Msaada Nataka kwenda Marekani kutafuta maisha

Msaada Nataka kwenda Marekani kutafuta maisha

Jamani nataka kwenda Marekani kutafuta Maisha nauli ninayo kwa anaejua Prosees za kufika kule na michongo ilivyo amtired Bongo maana sina ndugu yeyote anaekaa ulaya naombeni msaada jamani

Dogo nikuambie kitu hakuna maisha mazuri kama hapa nyumbani fanya kazi kwa bidii tafuta pesa popote ilipo kihalali bila kukata tamaa manake ukiwa na imani na juhudi utayafikia malengo, utanunua kiwanja utajenga nyumba nzuri , garden yako saaafi , pembeni una kavitz, utakwenda popote bila kubugudhiwa hela yako tu ukitaka kuishi kama ulaya unaweza mdau kujituma tu na malengo na usikate tamaa.
 
atanielewa kama ana HITAJI KUBADILISHA MAISHA YAKE MAANA NAULI,KUPROCESS MPAKA UJE UPATE MAKARATASI NA MAMBO YA HAPA NA PALE NI MTAJI MKUBWA SANA

Na mimi naruhusiwa kuku pm? nina mchongo nataka kukupa pia 😉
 
Marekani bila kuwa na skills zinazotambulika kwenye system utaishi kwa stamp wewe na kizazi chako chote.
 
Kama huna mipango wala pa kufikia hadi hapo Visa hawakupi, afu pembeni ya nauli ka huna angalau hata 10M marekani utapakimbia mapema sana.. N usidhani ukifika kazi unapata papohapo, wapo wamarekani wengi tu kazi hawana na si kua hawana ujuzi flani, what makes u think u can do better uweze kusecure job ya kukuwezesha angalau kupata msoc na sehemu flani ya kujiegesha kwa muda hadi mambo yatakapokua mazuri??

Alafu hadi leo unachanganya marekani na ulaya hadi hapo kazi unayo, tena kazi kubwa sana aisee.. Ushauri, movie zisikuharibu, na story za mtaani ati fflani alienda marekani sa hvi kajenga nyumba, mambo si mepesi ka unavofikiria
 
Kwanini unatamani kwenda Marekani wakati bongo hauna hata kaya?
Jitume hapahapa bongo utatoka tu! Singa Singa
 
Last edited by a moderator:
Marekani sio ulaya.

Michongo ya America unahitaji hela kweli, tafuta mjanja hapa ambaye yupo America akutafutie demu kule America ambae ana chapa kazi kiukweli, akuunganishie aje bongo, funga ndoa, zama nae embassy mukaombe visa, ukiramba, unatambaa nae. Kama demu utachukua jumla jumla sawa kama business tu mtaarishie $5000. Huo Ndio mchakato safi,na ukifika huko hakuna ku struggling kama mkimbizi

U mean dola elfu 5 !?? Vipi issue ya kumleta gharama na hiyo ndoa ya magumashi? Wanawake wengine bandidu wanaweza kukugeuka mkishafika huko America!
 
marekani..ulaya...popote
ningekuwa wewe ningejichimbia ma wilayani kwenye fursa....
Huko uendako utapata mahitaji muhimu tu.....
Lakini ni bahati sana kumiliki uchumi. Makato ni mengi..hakuna 'loophole' kama hapa bongo.....

Mzalendo nipe wilaya moja nijichimbie namie nifaidi fursa.
 
Jamani nataka kwenda Marekani kutafuta Maisha nauli ninayo kwa anaejua Prosees za kufika kule na michongo ilivyo amtired Bongo maana sina ndugu yeyote anaekaa ulaya naombeni msaada jamani

Mbona hapo ulipo tayari ni ulaya? Tena ni marekani ndani ndani kabisaaaa, wewe jipange vizuri tu ili uishi ki ulaya ulaya ya hapo ulipo.
 
marekani..ulaya...popote
ningekuwa wewe ningejichimbia ma wilayani kwenye fursa....
Huko uendako utapata mahitaji muhimu tu.....
Lakini ni bahati sana kumiliki uchumi. Makato ni mengi..hakuna 'loophole' kama hapa bongo.....

Hakuna kuishi kiujanjajanja kama bongo kule sheria ni msumeno haswa.
 
Naamini huko unakoenda TigO haitakamata..make ikikamata tu..uanaume unapotea..
 
Binafsi nimejenga kimjengo kidogo lakini cha kisasa na hakijazidi 15million.sina gari lakini nina mountain bike yangu kama yawazungu na ninaipenda sana,niko jijini Mwanza na ninakula samaki naemtaka..kiukweli sioni kama walioko Marekani wananizidi chochote..Penda nchi yako na kuitangaza kua inafaa mahala popote
 
Jamani nataka kwenda Marekani kutafuta Maisha nauli ninayo kwa anaejua Prosees za kufika kule na michongo ilivyo amtired Bongo maana sina ndugu yeyote anaekaa ulaya naombeni msaada jamani

Naomba nikupe ushauri wa bure, tumia hiyo nauli yako kama mtaji, waweza hata kujiingiza kwenye kilimo na ukapata faida kuliko kwenda huko Marekani, jua huko kwao kupata kazi ni changamoto, zile kazi zilizokuwa zinaonekana kufanywa na wageni zamani leo hii zinafanywa na wazawa. Hapa TZ maisha yanawezekana ni kujituma tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom