bhikola
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,133
- 1,668
- Thread starter
- #41
Kuna kitu umeficha hapa.
Sema ukweli kuna yoyote ambaye umemfanyia ubaya na unahisi labda atakurudishia kisasi?? Wake zako unawaamini kwa asilimia ngapi? Vipi hauna siri uliyoitunza kuhusu mali zako au chochote unachohisi labda kimejulikana?
Asante mkuu kwa maswali na tafakari yako fikirishi
Kiukweli sidani kama nina adui serious ambaye anaweza kundhuru, sidhani kama yupo. Kutofautiana na watu ni jambo la kawaida maishani lakini si kwa kiwango cha kunipa hofu ya kudhurika
Kumuamini mwanamke ni jambo nitakalofanya mwishoni kabisa, usimuamini mwanamke kwa zaidi ya 60%. Lakini wake zangu wanaishi pamoja, na wanaishi vizuri kabisa - to the best of my knowledge
Pesa, utajiri na kufanikiwa kuna siri zake, lakini namshukuru Mungu kwamba sina nilichokipata kwa mambo meusi wala ya ajabu. Tunashirikiana na hawa viumbe kuendeleza familia, so biashara, mikopo na kudunduliza ndo nguzo ya mtaji na kufanya yaliyoko ndani ya uwezo wetu
Ni hayo tu mkuu