole kwa hekima na busara na si kumsimanga sana utakuwa unaharibu mchezo mzima.

Kikubwa zaidi nikupe kasiri kadogo dada angu" ukipewa uume na kuwa mwanaume japo kwa wiki moja tu utaona tunavyopata shida na hii mikengere yetu". Mtuombee tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole Sana dada! Kama mna miaka minne naamini Kuna ifs and buts nyiingi, Kuna ups and downs nyiingi, lkn mnemhimili na kuvuka!

Kitendo Cha mshikaji kuuamua kupeleka ujumbe kwenu Ina maana anakuelewa! Anataka muache kuzini, mrasimishe Mahusiano yenu! Hicho alichokifanya na huyu mpinzani wako ni sawa na unachofanya nae saiv! Huyo siyo mmeo!

Naamini hata wew Kuna mtu ulimkuta nae, na wew huyo si wa kwanza kwako! Ni kweli inaumiza lkn nachokuambia ni kwamba, nyani ni walewale tofauti ni misitu tu! Kumuacha si suluhisho, zungumzeni!

Kama mtafungia Dar, msinisahau kadi ya ubwabwa! Dada msamehe mwenzio, maana kwa mazungumzo hayo, huyo anaekusumbua umeshampa talaka Tatu!

Rasimisheni Mahusiano yenu, mkishaoana, ataiheshimu hiyo nyumba automatically! Maana inawezekana hata mtaani anasema wew ni demu wake, ukiwa mke tayari hofu itatanda usoni mwake kwa Jina Yesu Kristu Mwana wa Nazareth! Alleluia!

Kila la kheri katika maandaliz ya ndoa yako!

Lugumya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina mpenz Wang nmeishi naye kwa miaka 4 sasa na mwezi wa 2 mwaka huu amepanga kupeleka mahari kwetu ili tufunge ndoa
cha kushangaza juzi usiku tumelala imeingia text kwenye cm yake ya mdada anamlalamikia kuwa yupo bize sana
nilichukua no za yule dada asubui nikampigia nikajitambulisha kuwa nimekuta text yake kwenye cm ya mme Wang

Una mpenzi wako na yupo mbioni kukutolea mahari....

Halafu then una lala naye na unamuita mume wako....

Hapa najaribu kujiuliza, kama umeshakuwa ukilala na mwanaume kwa muda, je mahari ni ya nini sasa????

Okay tuachane na hilo, kama mwanaume hajakuoa na analala na wewe, je kwa nini ushangae akilala na mwanamke mwingine ambaye hajamuoa pia?
 
Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake, kwa mantiki hiyo yawezekana umempigia ile kujitambulisha akaona afanye yake akuumize au awaachanishe ashike yeye hiyo nafasi, ulikosea kumtafutaa sanaaaa na hivyo ulimpa nafasi ya kuharibu, furahia matokeo ya matendo yako

Don't hunt what you can't kill.
 
Back
Top Bottom