Socialphobia + anxiety + depression + panic attack inaniua taratibu! Msaada

Maiti

Maiti

Member
Joined
May 14, 2018
Messages
44
Points
125
Maiti

Maiti

Member
Joined May 14, 2018
44 125
Kama ni udongo Mungu kaumba basi mi ni udongo wa mwisho kabisa tena mfinyanzi/tifutifu.

Niombe radhi kwa aina ya uandishi mbovu ntakayoandika hapa maana ni matokeo ya anxiety.

Mimi ni kijana mwenye umri 29, ambaye mpaka sasa siwezi kujieleza, sina confidence, sijui kipaji changu, sina marafiki, sihudhurii misiba, sherehe na shughuli zote zenye mikusanyiko ya watu ( na ukinipigia simu kunialika nije basi nitatoa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu ili mradi tu nisije ili niwe free), sina girlfriend/mke, most of my time napenda kushinda mwenyewe, sina kazi, sina ajira rasmi.

Nilikuwa college nasoma degree ila anxiety ikanifanya nikatishe masomo yangu ili niwe free maana sikuweza kuhimili hofu ya kujumuika na wenzangu kwenye discussions/ presentation na mengine mengi yanayohusiana na kujieleza.

Nimesali sana ila sasa nimepoteza imani ya Mungu ninayemtumikia maana anaona ninayoyapitia ila anakausha so what next? it means nipo duniani kimakosa right? so sioni faida ya kuishi mpaka sasa.

Kuhusu familia naweza kusema kuwa 95% sikuwa treated right, my parents walikuwa overprotective sana sikupewa ule uhuru wa kujichanganya na wenzangu pale nilipohitaji na sikupewa ule uhuru wa kujieleza zaidi pale nilipohitaji kufanya hivo so hii iliaffect maisha yangu ya utoto kuanzia kushiriki michezo na wenzangu mitaani , darasani katika shule zote nilizopita na hadi chuo kikuu.

Hii imeathiri vipikitaaluma?
Mfano unaweza ukawa unajua kitu na wengine hawajui sasa unatamani uwajuze/ujibu ila sababu ya anxiety siwezi kufanya hivo tena so nakaa nalo moyoni hii yote sababu siko na nguvu ya kujieleza.

Niko na low self esteem/sijikubali kwa kweli na hii siyo kwa mapenzi yangu ila nahisi kuna baadhi ya stages nilipokuwa mtoto sikuzipitia vyema na hazikuwa fair kwangu na ndizo zimeleta haya nayopitia sasa.

Not talkative at all. Ni mwepesi kuchange mood haraka pale napokwazika, kinachonishangaza zaidi ni kwamba kila napokwazika au nikikumbana na situation yoyote ambayo inanilazimu nilie ili nisahau ila SILII nakaa nalo moyoni na kila nikijaribu kujilazimisha kulia machozi hayatoki! ila tumboni na moyoni nasikia maumivu sana its like kama roho inalia sana ndani kwa ndani ila uso mkavu hauoneshi zaidi ya kubaki kutetemeka tu na kutokwa jasho + mapigo ya moyo kwenda kasi.

Hivi kuna binaadamu anayeishi kama mimi kweli?

Mwisho niseme tu kwamba anxiety imeathiri my lifestyle/ sio mtu wa kucheka/kufurahi at all, sio mtu wa kula japo uwezo kupika/kununua chakula ninao kwa maana hiyo nimedhohofu sana kimwili, anxiety imeathiri uwezo wangu wa kufikiri sababu sio mtu wa kujichanganya na watu so nashindwa kuwaza na kuongea vitu vya kujenga zaidi, anxiety imeathiri imani yangu kiroho si mkristu wala muislamu, anxiety imenipotezea marafiki wengi wao wanahisi naringa ila ukweli ni kwamba siko hivyo, nawa/niliwahitaji sana kwenye mambo yangu ya mafanikio ila hofu imefanya kutojumuika nao.

Nimekata tamaa ya kuishi. Ni bora nilale usingizii wa milele ili niepuka tabu hizi ambazo Mungu wenu anaona ila ananikaushia tu. Wanasema Mungu hakupi mzigo usiouweza pia wanasema What doesnt kill you make you stronger ila kwa hii hapana kwa kweli.

Binafsi sinywi pombe, sivuti unga wala sigara sina tabia mbaya za kimakundi/wahuni kwa hilo nashukuru ila natamani nianze kunywa pombe ila naogopa sitaacha maana ndo itakuwa tabia yangu daima incase matatizo yangu nikayasahau kwa muda mfupi baada ya kulewa.

