Nini cha kufanya ukipata maambukizi ya covid 19

piego

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
289
Reaction score
425
Habari za jioni wanajamvi

Mimi ni medical personnel. Ningependa kutoa walau mchango wangu wa mawazo katika ugonjwa huu wa COVID 19 na namna bora ya kuukabili ugonjwa huu.

Siko hapa kwa ajili ya kupinga au kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa kuhusu ugonjwa huu, bali ninaongezea katika kile ninachoamini kuwa ni sahihi na kinaweza kusaidia kwa namna moja ama nyingine

1. Ugonjwa huu wa COVID `19 upo. Na unasambazwa na virusi vya SARS- CoV2 ( Corona Virus) ambavyo vinasambaa kwa kugusa sehemu/kitu ambacho kimebeba virusi hivi( contaminated areas) na mtu huyo akajishika machoni, puani au mdomoni. Lakini pia wanasayansi wanafikiri kuna uwezekano mkubwa pia virusi hivi vinaambukizwa KWA NJIA YA HEWA. Hivyo basi

- Ni Muhimu kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni, jizuie kujishika katika maeneo ya uso na kuvaa barakoa pindi utokapo nje ya makazi yako

- Kuvaa barakoa yoyote ( iwe surgical mask au barakoa ya kitambaa) ni muhimu kwa sababu inapunguza uwezekano wa kuambukizana. Barakoa za kitambaa hazina uwezo wa kuzuia kirusi hiki kusambaa kwa hewa, lakini inaweza kuzuia yule anayepiga chafya au kukohoa kurusha mate au majimaji na kusambaa eneo kubwa Zaidi na watu kuathirika ikiwa watashika eneo hilo. Pia inasaidia kuzuia kuruka matemate kutoka mtu mmoja mpaka mwengine wakati wa kuongea, au kijishika maeneo yaliyofunikwa na barakoa, hivyo wote tukivaa barakoa, tunapunguza sana spidi ya kusambaa kwa virusi hivi kwa namna moja ama nyingine, hivyo jambo hili si la kupuuzwa ..

- Matumizi ya vitakasa mikono kadiri uwezavyo

2. Kama huna shughuli ya maana kukufanya utoke nyumbani kwako ni vizuri ukae nyumbani. Hii ni njia pekee ya kukuhakikishia walau usalama wako. Unapotoka nje, sawa utanawa mikono na kuvaa barakoa.. lakini kuna vitu utavibeba vinaweza kuwa vimekuwa ‘contaminated’ bila wewe kujua mfano: funguo, nguo ulizovaa, wallet, pochi, bidhaa ulizobeba( kila mtu alikuwa anachagua, kabla ya wewe kuchagua na kuibeba) .. hivyo ni ngumu sana kuweza kukabili kila kitu na kukifanya kiwe safi.. unavyopunguza nyendo, ni bora Zaidi, kwani unapunguza uwezekano wa kubeba virusi na kuvialika nyumbani kwako kwa namna moja ama nyingine

- Usisubiri mpaka litoke tamko kuwa tusitoke nje_’lockdown’_.. au usitegemee utakuja kuambiwa kuwa misikiti na makanisa yafungwe, au baa zote zifungwe… wewe jiongeze mwenyewe. Jinsi maingiliano na mkusanyiko unavyokuwa mkubwa ndio uwezekano wa maambukizo unakuwa mkubwa Zaidi.

- Usisubiri nduguyo wa karibu aumwe/kufariki kwa ugonjwa huu ndio uanze kuwa serious. Huwezi jua , it might be too late

3. Asilimia 80% ya watu wote wanaopata maambukizi wanapata dalili ambazo zinaweza kudumu kwa muda wa wiki moja hadi mbili. Watu hawa wanaweza KUPONA WENYEWE BILA KUHITAJI HUDUMA ZA HOSPITALI. Asilimia 15% watahitaji uangalizi hospitali kwa msaada wa kati, lakini watapona, na asilimia 5% wanaweza kupata ugonjwa mkali Zaidi na kuhitaji uangalizi wa hali ya juu ( ICU ) na baadhi yao, wanakuwa na nafasi kubwa ya kupoteza maisha.

- Ugonjwa hauchagui umri, watoto , vijana hadi wazee wanaweza kupata.

