Msaada; Nini cha kufanya ili kupona haraka masikio baada ya kutoboa

Titia

Senior Member
Jul 3, 2013
155
113
Habari zenu warembo na watanashati,
Mimi naombeni msaada wenu.

Nimetoboa masikio yapata wiki ya pili sasa. Nilitoboa kwa sonara na nikapewa na vihereni orijino vyenye mchanganyiko wa dhahabu na niliambiwa kwamba zile hereni ni za moja kwa moja nachotakiwa kufanya ni kupaka mafuta ya nazi kila siku na kuzungushia hereni kwa sikio.

Sasa tatizo nimefanya hivyo yapata wiki ya pili sasa lkn masikio hayana dalili za kupona. Mara kama yanatoa usaha kwa mbali wkt mwingine yanaonekana yamekauka.

Naomba msaada wapendwa nifanyeje ili yaweza kupona haraka.
NB: pia ngozi yangu nina mzio sitakiwi kuvaa hereni za kawaida kama silver basi original na gold hivyo hivyo.
 
Hayo mafuta ya nazi unatakiwa uyapashe yawe na joto kiasi sio la kuunguza. Ndo upakae hapo kwenye sikio ulipotoboa.
 
umesema ulipewa dhahabu mchanganyiko huku unasema una uzio hutakiwi kuvaa isiyokuwa dhahabu hueleweki, basi ziondoe uwe unavaa hereni yakubana sio aina hiyo acha masikio yazibe tu isisababishe madhara makubwa
 
umesema ulipewa dhahabu mchanganyiko huku unasema una uzio hutakiwi kuvaa isiyokuwa dhahabu hueleweki, basi ziondoe uwe unavaa hereni yakubana sio aina hiyo acha masikio yazibe tu isisababishe madhara makubwa[/Q
sonara aliniambia hizo ni orijinal hazitonisumbua. yamepona lkn nimepaka sprit.
 
umesema ulipewa dhahabu mchanganyiko huku unasema una uzio hutakiwi kuvaa isiyokuwa dhahabu hueleweki, basi ziondoe uwe unavaa hereni yakubana sio aina hiyo acha masikio yazibe tu isisababishe madhara makubwa
yamepona my, hereni niliambiwa na sonara hazisumbui. maana nilijieleza kuwa nna allergy.
 
Watu wazamani walikua wanasema anaekutoga masikio pia hatakiwi kua mzinzi au kutumika hadi upone mashart yake yalikua kama kutahiriwa ila asaivi mmmm
 
Watu wazamani walikua wanasema anaekutoga masikio pia hatakiwi kua mzinzi au kutumika hadi upone mashart yake yalikua kama kutahiriwa ila asaivi mmmm
Na atakayekutoboa anapaswa awe mtu mzima au mtoto mdogo ambae hajaaanza mambo ya kikubwa pia ndio wanafaaa kutoboa
 
Back
Top Bottom