Niombe radhi kwa mwandiko wangu mbovu dunia nzima utadhani nimezaliwa Rwanda huko kumbe ni mtz na mdaresalaam wa hapa hapa!

Yaani hapa nilivyoandika hivi najisikia amani sana its like kama kuna kamzigo nimekatua hivi mwilini mwangu.

Niwashukuru wale wote mlio/mnaoshirikiana nami kwenye maisha yangu ya kawaida/ mtaani, college na mitandaoni.
 
Dr. Wansegamila

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Messages
1,560
Points
2,000
Dr. Wansegamila

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2012
1,560 2,000
Pole sana kijana. Kwanza badilisha hilo jina unalotumia humu, unamkufuru hata Mwenyezi Mungu.

Uzuri ni kwamba wewe tayari tatizo lako unalifahamu vizuri sana, na umeweza kulieleza kwa ufasaha kabisa kiasi cha ku pin point kwamba kiini ni nini.

Unahitaji kuchukua hatua moja tuu ya ziada ambayo itakua a turning point kwa maisha yako. SEEK HELP!! Tafuta msaada kuhusiana na hiyo hali yako kwa wataalamu au mtu mzima unaemuamini na kuona kwamba anaweza kuwa msaada kwako,
Nenda hata hosiptali, ingia chumba cha daktari mwambie wewe huna tatizo physically, ila tu unahitaji mtu ambae anaweza kukusikiliza.

Unahitaji tu kuongea na mtu na yeye anachotakiwa kufanya ni kukusikiliza tuu, na kukufanya uongee zaidi, Basi!!
Uko mkoa gani kijana? I can conect you with someone who might help you out. Natamani ningekuwepo mkoa uliopo, ningekusaidia mimi mwenyewe bila kuhitaji chochote kile kutoka kwako.

Pia kijana, unatakiwa kujikumbusha kwamba wewe mwenyewe nie mwamuzi wa kile ambacho kitatokea katika maisha yako; na sio mtu au kitu kingine chochote. At this point in your life, kitu kitakachotokea baada ya hapa, kitaamuliwa na WEWE MWENYEWE.

Je, unaweza kuongea vizuri lugha ya kingereza? Na ni mpenzi wa kusoma vitabu? Kama jibu ni ndiyo, kuna kitabu nataka nikupatie ambacho nadhani kinaweza kukusaidia.
Maiti
 
Maiti

Maiti

Member
Joined
May 14, 2018
Messages
44
Points
125
Maiti

Maiti

Member
Joined May 14, 2018
44 125
Asante mkuu wangu Dr. Wansegamila kwa kunipa moyo, unaweza kunipa link ya hiko kitabu nikisome ila nisikudanganye tu, hiko kitabu sina uhakika kama kitabadili chochote kwenye maisha yangu maana nimesoma vingi na nimetoka kapa. Its like kama akili yangu ishakubali kilichotokea na haiko tayari kubadilika. naweza nikafanya changes leo ila kesho nikarudi vile vile nilivyokuwa mwanzo. Alafu hospitali nyingi wako after money so nimekata tamaa kwa hilo pia.
 
Dr. Wansegamila

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Messages
1,560
Points
2,000
Dr. Wansegamila

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2012
1,560 2,000
asante mkuu wangu kwa kunipa moyo, unaweza kunipa link ya hiko kitabu nikisome ila nisikudanganye tu, hiko kitabu sina uhakika kama kitabadili chochote kwenye maisha yangu maana nimesoma vingi na nimetoka kapa. Its like kama akili yangu ishakubali kilichotokea na haiko tayari kubadilika. naweza nikafanya changes leo ila kesho nikarudi vile vile nilivyokuwa mwanzo. Alafu hospitali nyingi wako after money so nimekata tamaa kwa hilo pia.
Nime attach hicho kitabu hapa; kinaitwa "The Secret"; Kinajaribu kueleza kwamba chochote ambacho kinakutokea kwenye maisha yako, YOU are the one who attracted it to your life. CHOCHOTE KILE. Ni kitabu kizuri.
Pia, kama unafikiri kuwa hospitali ziko after money, well and good. Just find ANYONE to talk to. Unahitaji hicho kwa sasa kuliko kitu kingine chochote kile. Tafuta mtu uongee nae, ufunguke kuhusu kila kitu unavyojisikia, your disappointment, your failures, kila kitu. Itakusaidia sana. Maiti
 
Attachments:

Maiti

Maiti

Member
Joined
May 14, 2018
Messages
44
Points
125
Maiti

Maiti

Member
Joined May 14, 2018
44 125
Nime attach hicho kitabu hapa; kinaitwa "The Secret"; Kinajaribu kueleza kwamba chochote ambacho kinakutokea kwenye maisha yako, YOU are the one who attracted it to your life. CHOCHOTE KILE. Ni kitabu kizuri.
Pia, kama unafikiri kuwa hospitali ziko after money, well and good. Just find ANYONE to talk to. Unahitaji hicho kwa sasa kuliko kitu kingine chochote kile. Tafuta mtu uongee nae, ufunguke kuhusu kila kitu unavyojisikia, your disappointment, your failures, kila kitu. Itakusaidia sana. Maiti

asante sana mkuu ntajitahidi nifanye hivo
 
T

Tuchki

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2017
Messages
1,354
Points
2,000
T

Tuchki

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2017
1,354 2,000
Samahan maiti..Naomba unijibu maswali yangu kidogo..umezaliwa tarehe ngapi Na mwezi gani, maana kuna watu wanaathirika Na depression kutokana Na miezi waliozaliwa wanasema kipindi cha mwezi ukiwa foolmoon
Mkuu hilo ni jina la kimtandao tu, haliwezi kubadili chochote juu yangu so usitishike kaka. Feel free ongea chochote ntakusikia na ntajaribu kufanyia kazi hata kama kitaniumiza sitajali.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
T

Tuchki

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2017
Messages
1,354
Points
2,000
T

Tuchki

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2017
1,354 2,000
Maiti

Maiti

Member
Joined
May 14, 2018
Messages
44
Points
125
Maiti

Maiti

Member
Joined May 14, 2018
44 125
Samahan maiti..Naomba unijibu maswali yangu kidogo..umezaliwa tarehe ngapi Na mwezi gani, maana kuna watu wanaathirika Na depression kutokana Na miezi waliozaliwa wanasema kipindi cha mwezi ukiwa foolmoon

Sent using Jamii Forums mobile app
Hello Mkuu Tuchki kwa sababu za kiprivacy sitoweza kuweka tarehe yangu hapa in public labda in private. ila nyota yangu ni kaa
 
Don Clericuzio

Don Clericuzio

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2017
Messages
7,185
Points
2,000
Don Clericuzio

Don Clericuzio

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2017
7,185 2,000
Mkuu hilo ni jina la kimtandao tu, haliwezi kubadili chochote juu yangu so usitishike kaka. Feel free ongea chochote ntakusikia na ntajaribu kufanyia kazi hata kama kitaniumiza sitajali.
Sometimes we create our destinies bila kujua, you might think kwamba ni mtandaoni tu lakini it didn't just come.

Ngoja nisome michango ya wadau tutapata tu majibu.

Mshana Jr, Heaven Sent, Sky Eclat, Da'Vinci: mnaweza kuwa na mchango hapa.
 
Maiti

Maiti

Member
Joined
May 14, 2018
Messages
44
Points
125
Maiti

Maiti

Member
Joined May 14, 2018
44 125
Sometimes we create our destinies bila kujua, you might think kwamba ni mtandaoni tu lakini it didn't just come.

Ngoja nisome michango ya wadau tutapata tu majibu.

Mshana Jr, Heaven Sent, Sky Eclat, Da vincci; mnaweza kuwa na mchango hapa.
sina uhakika kwa kweli, ila asante kwa kunisaidia kuwaita wakuu wengine nipate ushauri wao pia.
 
Don Clericuzio

Don Clericuzio

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2017
Messages
7,185
Points
2,000
Don Clericuzio

Don Clericuzio

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2017
7,185 2,000
sina uhakika kwa kweli, ila asante kwa kunisaidia kuwaita wakuu wengine nipate ushauri wao pia.
Kuna thread naitafuta nitaiweka hapa, kuna watu kibao wanapitia kwenye hii hali unayoipitia, ukisoma michango ya wadau hutakosa chochote.

Ila ondoa mentality ya kwamba haiwezekani.
 
U

Upendo iswa

Member
Joined
Aug 28, 2018
Messages
49
Points
125
U

Upendo iswa

Member
Joined Aug 28, 2018
49 125
Kama ni udongo Mungu kaumba basi mi ni udongo wa mwisho kabisa tena mfinyanzi/tifutifu.

Niombe radhi kwa aina ya uandishi mbovu ntakayoandika hapa maana ni matokeo ya anxiety.

Mimi ni kijana mwenye umri 29, ambaye mpaka sasa siwezi kujieleza, sina confidence, sijui kipaji changu, sina marafiki, sihudhurii misiba, sherehe na shughuli zote zenye mikusanyiko ya watu ( na ukinipigia simu kunialika nije basi nitatoa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu ili mradi tu nisije ili niwe free), sina girlfriend/mke, most of my time napenda kushinda mwenyewe, sina kazi, sina ajira rasmi.