- Kinga yako ya mwili ndio itaamua uwe miongoni mwa wale wa asilimia 80%, 15% au 5%

- Kama kinga yako iko vizuri, bado unaweza kuambukizwa ukaumwa kiasi au unaweza usionyeshe dalili kabisa lakini una uwezekano mkubwa wa kuambukiza wengine, hivyo unaweza kuhatarisha maisha ya mzazi wako, watu wengine wa karibu wenye kisukari, magonjwa ya moyo, cancer na kuwasababishia vifo ambavyo vingeweza kuzuilika

- Ni vizuri kila mtu akajilinda ili umlinde mwenzio/mzazi/mtoto wako/jirani yako etc

- Pia tukumbuke sisi watanzania hatuna hulka ya kupima afya zetu, hivyo wengi tunaweza jikuta tuna kansa au kisukari bila kujijua na kudhani tupo vizuri kumbe la hasha!! Na magonjwa haya kwa sasa hayachagui vijana wala wazee.. hivyo huwezi jua , unaweza kuwa wewe ni miongoni mwa ‘ wenye magonjwa sugu’

UFANYE NINI UKIPATA MAAMBUKIZO:
Ikiwa umeambukizwa, unaweza sikia hali ya homa kali, kikohozi, maumivu ya kifua, kubanwa pumzi, madonda kwenye koo, mwili au misuli kuuma, kuchoka sana au dalili kama za mafua. Mimi naamini pia kupungua/kukosa uwezo wa kuhisi harufu au ladha ni mojawapo ya dalili ya ugonjwa huu( hili liko debatable- lakini wengi wa waliothibitika kwa kupimwa na kukutwa na maambukizi ya corona wameripoti kupata dalili hii)- na inaweza kuwa ni dalili pekee na usiumwe kingine chochote au usipate dalili kabisa

- Nashauri kama ukihisi dalili hizi, jitahidi kujitenga na watu kwa kiasi uwezavyo. Ukikaa nyumbani na kujizuia kukutana na watu wengine ni vizuri Zaidi kwani utapunguza sana kasi ya maambukizo.

- Wengi wanaweza kupona bila kuhitaji uangalizi wa hospitali. Kwani, hata hospitali utapata matibabu ya kuondoa dalili tu, sababu hamna dawa ya COVID 19. Hivyo basi, unashauriwa kutumia dawa za kupunguza homa ie. Paracetamol, dawa za mafua eg: anti histamines, kusukutua koo kwa maji ya uvuguvugu yenye chumvi, kutumia vyakula vyenye vitamin C na kula mlo kamili( walau wenye matunda na mboga mboga za kutosha), kunywa maji mengi, kupumzika kiasi cha kutosha na kuupa mwili nafasi ya kupambana na virusi hivi. Pia tiba za mvuke zinaweza kusaidia.(ingawa hili halina uthibitisho sana kisayansi)

- Pia walinde wengine kadri uwezavyo: vaa barakoa, nawa mikono mara kwa mara kuzuia kusambaza virusi kila sehemu unayoshika. Tumia maliwato vizuri, decontaminate kadiri uwezavyo maeneo unayoyatumia au kushika.

- Punguza kutumia vitu/sehemu zinazotumiwa na watu wengine wengi ie. Usafiri wa uma, vyoo vya uma,maofisini
- Jitahidi sana kuwalinda wale unaowajua fika wako hatarini ie. Wazee, wenye maradhi mengine , watoto wachanga
- Ikiwa dalili zinakuwa mbaya siku hadi siku, ni vizuri kwenda hospitali mapema. Ni vizuri kupima na kujihakikishia afya yako na ikiwa unahitaji msaada wa ziada, basi itakuwa ni rahisi kusaidiwa ikiwa utawahi hospitali mapema.

- Ikiwa ulimhudumia, au ulikuwa karibu na mgonjwa/ mtu anayehisiwa kwa kiwango kikubwa kuwa na maradhi haya, basi ni vizuri pia kujitenga na watu na kuwahi kufanya vipimo ili kuepuka kusambaa Zaidi kwa ugonjwa huu

Kuna uwezekano mkubwa watu wengi wana dalili za ugonjwa huu ila wanahofia kwenda kupima . Au wengine wana hofu ya kuwekwa quaranteen na kuwa mbali na familia. Badala ya kuzunguka mtaani na kuendelea kusambaza huku ukiwa na hofu , ni vizuri Zaidi ujitenge na watu kadri unavyoweza, KAA NDANI, JITENGE. WALINDE WENZAKO, USISAMBAZE!!Na ukihisi dalili zinazidi ni VIZURI KUWAHI HOSPITALI, kwani utapata msaada haraka.

Nina mengi ya kuandika ila nimeona nishee nanyi hayo machache ili tusaidiane katika mapambano na ugonjwa huu.. mimi muda mwingi siko online. Hivyo mnaweza kuuliza maswali na nikakosa kuyajibu. Nakaribisha yeyote mwenye kuweza kujibu na kuchangia Zaidi juu ya mada hii.
Asanteni
 
Njia sahihi ndio hii kutoka kwa mkemia
IMG_20200422_184713_505.JPG
IMG_20200422_184759_301.JPG

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ni kujifukiza tuu, hamna dawa hamna chanjo...ila kama Mh. Raisi alivyosema, kuna waraka wa maelekezo ya hizi njia zetu za asili tuufuate..natural remedies..kitunguu SAUMU, pili pili kichaa, tangawizi na kitunguu maji, mix vyote saga kunywa usiwe mbishi...waafrika tuna asili zetu na zinasaidia..ukitaka chanjo subiria "clinical test" za mzungu
IMG-20200422-WA0007.jpg
IMG-20200422-WA0008.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom