Msaada, naweza pata BP muda si mrefu

bhikola

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,130
1,660
Habari wadau,

Kama mada inavyoeleza

Kwa kifupi, at this age 45+ nimeajiriwa sekta binafsi (kampuni ya mawasiliano), nina wake 2 (wote ni waajiriwa wa serikali) na watoto 5 (mdogo kabisa ana miaka 5). Maisha yanakwenda poa tu kwa hali ya kitanzania. Ninaishi kwangu, na nina nyumba nyingine 4 sehemu mbalimbali Tanzania

Changamoto niliyonayo ni hofu. Yaani hata sijui ninaogopa nini?! Lakini nimejawa ha hofu kiasi kwamba kuna time nakosa kabisa usingizi. Nimejaribu kusoma vitabu, makala, na majarida yanayoeleza fear, anxiety, and worries lakini naona sipati ufumbuzi.

Wakuu msaada nifanye nini? Nimeongea na wake zangu mmoja mmoja na wote kwa pamoja maana ilifikia time sifikii ule "uwezo wangu chumbani". Lakini sielewi aisee. I am real worried naweza pata pressure au sukari soon - Mungu aniepushie mabalaa haya

Nawasilisha
 
wake wawili tu ndilo tatizo.... ukilala kwa mkubwa unahofia mdogo analiwa.... TENA WANAUME WENGINE WANAKULAGA KOTEKOTE. pAMBANA NA HALI YAKO.
 
Unawaza sana kufa pili ujiamini Unawaza sana wake zako na mali zako badala ya kuwaza mwili wako jipende wewe tembelea sehemu zenye kelele kuondoa mfadhaiko wa moyo
 
Jitahidi kubadili mfumo wa vyakula zingatia mboga mboga kwa wingi na mazoezi pia usipende kukaa mwenyewe muda mrefu
Usiwe na wasiwasi na wake zako jiamini na uwa amini pia
 
Pole sana Mkuu..jaribu kuwaona wataalam wa mambo ya saikolojia uwaelezee kinaga ubaga nn kinakusumbua hasa nadhani unaweza pata suluhisho la tatizo lako..humu ndani wastaarabu wapo na wahuni pia wapo ambao kwa mtazamo wangu wanaweza kuongeza tatizo zaidi badala ya kulitatua,asante

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Morogoro
 
ili uweze kusaidiwa lazima tujue ni hofu ya kitu gani inakusumbua,,,,,
hiyo hofu uliyonayo ni ya kuhusu nini?
 
Hapo tatizo ni kwamba unalogwa na wote hao wake wawili so utachanganyikiwa.
HAPO NI KUWA DAWA ZINAGONGANA.
Habari wadau
Kama mada inavyoeleza
Kwa kifupi, at this age 45+ nimeajiriwa sekta binafsi (kampuni ya mawasiliano), nina wake 2 (wote ni waajiriwa wa serikali) na watoto 5 (mdogo kabisa ana miaka 5). Maisha yanakwenda poa tu kwa hali ya kitanzania. Ninaishi kwangu, na nina nyumba nyingine 4 sehemu mbalimbali Tanzania
Changamoto niliyonayo ni hofu. Yaani hata sijui ninaogopa nini?! Lakini nimejawa ha hofu kiasi kwamba kuna time nakosa kabisa usingizi. Nimejaribu kusoma vitabu, makala, na majarida yanayoeleza fear, anxiety, and worries lakini naona sipati ufumbuzi.
Wakuu msaada nifanye nini? Nimeongea na wake zangu mmoja mmoja na wote kwa pamoja maana ilifikia time sifikii ule "uwezo wangu chumbani". Lakini sielewi aisee. I am real worried naweza pata pressure au sukari soon - Mungu aniepushie mabalaa haya
Nawasilisha
 
Kwa kifupi, at this age 45+ nimeajiriwa sekta binafsi (kampuni ya mawasiliano), nina wake 2 (wote ni waajiriwa wa serikali) na watoto 5 (mdogo kabisa ana miaka 5). Maisha yanakwenda poa tu kwa hali ya kitanzania.
Changamoto niliyonayo ni hofu. Nimeongea na wake zangu mmoja mmoja na wote kwa pamoja maana ilifikia time sifikii ule "uwezo wangu chumbani". Lakini sielewi aisee. I am real worried naweza pata pressure au sukari soon - Mungu aniepushie mabalaa haya
Nawasilisha
Pole, hofu ni Roho ya shetani, na usipotafuta amani ya kweli itakupoteza!
Binafsi niliwahi kutaabika na hofu, Mdogo wangu wa mwisho aliwahi pia kutaabika na hofu.
Nilikuwa naona vitu vya ajabu ajabu sana! rafiki yangu mmoja anasema
"picha za manyau nyau" like watu wananiwinda kuniua", da kumbe ilikuwa Illusions tu.
Pata muda sikiliza mahubiri, bila kujali dini uliyo nayo, ukiweza hudhuria hata Kanisani, utapata Amani ya kweli.
1.https://youtu.be/T5Ne1TqP6Tg
2.https://youtu.be/605ciBotGvE
3.https://youtu.be/sL8boXkdG8A
4.https://youtu.be/JiwJupmnJc4
God bless You.
 
Mkuu usiwe unakaa peke yako, jichanganye sehemu yenye stori za hapa na pale mfano vijiwe vya kahawa/tangawizi, draft. Kama Ni mpenzi wa mpira nenda vibanda umiza. Kama ni mpenzi wa music, sikiliza miziki unayoipenda.
 
Ongeza mke mwingine wa tatu na ambaye siyo mwajiriwa serikalini ili akusaidie kupunguza hiyo hofu/stress baada ya hao wawili kushindwa kukusaidia.
 
epuka kukaa peke yako muda mwingi Mkuu,tafuta kitu kitakachokuweka busy simply nunua PS4 na padi 2 uwe unacheza na wanao itasaidia
 
Back
Top Bottom