Nilikuwa college nasoma degree ila anxiety ikanifanya nikatishe masomo yangu ili niwe free maana sikuweza kuhimili hofu ya kujumuika na wenzangu kwenye discussions/ presentation na mengine mengi yanayohusiana na kujieleza.

Nimesali sana ila sasa nimepoteza imani ya Mungu ninayemtumikia maana anaona ninayoyapitia ila anakausha so what next? it means nipo duniani kimakosa right? so sioni faida ya kuishi mpaka sasa.

Kuhusu familia naweza kusema kuwa 95% sikuwa treated right, my parents walikuwa overprotective sana sikupewa ule uhuru wa kujichanganya na wenzangu pale nilipohitaji na sikupewa ule uhuru wa kujieleza zaidi pale nilipohitaji kufanya hivo so hii iliaffect maisha yangu ya utoto kuanzia kushiriki michezo na wenzangu mitaani , darasani katika shule zote nilizopita na hadi chuo kikuu.

Hii imeathiri vipikitaaluma?
Mfano unaweza ukawa unajua kitu na wengine hawajui sasa unatamani uwajuze/ujibu ila sababu ya anxiety siwezi kufanya hivo tena so nakaa nalo moyoni hii yote sababu siko na nguvu ya kujieleza.

Niko na low self esteem/sijikubali kwa kweli na hii siyo kwa mapenzi yangu ila nahisi kuna baadhi ya stages nilipokuwa mtoto sikuzipitia vyema na hazikuwa fair kwangu na ndizo zimeleta haya nayopitia sasa.

Not talkative at all. Ni mwepesi kuchange mood haraka pale napokwazika, kinachonishangaza zaidi ni kwamba kila napokwazika au nikikumbana na situation yoyote ambayo inanilazimu nilie ili nisahau ila SILII nakaa nalo moyoni na kila nikijaribu kujilazimisha kulia machozi hayatoki! ila tumboni na moyoni nasikia maumivu sana its like kama roho inalia sana ndani kwa ndani ila uso mkavu hauoneshi zaidi ya kubaki kutetemeka tu na kutokwa jasho + mapigo ya moyo kwenda kasi.

Hivi kuna binaadamu anayeishi kama mimi kweli?

Mwisho niseme tu kwamba anxiety imeathiri my lifestyle/ sio mtu wa kucheka/kufurahi at all, sio mtu wa kula japo uwezo kupika/kununua chakula ninao kwa maana hiyo nimedhohofu sana kimwili, anxiety imeathiri uwezo wangu wa kufikiri sababu sio mtu wa kujichanganya na watu so nashindwa kuwaza na kuongea vitu vya kujenga zaidi, anxiety imeathiri imani yangu kiroho si mkristu wala muislamu, anxiety imenipotezea marafiki wengi wao wanahisi naringa ila ukweli ni kwamba siko hivyo, nawa/niliwahitaji sana kwenye mambo yangu ya mafanikio ila hofu imefanya kutojumuika nao.

Nimekata tamaa ya kuishi. Ni bora nilale usingizii wa milele ili niepuka tabu hizi ambazo Mungu wenu anaona ila ananikaushia tu. Wanasema Mungu hakupi mzigo usiouweza pia wanasema What doesnt kill you make you stronger ila kwa hii hapana kwa kweli.

Binafsi sinywi pombe, sivuti unga wala sigara sina tabia mbaya za kimakundi/wahuni kwa hilo nashukuru ila natamani nianze kunywa pombe ila naogopa sitaacha maana ndo itakuwa tabia yangu daima incase matatizo yangu nikayasahau kwa muda mfupi baada ya kulewa.

Niombe radhi kwa mwandiko wangu mbovu dunia nzima utadhani nimezaliwa Rwanda huko kumbe ni mtz na mdaresalaam wa hapa hapa!

Yaani hapa nilivyoandika hivi najisikia amani sana its like kama kuna kamzigo nimekatua hivi mwilini mwangu.

Niwashukuru wale wote mlio/mnaoshirikiana nami kwenye maisha yangu ya kawaida/ mtaani, college na mitandaoni.
Hongera kwa kujua tatizo linalokusumbua hiyo ni tiba tosha.

Jaribu kujichanganya na watu hasa wa rika lako, pia fanya mazoezi hata kama hupendi nenda tu hata kiwanjani kaangalie watu wanavyocheza mpira.

Tafuta mtu mzima unayemwamini mwelezee tatizo lako hapa nashauri zaidi professional counselor naimani utabadilika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,284,775
Members 494,236
Posts 30,839,360
Top